Hongera Chadema Bungeni, hongera Kitila Mkumbo...

Waberoya

Platinum Member
Aug 3, 2008
15,169
10,785
HONGERA CDM

Si rahisi kutoa hongera yangu kirahisi rahisi. Katika muda huu na nyakati hizi, natuma salamu za Hongera kwa wabunge woote wa CDM Dodoma. Kazi nzuri, hoja nzuri, mmejipanga vizuri sana. Pia peongezi kwa vyama vyote vya upinzani vyema malengo mema..recently nimeona NCCR mmejitahidi.

CDM Piganieni umoja ndani ya chama .....disunity should never be an option kwenu


HONGERA KITILA MKUMBO

However, ukija kwenye academic nampongeza sana Kitila Mkumbo kwa kuwa Promoted kuwa Senior Lecturer ...speed kubwa mkuu!!!

I am proud of you brother, najua majungu na fitina kwako mwiko,ENDELEA kuwa na roho nzuri...yees watu wanasema hivyo-una roho nzuri!


TIMU YA CHADEMA:

PAMOJA NA HIZI EVENTS AU TOPICAL ISSUES....Please msirogwe hata siku moja kuondoka kwenye ile line ya kudai katiba.

wekeni at least kamati maalumu ambayo ikilala ikiamka itasema katiba.........wakati wa kula, kulala, kunywa, na mambo yetu yaale tusikie wimbo wa katiba!!!!! kamwe asitokee mtu wala msijisahau katika hili. Kuna upepo unaletwa makusudi kwani mabadiliko ya katiba ni sumu ya mafisadi na vizazi vyao.


WATUMWA HADI LINI?

Nchi ya Tanzania iko utumwani bado na uhuru tutaupata pindi tukipata serikali mpya na katiba mpya...hakuna jema chini ya CCM hii!!

wengi najua mnapoteza muda wenu adimu kufuatilia Kikwete kasema hivi au kile, wengi mlikesha kusikiliza hotuba ya Mkulo, wengi mnaamini kuwa CCM inaweza kuleta maendeleo,mimi na nyumba yangu kamwe hatutaki hata kuisikia CCM na mambo yake yooote.



Slaa nadhani ingekuwa muda mzuri kuendeleza ule moto wa katiba, your voice together with your MPs' voice-kule bungeni italeta kitu fulani kizuri..uko kimya kunani??
 
hongera mwandishi

hongera Dr Mkumbo.. wewe umekuwa icon katika jamii ya wasomi hasa pale umaposimamia hoja bila kuangalia makunyanzi...

by the way, will visit dar sometimes na i will call for a soup again close to fine travellers...

hongera tena kwa kuwa Seniour Lecturer.. a Professor in the making.
 
Kitila , hongera kijana . Nakutambua ulivyo na ndiyo maana wengi hawawezi kuhimili mapigo yako .Mwandishi asante . Chadema hongera .
Slaa ni kiongozi mkubwa na makini anaongea anapo ona kuna sababu hawezi kuwa kama Mrema kusema sema hovyo atazoeleka .Yuko makini anasoma na kutafakari nini kifanyike baada ya Bunge kuisha kazi bado sana .
 
Good ideas!
Bila kuficha cdm wamesaidia sana kuamsha wananchi juu ya hakizao na aina ya uongozi unaotakiwa kwa Tanzania ya leo!
 
- Sawa sawa, nimesema mara nyingi sana kwamba Dr. Kitila na Mwanakijiji, wanatakiwa kuwa sura ya the future of Chadema, Viongozi wa sasa wa Chadema wanatakiwa kuanza kuwatayarisha hawa kushika usukani huko!

Willie @ NYC, USA.

Sometime Willy unakuwa mkweli kulingana na nafsi na myo wako unavyohisi kwa wakati huo na husukumwi kwa hisia au ushabiki
Safi sana mkuu na endelea kufanya hivyo
 
Kwa kweli kinachofanyika kilitakiwa kifanyike kabla hata ya uchaguzi kuwanyanyua watanzania na kuwaeleza haki zao za msingi na kuwaonyesha yale wanayofanyiwa na viongozi waliowachagua
 
Tanzania mpya yaja, wakat, siku na mwezi upi? bado ni kitandawili ila ukombozi umekaribia, sijui nitakuwa hai? ooooooooooooooo...... yawezekana, CHADEMA tukaze buti. kila kukicha wimbo wetu ule ule, Katiba......katiba......katiba.
Hakuna ukombozi bila katiba mpya.....

Nilibahatika kusimamia uchaguzi 2010, yale niliyoyaona ...... dah....Jamani ukombizi bila katiba mpya hatuwezekana.

Kiktuoni mawakala watakuwepo......

Kwa katibu kata jeee...... Hakuna wakala wala mwakilishi....Ni mtihani sheeeee.

Sasa hapo kwa mkulugenzii..... ooooo sitaki niseme kwani niliapa.
 
Jenerali Ulimwengu alimshauri Dr. Slaa azungumze pale tu inapobidi.

Dr. ana hadhi ya mkuu wa nchi si vyema akaongea hovyo hovyo kila mara.

Kuhusu katiba hapo umenena Mkuu, hawa CCM wanajua watanzania ni wasahaulifu kwa hiyo si vyema kuacha moto wa katiba ukazimwa na jambo jingine lolote.
Kwa umuhimu katiba ichukue nafasi ya kwanza!
 
Back
Top Bottom