Hongera Kamanda Kova - Kaza uzi ule ule! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera Kamanda Kova - Kaza uzi ule ule!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 11, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 11, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Nipashe
  Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Selemani Kova, amesema miongoni mwa vitu vinavyomkosesha usingizi ni vitendo vya uhalifu, biashara ya dawa za kulevya na suala la wapiga debe na vibaka, lakini amedai kuwa amepunguza uhalifu huo kwa asilimia 50.

  Alisema hayo jana ikiwa ni siku 100 tangu ashike wadhifa huo wenye changamoto nyingi akitokea mkoa wa Mbeya.

  Alikuwa akizungumza na Nipashe katika mahojiano maalumu kuhusu mipango yake ya sasa na ya baadaye katika kupambana na uhalifu na suala la wapiga debe.

  Alisema hivi sasa uhalifu uliopo ni wa kuvizia lakini sio kama ilivyokuwa huko nyuma ambapo wahalifu walikuwa wakitamba.

  Alitoa mfano kwamba kuanzia Jumatatu wiki hii hakuna tukio lolote la uhalifu lililoripotiwa kwake, jambo ambalo anaamini kwamba kazi ya kupambana na uhalifu imefanikiwa.

  Akitoa takwimu, Kova alisema, jumla ya vibaka 3120 walikamatwa katika msako maalumu jijini, wapiga debe 1586, watuhumiwa wa dawa za kulevya watu 3109, wauzaji wa bangi 1537 na pombe haramu ya gongo 1490.

  Alisema takwimu hizo ni mpaka jana na kwamba bado mkakati wake wa kupambana na uhalifu uko pale pale.

  Alifafanua kuwa kilichomsaidia kufikia malengo yake ni mbinu ya kuwashirikisha wananchi ambao anawatumia kufichua wahalifu katika maeneo wanayoishi.

  Kova alisema, ameandaa kompyuta maalumu ambayo wananchi wanapomtumia ujumbe mfupi kupitia kwenye simu zao za mkononi kufichua uhalifu hufikia humo na kuhifadhiwa na baadaye anaufanyia kazi haraka.

  Alisema ujumbe huo unatakiwa kutumwa kwenda namba ya simu 0785034224 na kwamba kila mwananchi anayetoa siri za uhalifu anahifadhiwa jina lake.

  Kwa upande wa nidhamu kwa askari wake alisema, wale wenye mchezo wa kuwabambikia kesi wananchi siku zao zinahesabika.

  Alisema enzi za kubambikia wananchi kesi zimepitwa na wakati na yule atakayebainika atajuta kwa nini alifanya hivyo ili mradi wananchi wampatie taarifa sahihi.

  Kuhusu uhalifu, alisema watu wenye ndoto za kufanya uhalifu kama njia ya kupata utajiri wamechelewa na hivi sasa hawatafanikiwa.

  Aliwataka watu wa namna hiyo kubuni na kufanya kazi za halali zenye kuwapatia riziki badala ya kuendelea kuwabugudhi wananchi.

  Aidha, Kova alisema amebaini njia inayotumiwa na vibaka wanaoandamwa ambapo wanavizia wananchi kwenye purukushani za kugombea daladala na kuwaibia mali zao.

  Alisema kutokana na hali hiyo, jeshi la polisi kanda ya Dar es Salaam, linatarajia kuanzisha utaratibu wa wananchi kupanda daladala wakiwa kwenye mstari.

  Kamanda Kova alisema, hilo linawezekana kwani hata nchi jirani ya Kenya inafanya hivyo na kwamba hatua hiyo itasaidia kuondoa wizi wa simu na fedha kutoka mifukoni.

  Aliwashukuru wananchi kwa kutoa ushirikiano kwa polisi katika kufichua uhalifu na kwamba kila askari atakayejituma kupambana na majambazi kwa ujasiri atapata zawadi anazotoa kila mwezi.

  My Take:
  Uongozi si maneno tu bali ni vitendo pia. Na vitendo vinaweza kupimwa. Kwa mtindo huu nampigia debe Kova. Kwa wanaokumbuka tulizungumza na Kamanda huyu akiwa kule Mbeya mara baada ya soko la Mwanjelwa kuungua. Ni mtu anayetoa ushirikiano mkubwa sana kwa waandishi. Swali je, upele umepata kucha Dar? Only time will tell. Lakini kupunguza uhalifu kwa asilimia 50 ndani ya siku mia moja, si utani!!
   
 2. M

  Masatu JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hii iende kwenye habari mchanganyiko....
   
 3. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2008
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,718
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha....teh teh teh....,bwaha ha ha
  Omba kazi ya umoderator.
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hey! yamekuwa haya?
   
 5. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #5
  Sep 11, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu can't you take a joke....si unaona mwenzio amenza na kicheko cha nguvu; inaashiria burudani kwenye bulogu.!!
   
 6. M

  Masatu JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Im joking as well cant u see it?
   
 7. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Suala la wapita debe ndio nini ? Wapiga debe wamefanya nini? Nipashe kwa kupasha!

  Halafu mbona hakuna suala la mauaji ya ujambazi hapa? Hii inaweza kuwa ni smokescreen ya huyu chifu.
   
 8. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Yah,anastahili pongezi kwa mafanikio ya KUKAMATA DAGAA wakati MAPAPA wanaendelea kutanua.Wengi wa wapiga debe ni uzao wa social and economic injustices zinazosababishwa na ufisadi.KUkamata mawakala wa kuuza unga bila kugusa wafadhili wa biashara hiyo hakuwezi kumaliza tatizo la mihadarati.
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Huyu kiranja ni Mtanzania mwenye uchungu na nchi yake na watu wake ,na naamini katika kichwa chake kuna mstari unaosomeka...kwa nini kwenye nchi nyengine inawezekana kuzuia ujambazi kwa wananchi wa kawaida,kuna nchi husikii majambazi kuvamia duka na kuiba kadi za simu au kuvunja nyumba na kuiba redio na tv au kukwapua simu za mikononi ? Au kuvizia vichochoroni na kumkaba mtu na kumuibia vijisenti vya kupandia daladala au kumvua viatu.
  Hivyo kwa kamanda huyu anastahili pongezi kwa kuwa amsha majambazi kuwa wakati wa kuiba tv na cadi za simu au kumvua mtu saa na viatu umepitwa na wakati kwani kero hizo sasa kwa nchi nyengine zimebaki kama historia.
   
 10. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #10
  Sep 12, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Hongera kamanda
   
 11. W

  WildCard JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Ina maana Mzee Tibaigana hakuwa anafanya kazi hadi uhalifu ukafikia 100%?
  Tusifanye kazi za UMMA kama wale wanaoanzisha madhehebu mapya akina Kakobe, Mwingira, Lusekelo,...Wao wanadhani wanamjua Yesu kuliko akina Pengo, Malasusa, Kilaini, Mokiwa ....
   
 12. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2008
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  only time will tell!!
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Sep 12, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwenye opetty crime anaweza kuwa anafanya vema, wasi wasi ni kuwa matukio ya ujambazi yanaanza kurejea kwa kasi ya kutisha shaka. Siku hizi wamebuni mbinu ya kuvamia maduka yanayouza vitu vya bei ghali ambavyo vina soko sana. matukio kama haya kwa muda wa wiki mbili zilizopita yamekuwa yakitokea sana katika maeneo ya Mikocheni na Masaki
   
 14. M

  Major JF-Expert Member

  #14
  Sep 12, 2008
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 1,425
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  NAa hili ni tatizo kubwa sana kwa viongozi wa Tanzania kila mtu kufanya kazi kivyake na kujisifia kivyake yaani hawako ki team na ndiyo maana leo unakuta eti mkapa na mwinyi hawaivi mwinyi na nyerere walikuwa hawaivi,tena mkapa na kikwete hawaivi sumaye na pinda hawaivi lowasa na sumaye hawaivi, sasa kwa mtindo huu hivi kweli hii itakuwa ni nchi au kichekesho na ndiyo maana tumeshindwa kuwa na mipango endelevu maana kila mtu analipuka na mpango wake mpya, haya leo iko wapi mvua ya lowasa?ile mipango ya mkapa iko wapi?je na ya sumaye iko wapi,yaani kwa kweli ni kichekesho
   
 15. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #15
  Sep 12, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji,

  Hizo takwimu hapo juu zinatia kichefuchefu. Wapiga debe, watuhumiwa wa madawa ya kulevya, wauza gongo na wauza bangi ni wengi wao ni watu wa hali ya chini sana na wanaishi maisha ya kubahatisha sana! Kwa hiyo kwao kubambikiwa kesi na polisi ni jambo ka kawaida. Hebu niambie ni wangapi kwenye hilo kundi ana uwezo wa kuweka wakili kwenye kesi yake? Polisi wa Dar wanaongoza kwa kubambikia watu kesi!

  Matukio ya ujambazi yameanza kurudi tena kwa kasi Dar, wizi wa magari, uvunjani wa nyumba za watu (bulglary) mbona hajazumzia?

  MY TAKE:
  Kwa mtazamo wangu UBORA wa utendaji mzuri wa kazi wa afisa wa serikali ambaye kazi yake ya kila siku inayagusa moja kwa moja maisha ya Watanzania unatakiwa uonekane moja kwa moja kwa wananchi wenyewe, na wala yeye hatakiwi kwenda kwenye vyombo vya habari na takwimu za kuletewa mezani na kujidai kwamba ni mchapa kazi. Huo ni unafiki. Namba za simu kwenye vituo vya polisi kwanini hazifanyi kazi mpaka leo? Kwanini watu wapige simu kwenye namba ya simu ya mkononi ya askari?

  Kamanda Kova, tunataka kuona polisi wa doria mitaani wakati wa mchana na usiku, simu za mezani zipokelewe kwenye vituo vya polisi, polisi waadilifu na wasio bambikizia kesi watu wanyonge, polisi wasioshirikiana na majambazi. Kwa kifupi huduma ya polisi kwa jamii ikiwa bora wananchi wenyewe tutasema, hatutaki TAKWIMU tunataka VITENDO!
   
 16. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #16
  Sep 12, 2008
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  [/B]

  Kova ni mtu anayependa kufanya kazi na vyombo vya habari kwa hilo tunampongeza kwa kuwapa ushirikiano wa kutosha wanahabari.Kuanzia mbeya kwa wachuna ngozi na wasafirishaji wa madawa ya kulevya hadi dar kwa wapiga debe.Hata tibaigana hakuwa mbali na vyombo vya habari, na waandishi walikuwa wakiridhika na ushirikiano waliokuwa wakiupata toka kwake.Halafu jamani naomba mnisaidie labda mi sielewi vizuri,kuna tofauti gani kati ya madawa ya kulevya na bangi?mimi navyojua bangi ni madawa ya kulevya, ama!!!??
  Jambo la msingi hapa ni hali halisi ilivyo mmitaani, sio hizo takwimu.Uzoefu unatuonyesha kuwa serikali hupenda kutumia takwimu kuonyesha mafanikio wakati hali halisi sivyo.Mbona katika hizo takwimu hakuna majambazi?au hawajakamatwa?au keshawamaliza?Jana tumesoma hapa kuna meneja mmoja wa kampuni ya UNILEVER kavamiwa na kuuawa,sasa hao wanovamia na kuua ni vibaka au wapiga debe?
  Mi nadhani ni mapema mno kova kusema kuwa amepunguza uhalifu kwa 50%, hizo takwimu zake zina walakini.
  lakini kama walivyosema wenzangu, TIME WILL TELL.
   
 17. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #17
  Sep 12, 2008
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  ndugu yangu vipi!
  una ugomvi na hao waungwana??
  kwasababu nijuavyo mimi kila mtu kwa imani yake ya dhehebu lake la kikristo,anaamini kuwa yuko sahihi.
  sasa unaposema hao waungwana wanawadharau wenzao sijui inakuwaje hiyo!!
   
 18. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #18
  Sep 12, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Hongera ya nini? Mkjj sasa unapoteza imani za watu kwako au una-kainterest fulani kwa Kova, hebu fikiria figure hizo za wauza gongo, wapiga debe, dawa za kulevya na wa baaaaangili !!! Kova atatatua au atalimaliza tatizo? watu hawana ajira wafanye nini kama sio kuuza gongo kwa wapiga kura wenzao? watu wamepigika choka mbaya kuanzia kijijini mpaka mjini leo usitoe chochote kwa mpiga debe kila siku utaziba pancha,umaskini umetopea na watoto wa mafisadi ndio angalau wana vijisenti vya baba zao hivyo basi ili tugawane ni lazima hao wafundishwe kula msuba dope ya bei mbaya ili tu walete vijisenti huku uswazi, ni vicious cycle ambayo haiitaji nguvu za kova bali the wright community aproach or problem centred,kumbuka nguvu zile zamani za mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kuwafukuza nduguze kutoka pale Kisutu pamoja na kutumia vyombo vya dola lakini alifeli kwani wakati ule wa shida nyingi hasa kule kwao mpakani kulikuwa hakukaliki na matokeo yake wakatawanyika lakini hawakutoka Dar na wapo mpaka leo wanaendesha biashara yao kama kawa pamoja na kuwa na gonjwa jipya. Hawa vibaka kamwe hawataisha kwani hakuna msukumo wa dhati toka kwa viongozi wa kisiasa na Kova ataendelea kukamata mpaka na yeye atamfuata Tibaigana kwenda omba ubunge kijijini kwao
   
 19. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #19
  Sep 12, 2008
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Dawa ya kuondoa kero ya mti unao chafua mazingira ni kuukata wote hadi unachimbua na shina lake (mizizi) sio kupunguza matawi yake. Ningemsifu kama angengoa mizizi kwanza.
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Sep 12, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni watu kuishi katika nchi ya kufikirika. Upolisi siyo siasa. Katika kupambana na uhalifu kuna vitu unapanga na kuanza kufanya. Kutotambua na kukubali hatua zilizochukuliwa ndani ya siku mia moja na kupungua matukio ya uhalifu kwa asilimia 50 ni kujaribu kuficha kichwa mchangani.

  Watu wengi hawakabiliani na ujambazi kila siku au mauaji kila siku. Lakini wanapambana na vitu ambavyo watu wanaviita petty crimes ambazo kwa kweli nuisances za kila siku. Siku moja nikiwa nimeketi kiti cha nyuma cha daladala kuelekea Ubungo tulipofika pale Manzese (msufini) nikiwa nang'aa ng'aa macho kibaka akapita karibu na kuchomoa miwani yangu na kutokomea nayo! Ile ilikuwa ni kero!

  Lakini ukweli pia unabakia kuwa a lot need to be done. Kova au mtu mwingine asioneshe kana kwamba tayari uhalifu umetoweka au vita vimepiganwa na tumeshinda. Lakini ni wajibu kusema kuwa tunatambua jitihada hizo, tunazikubali, na tunamtia moyo Kova kwenda na kufanya zaidi. Tukimtia moyo na kukubali msije kushangaa siku moja vijana wake wanagonga mlango kwa mwanasiasa na kumtia pingu. Polisi wakijua watu wako nyuma yao wana uwezo wa kufanya makubwa.

  I Support Kova!!
   
Loading...