Wakuu wa Wilaya na Mikoa ni chanzo Cha wafanyakazi kupoteza haki zao za kisheria

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,393
3,234
Nadhani ni jukwaa sahihi!

Mimi ni wakili wa kujitegemea ninayefanya shughuli zangu jijini Dar Es Salaam. Miongoni mwa kesi ninazokutana nazo ni kesi za migogoro ya kazi (Labour Disputes). Migogoro mingi ninayokutana nayo ni migogoro inayohusiana na mfanyakazi kufukuzwa kazi pasipo kufuata sheria na taratibu, madai ya mishahara na malimbikizo mengine na migogoro inayohusiana na terms za mikataba nk.

Sasa ipo hivi Kwa mujibu wa sheria nchini chombo chenye mamlaka ya kushughulika na migogoro ya wafanyakazi ni Tume ya Usuluhishi ya maswala ya kazi (Commission for Mediation and Arbitration-CMA). Sheria za kazi zimeweka muda maalumu ambapo mtu anatakiwa kupeleka mgogoro CMA, na muda huo ukipita basi mfanyakazi huwa nje ya muda wa kupeleka malalamiko CMA (Time barred). Kwa mgogoro wa kufukuzwa kazi kimakosa mfanyakazi anatakiwa kupeleka mgogoro CMA ndani ya siku 30 tangu alipofukuzwa kazi huku Kwa migogoro mingineyo ikiwa ni siku 60 tu tangu mgogoro husika uibuke.

Tatizo lilipo ni kwamba kumekuwa na huu utaratibu usio rasmi ambao wafanyakazi hupeleka malalamiko yao Kwa Wakuu wa Mikoa punde tu migogoro inapoibuka. Huu utaratibu umekuwa chanzo Cha wafanyakazi kukosa haki zao. Mfanyakazi hupoteza muda mrefu sana akisuluhishwa na mkuu wa wilaya halafu baada ya mwaka mmoja au miezi kadhaa ndiyo watendaji wa wakuu wa wilaya wanawaambia wafanyakazi waende CMA huku wakijua fika kuwa wapo nje ya muda.

Ingekuwa ni vema wakuu wa wilaya na watendaji wao wangewaelekeza wafanyakazi kupeleka malalamiko yao CMA kabla muda haujaisha. Bahati mbaya zaidi ni kwamba watendaji Hawa wa wakuu wa wilaya na Mikoa ni wanasheria hivyo wanajua wanachokifanya.

Imefika wakati inafanya tuhisi pengine labda Kuna rushwa au mchezo mchafu baina ya wakuu watendaji hao na waajiri kutumika kuwachelewesha wafanyakazi makusudi.

Niwashauri watendaji wa wakuu wa wilaya kuwaeleza wafanyakazi ukweli kuwa chombo chenye mamlaka ya kusuluhisha migogoro ya wafanyakazi ni CMA na si vinginevyo na kwamba muda unaohitajika kufanya hivyo ni mfupi mno.
 
Elimu inabidi iendelee kutolewa juu ya haki za wafanyakazi.

Viongozi wengi wanawajibikia matumbo yao, hawako kwa ajili ya kuwajibika kwa wananchi.
Inasikitisha sana wakati ilipaswa viongozi ndiyo watoe elimu Ili wafanyakazi wajue njia stahiki wanazopaswa kuzifuata matokeo yake viongozi wanawapotezea muda wafanyakazi.
 
Mimi mwenyewe ni wakili wa kujitegemea ila ni siasa tu sio kwamba wafanyakazi wote wanaoenda sehemu zilizotajwa hawajui uwepo wa Tume.
 
Back
Top Bottom