Hongera Kamanda Kova - Kaza uzi ule ule!

Vyovyote vile kuna kazi imefanyika hata kama ni kidogo! wengine tunakaa uswahilini hali ilikuwa noma, roba kila kona na mateja wanavamia na kuiba. Ukizungumzia mapapa hayo tulikuwa tunayasikia sababu huku kwetu uswahili wanaosumbua sana vibaka majambazi dili zao hakuna.

Ukitoka aljajiri lazima wakudandie sasa kama siku hizi shwari inamaanisha kuna kazi imefanyika. Uhalifu hauwezi kwisha mbona Uk watu wanavamiwa manake magazeti ya leo yanasema Keane kaibiwa home, lazima atakuwa anakaa prime area na security si ya kitoto.
 
Mzee ni vyema umerudi tena. nakumbuka wakati fulani ulisema umeamua kunga'tuka baada ya hotuba ndefu ya mtukufu Rais kutokidhi haja yako na wengine wengi. Karibu tena.

Nimjuavyo mimi Kova ni mshirikishaji mzuri wa wananchi. Na hii inasaidia kupunguza matendo yote ya uhalifu. Kwani wahalifu huishi miongoni mwa wananchi. Hii ni changamoto kwetu wanajamii kumsaidia yeyote mwenye mapenzi mema na nchi.
 
Hata wananchi wanastahili pongezi kwa kuwachoma vibaka mwitu ,ambao wanatisha sana mitaani tofauti na wale wanaovamia majiduka makubwa wasiotoa zaka ,vibaka mwitu wakipungua na kutoweka basi mambo yatakuwa si mabaya , ni kama alivyosema vibaka watafute kazi ya kufanya na sio kunyanyasa watu wanaopokea mishahara ya vibarua , mishahara ambayo hata ukiipangia mikakati ya kupata mlo wa siku basi utaikuta haitoshi ,halafu kibaka mwitu anakukwapua ,si ndio anakuwa amekupa mtihani mkubwa wa mwezi mzima, naona Kova awashauri wananchi nao wazidishe kuwawasha moto vibaka mwitu ili kumsaidia kazi kwa upande fulani.
 
Tokea 2008 hadi 2015...

nampongeza kwa kupanda cheo... lkn bado malengo mengi hayajatekelezwa.
 
Nampongeza ameongeza malori yake ya kubeba mizigo kupeleka nchi za nje madereva wake wanavunja sheria ukiwakamata wanampigia Kova.Kwa ujumla ni mtu wa ajabu sana
 
Kazi yoyote, hata kama ni ya kuuza majeneza, ukishateuliwa na mwanasiasa basi sishangai ukaitukana mochari pasi kujua siku moja nawe utakua maiti! Kova aliitwa Kova enzi hizo za uwajibikaji ila sitamkosea adabu kamanda wetu nikimwita msemaji wa propaganda za chama cha mapinduzi!
 
Hili nalo ni kweli Kova kwa sasa ni kama kaanzisha tawi la ccm polisi kanda maalum.Yaani utendaji wake juu ya ccm ni zaidi ya Nape na Kinana
 
Back
Top Bottom