Hongera CMA kwa kuendesha kesi na Migogoro Makazini kwa weledi

Kugosola

Senior Member
Aug 7, 2021
191
261
Leo tarehe 19 Agosti, 2021 nimeweza kusikiliza kipindi cha CMA - Commission for Mediation and Arbitration kilichorushwa na TBC.

Katika mahojiano hayo yaliyoendeshwa na Lusekelege Mpula wa CMA ambae ni Afisa Mfawidhi wa CMA Kanda ya Dar, ameweza kueleza ni jinsi gani CMA imejikita kuhakikisha kuwa kesi zote za makazini zinamalizwa kwa wakati bila kukiuka sheria, na hilo wameweza!

Pia ameweza kueleza kuwa kwa kipindi cha mwaka 2020 wameweza kutatua migogoro ya kwa 76% ikijumuisha migogoro ya wafanyakazi waliofukuzwa kazi ambapo inaonekana kuwa wafanyakazi wengi wamekuwa wakifukuzwa kazi kimakosa na kwa kuonewa na waajiri.

Nawapa hongera sana CMA kwa kusimamia haki kuhakikksha kuwa haki ya mtumishi inalindwa, haiporwi kama Mamlaka zingine zinavyofanya uporaji wa haki za watumishi.
 
Afadhi Mfawidhi wa CMA Kanda ya Dar, amesema kwa Sheria mpya inawapa Mwakili mamlaka ya kusikiliza na kuamua migogoro makazini badala ya kuwatumia tu CMA - Hongereni sana CMA kwa hilo najua kesi nyingi za watumishi zitaisha ndani ya muda mfupi zaidi na hivyo kulinda haki ya mtumishi.

I wish, hata Mamlaka zingine za Rufaa wanakokata rufaa watumishi zingeiga utaratibu huo wa CMA.
 
Juzi kulikuwa na uzi wa mdau akiwashutumu tume ya utumishi wao wanalalamika work load kubwa hawa CMA wao mbona wameweza?
 
Hakuna uhalisia kwa unachodai ni nadharia tupu. Watu mko rahisi sana kupindishwa uelewa kwa maneno matamu wakati vitendo hujaoneshwa na kupata ushuhuda usiofungamana na mtu uliyekuwa unamsikiliza ili kuthibitisha kile kilichoelezwa ndiyo kinatendeka.

Sheria mpya ipi? ELRA ya 2004 na kanuni zake za 2007 pamoja na marekebisho kwenye vipengele kadhaa kwa miaka tofauti hadi sasa tangu sheria ya mahusiano kazini na kanuni zake zilizotungwa na kuanza kufanya kazi?

CMA ni porojo tupu
 
Hakuna lolote wamejaa rushwa na udalali kwa waajiri ,umesikia ukasema wako POA nenda na kesi uone .wapuuzi Sana wale

USSR
Hata mm nilitaka kusema hao hawana msaada wowote ni polojo hakauna jipya
 
Hakuna uhalisia kwa unachodai ni nadharia tupu. Watu mko rahisi sana kupindishwa uelewa kwa maneno matamu wakati vitendo hujaoneshwa na kupata ushuhuda usiofungamana na mtu uliyekuwa unamsikiliza ili kuthibitisha kile kilichoelezwa ndiyo kinatendeka.

Sheria mpya ipi? ELRA ya 2004 na kanuni zake za 2007 pamoja na marekebisho kwenye vipengele kadhaa kwa miaka tofauti hadi sasa tangu sheria ya mahusiano kazini na kanuni zake zilizotungwa na kuanza kufanya kazi?

CMA ni porojo tupu
Hakuna division ya I mahakama ya hovyo Kama CMA ni wapuuzi na wezi Kama wezi wengine

USSR
 
Back
Top Bottom