Hongera Chadema Bungeni, hongera Kitila Mkumbo...

Hongera Chadema Bungeni, hongera Kitila Mkumbo...

1. Bob Dr. Slaa na Mbowe, wameshindwa tayari na sio mara moja, sasa ustaarabu wa siasa uantaka kuwaachia wengine, kurudisha gari la ubunge sio dhana ya kua Rais mzuri, Zitto sio siri kwamba ndiye mbunge namba moja wa Upinzani mwenye heshima sana ndani ya bunge kwa uelewa wa ishus, Lissu ana style yake ya in your face ambayo ndio hasa hili taifa tunaiihitaji, kwa hiyo kama ni siasa ni wakati muafaka wa kuwapa na wengine nafasi sasa, baada ya kushindwa tayari!

2. Majimbo ya Kinondoni na Ilala peke yake hayatoi Urais, infact kuna majimbo ambayo Chadema hawakuweka mgombea kabisaa, idadi ya wabunge wa CCM na Chadema iko mbaali sana mkuu, ambayo inatakiwa kuwa mfano mdogo sana on kushindwa kwa Slaa, na ninasema tena sijawahi kumsikia Slaa mwenyewe akisema alishinda, ukweli ni kwamba Chadema mara nyingi nimeona wakitengeneza mazingara ya sababu za kutokea mapema kwa hiyo wakishindwa tu, haikua Demokrasia, wameibiwa kura, lakini wakishinda huwa ni saafi.

3. Well, uamuzi ni wenu mkuu, lakini kwa Chadema kwenda tena kwenye uchaguzi ujao na walioshindwa tayari yaani Slaa na Mbowe ni wenu, sisi wengine watazamaji tu!, ingawa kwa kuwa hapa ni uwanja wa maoni, ya kwangu ni kwamba panahitajika mabadiliko kwenye safu ya mbele, yaani sura inahitaji kubadilika kidogo!

Willie @ NYC, USA.
Unaona sasa unavyochanganya - tumefikia kubishana kisomali kumbe bado hujaelewa muundo wa Chadema kama chama!...CDM haifuati muundo wa CCM hata kidogo mkuu wangu.

Wewe unamtaka Mbowe aachie madaraka kwa sababu kashindwa na nimekuuliza kwa ushahidi gani? wewe unaenda katika maswala ya Urais? nani alikwambia mwenyekiti au katibu wa Chadema ndiye mgombea wa Urais?..Mkuu, Tunazungumzia kazi mbili tofauti hapa na maelezo yako yanaonyesha wazi unapotea.

1. Swala la uongozi wa chama:- Toka Mbowe amekuwa mwenyekiti, chama kimefanikiwa zaidi ya mara 500 toka aliporithi uenyekiti. Ujio wa Dr.Slaa kama katibu tumepata wanachama zaidi na wanazidi kujiunga kila siku..Na chama kinazidi umaarufu pengine kushinda hata CCM yenyewe. Sasa waache kwa sababu gani? - Prof. Kitila na M. Mwanakijiji wanaweza kujiunga kuongeza nguvu lakini sio kuachiwa uongozi wa chama wakati wao wana majukumu mengine ambayo pengine CCM inasubiri makosa kama haya wayatumie kuwadhoofisha wao au chama - They are smart than that!

SISI wanachama tunajua nani kiongozi bora wa chama kiitikadi tena nje kabisa ya Zitto wala Lissu kwa sababu hawa sii wanasiasa, hiyo kukiwasha bungeni ni ktk maswala ya mbunge ktk utunzi wa sheria, kupitisha budget na kazi za mabaraza yao kama wabunge ambayo hayawezi kuwa kigezo cha uongozi wa chama. Labda nikwambie tu kwamba Chadema inafuata mfumo wa Marekani ambapo rais wa nchi sio lazima awe mwenyekiti wa chama.

Sasa kama una maana Lissu au Zitto wagombee urais hakuna mtu Chadema anayewazuia kwa sababu wanafit kuongoza na pia hilo ni swala la wananchi wapiga kura kuwachagua. Nachopinga mimi ni maelezo yako kwamba Mbowe na dr.Slaa waachie hawa watu wengine ambao unasema wana mambo ya in your face... Mkuu hatutaki kiongozi wa namna hiyo kuongoza chama bali mwenye busara na hekima kutumia mrengo wa chama ktk kuhamasisha wananchi kujiunga au kuzikubali itikadi, sera na ilani za chama kama mwongozo unaoweza kuwaletea maendeleo na sii elimu ya darasa, CV na machachari ya bungeni. Ila ni vizuri kuwa na watu hawa ndani wanaleta challenge hata ktk msimamo wa baadhi ya maswala ya kiitikadi.

2. Swala la Chadema hawakusimamisha wagombea ktk majimbo fulani sio sababu ya wapiga kura kutomchagua rais, naona unachanganya vitu hapa. Kama jimbo halina Mbunge wa Chadema au chama chochote haina maana hata jina la mgombea Urais linaondolewa. Kwa hiyo jina la Dr.Slaa na wagombea wote wa urais majina yao yalikuwepo ktk majimbo yote na mwananchi uliweza kumchagua mbunge wako, kisha unamchagua rais kati ya orodha ya wagombea urais, hivyo hii sio sababu kabisa - Katika hili nadhani tumeelewana.

3. Utaendelea kuwa mtazamaji kwa sababu hutaki kujifunza kwamba Zitto, Lissu, Kina Kitila na wengineo wakitaka kugombea uongozi wa nchi wanaruhusiwa kabisa na pengine Mbowe na Dr.Slaa wasisimame kabisa kugombea ( kwa matakwa yao) lakini chama hakiwezi kubadilisha mgombea kwa sababu kuna watu wanafikiria Mbowe na dr.Slaa hawawezi kuleta ushindi tena kwa sababu za Ukabila na Udini. Kwa yeyote anayefikiria au kusema hivi basi yeye mwenyewe ndiye mwenye matatizo..
Kwenye FB nimeandika hivi - When searching for truth,look no further than yourself! ina maana kubwa zaidi mkuu wangu..
 
HONGERA CDM

PAMOJA NA HIZI EVENTS AU TOPICAL ISSUES....Please msirogwe hata siku moja kuondoka kwenye ile line ya kudai katiba.

wekeni at least kamati maalumu ambayo ikilala ikiamka itasema katiba.........wakati wa kula, kulala, kunywa, na mambo yetu yaale tusikie wimbo wa katiba!!!!! kamwe asitokee mtu wala msijisahau katika hili. Kuna upepo unaletwa makusudi kwani mabadiliko ya katiba ni sumu ya mafisadi na vizazi vyao.

Hili la katiba nakubalina nawe kabisa Mkuu. CHADEMA wasilinyamazie kabisa swala hili na kuwaachia chama cha magamba kujionyesha kama wana nia ya kweli ya kuandika katiba ambayo ina maslahi kwa Watanzania wote Wameshavurunda mara ya kwanza walikurupuka na kupeleka muswada haraka haraka bungeni na hawatashindwa kukurupuka tena ili kuandika katiba mabyo itakipendelea chama cha magamba

WATUMWA HADI LINI?

Nchi ya Tanzania iko utumwani bado na uhuru tutaupata pindi tukipata serikali mpya na katiba mpya...hakuna jema chini ya CCM hii!!

wengi najua mnapoteza muda wenu adimu kufuatilia Kikwete kasema hivi au kile, wengi mlikesha kusikiliza hotuba ya Mkulo, wengi mnaamini kuwa CCM inaweza kuleta maendeleo, mimi na nyumba yangu kamwe hatutaki hata kuisikia CCM na mambo yake yooote.

Nyumba ambazo ziko kama yako ambazo hawataki kusikia chochote kile kuhusiana na chama cha magamba zinaongezeka kila leo katika kona mbali mbali za nchi yetu. Tuombe Mungu kipigwe chini kwa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao


Slaa nadhani ingekuwa muda mzuri kuendeleza ule moto wa katiba, your voice together with your MPs' voice-kule bungeni italeta kitu fulani kizuri..uko kimya kunani??

Hapa nakubaliana nawe pia. Katika hili la kudai katiba mpya sauti ya Dr Slaa ndiyo inabidi iongoze madai haya na kuhakikiha katiba hii inapatikana at least mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015.
 
Back
Top Bottom