Hoja zangu za Kisiasa, Katiba, Sheria na Haki humu JF zina mashiko? Zimesaidia kitu? The Consequences ya baadhi ya hoja zangu! Kazi inaendelea!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,503
113,616
Wanabodi

Mimi ni mwana JF mwenzenu humu JF na ni verified tangu 2008, katika miaka hii zaidi ya 15, nimepandisha mabandiko mengi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Kati ya mabandiko hayo, kuna mabandiko ni powerful na yameleta some positive impact kwa kujibiwa kwa utekelezaji.

Hili ni bandiko la kufanya assessment ya baadhi ya mabandiko yaliyoleta impact kama hoja zangu zina mashiko?, zimesaidia kitu au ninaandika for nothing kupoteza tuu muda?.

Wakati ukitafakari na mimi pia najifanyia self assessment, kuna baadhi ya mada zangu huwa zinaandamana na ushauri wa a way forward na baadhi zina onyesha the consequences za kitakachotokea. Baadhi ya mabandiko yangu yenye matokeo nimeyazungumza hapa "Ombeni Mtapewa", "Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je, Wajua Kuna "Kauli" na "Kauli Umba" Ambazo Huumba? Shuhudia

Kwa vile mwandishi ni mimi, karibu kila bandiko langu lina the drive force, the motives behind and the intended consequences, yaani naandika ili nipate nini au hilo bandiko lilete matokeo gani chanya.

Sasa from now on nitakuwa na share na nyinyi the motive behind ya baadhi ya mabandiko yangu na the intended consequences ya mabandiko hayo na kuitumia hiyo consequences au matokeo hayo as the drive force behind me kuendelea kuandika kwa kuthibitisha sifanyi kazi bure na kazi iendelee!.

Hapa kwenye bandiko kuu nitaweka line up ya mabandiko yenye big impact only halafu uchambuzi utafuata kwenye individual posts.

Na hii ni lineup ya mabandiko yote
Inaendelea
Paskali
 
Umekuwa na uandishi traditional kwa muda mrefu, nakukumbusha kwamba Kuna YouTube pia ambako Kuna watu wengi, umesahau kwamba ukiweka jambo kwenye maandishi mwafrika halisomi?

Asili ya mwafrika ni kupashana mambo kwa fasihi simulizi, hizi za maandishi si asili yetu
 
Zinaweza kuonekana zina matokeo au laa,kwa muda fulani,sio lazima iwe muda huo huo.Mwandishi wa kitabu cha "Wreck of titan" bwana Morgan Robson aliandika riwaya tu,lakini baada ya ajali kubwa ya meli ya Titanic iliyokuwa ikitoka Uingereza kwenda USA,iliwaacha watu midomo wazi na kubaki fumbo mpaka sasa juu ya kilichomo kwenye kitabu na utokeaji wa ajali hiyo.

Hivyo basi maandishi yako yanaweza kuja kuwa na maana kubwa sana iwe sasa au baadaye, maana muda ndo hakimu mzuri.
 
Kuhusu bandiko hili Madudu ya Ajabu ya Ubatili wa Katiba Yetu, Mabadiliko Fake ya Sheria na Tume ya Uchaguzi, Rais Samia Asilaumiwe Kwasababu Yeye Sio Mwanasheria!. The motive behind ni kumfungua macho Mama, asiwategemee sana wasaidizi wake tuu, kwa kuwaamini wana uwezo na wanamsaidia, hivyo hapa nimeonyesha jinsi baadhi ya hao anaowategemea wasivyo na uwezo kwa kuyaweka baadhi ya madudu walivyofanya kule nyuma hivyo asikilize na ushauri wa nje ya washauri wake ili alisaidie taifa letu.
Mzizi wa ukosefu wa haki kwenye demokrasia changa ni katiba kwanza ndipo tuje kwenye sheria.

Kumuonyesha rais wetu madudu ya washauri wake na vyombo vyake Bunge na Mahakama, kutamuwezesha kuona mwanga zaidi hivyo kuwapatia haki bin haki Watanzania.

Kama baada ya Rais Samia kuiona hii dhulma kubwa Watanzania waliotendewa na yeye akaamua kuiacha iendelee kwasababu imekuwapo kwa watangulizi wake wote, then uchaguzi utakuwa ni as usual, nothing will happen to her hata akiacha the usual practices ila akiamua kubadilisha, then atabarikiwa sana!.
P
 
Zimesaidia sana na wala siyo kidogo .mimi binafsi nimekuwa nikisoma makala zako kwa miaka mingi sana kabla hata ya kujiunga humu maana nilianza kusoma habari za jf tangia mwaka 2013 hapo .jf ndio jukwaa langu pendwa na wewe ni miongoni mwa watu walionifanya niipende jf na kuifuatilia vyema habari zinazoandikwa humu.

Makala zako pamoja na za akina mzee mwanakijiji wakati huo akiwa active Sana nilikuwa nasoma sana.ndio maana mwaka jana nikaamua kujiunga Rasmi ili nami nianze kuchangia mijadala.ndio maana mimi nimeingia nikiwa sitetereshwi na wanaonitukana matusi kwa kusema mimi ni chawa msaka uteuzi ,mlamba viatu 😄😄😄maana matusi nilikuwa nayasoma humu pia.

Niliingia nikiwa najua jf ni jukwaa la aina gani na lina watu wa aina ipi.kwa hiyo kupitia wewe na wengine nimeingia nikiwa na uzoefu wa mijadala ya humu na namna inavyohitaji ngozi ngumu katika kukabiliana na watu wanapokushambulia kwa matusi,kejeli na udhalilishaji. Mungu aendelee kukubariki na uendelee kuandika zaidi na zaidi maana katika kila andiko uandikalo kila mtu atabeba na kuelewa kile alichoelewa kulingana na upeo wake,mtizamo wake na upande anaouamini.
 
Bandiko hili Tujifunze kuwa na Shukrani kwa Madogo ili Tupatiwe Makubwa!. Japo Tulitaka Kikubwa, Tumepewa Kiduchu!, Tukipokee Tushukuru, au Tususe Kudai Kikubwa?. hili ni bandiko la ushawishi kuwashawishi tuwe watu wa shukrani kwa kukubali chochote tunachopewa na serikali yetu. Tulitaka katiba mpya ili tuibadili sheria ya uchaguzi na kuunda tume huru ya uchaguzi, kabla ya uchaguzi Mkuu wa 2025, na kwavile muda uliobaki kabla ya 2025 ni muda mfupi hautoshi kwa mchakato wa katiba mpya, tukashauri tufanye mabadiliko ya katiba hii hii iliyopo kwanza ndipo twende kwenye sheria na tume huru ya uchaguzi. Tumeletewa sheria tuu bila mabadiliko ya katiba, hivyo kuwashawishi Watanzania tukubali kupokea hiki kidogo tulicholetewa kisha tuendelee kutafuta kile kikubwa.
P
 
Shida huwa unaandika kwa kuzunguka saaanaaa. Mtu akisoma mabandiko yako mengi huwa anashindwa kupata points directly kwa sababu maelezo yako huwa yanajicontradict..

Na hilo linathibitishwa na wewe mwenyewe leo hii unarudia mabandiko yako na kuyatolea ufafanuzi ulikuwa una lenga nini.

Punguza kuzunguka sana. Heading zenyewe tu unaweka ndeeefu sana. Jaribu kuanza kwenda straight kwenye point.

Cha mwisho, punguza kujibaraguza na uchawa..
 
Bandiko hili Ushauri kwa Rais Samia: Kwenye mabadiliko ya Cabinet kufuatia Ripoti ya CAG, tumia wazoefu; Fedha mpe Dkt. Kimei, Biashara Uwekezaji mpe Deo Mwanyika ni ushauri kwa mamlaka ya uteuzi kuwatumia more able people waliopo wenye experience in delivery na sio kuangalia watu wa masifa wenye mavyeti makubwa ya usomi lakini delivery ni sifuri!.
Maji hufuata mkondo, the law of attraction applies money attracts more money, Wizara ya fedha apewe mtu wa kihela hela kutoka makabila ya kipesa pesa ili kuvutia fedha zaidi. Kuna makabila tajiri na makabila masikini, ukimpa masikini issue ya kuvutia utajiri, atavutia umasikini!.
P
 
Katika sakata la mkataba Ule BATILI,

Umeshiriki Kwa kiasi kikubwa kulizamisha Taifa Kwa Maslahi Yako binafsi na kikundi kidogo.

HAKIKA, IPO siku utalipia.
 
Wanabodi

Mimi ni mwana JF mwenzenu humu JF na ni verified tangu 2008, katika miaka hii zaidi ya 15, nimepandisha mabandiko mengi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Hili ni bandiko la kufanya assessment, jee hoja zangu zina mashiko?, zimesaidia kitu au ninaandika for nothing kupoteza tuu muda?.

Wakati ukitafakari na mimi pia najifanyia self assessment, kuna baadhi ya mada zangu huwa zinaandamana na ushauri wa a way forward na baadhi zina onyesha the consequences za kitakachotokea.

Kwa vile mwandishi ni mimi, karibu kila bandiko langu lina the drive force, the motives behind and the intended consequences, yaani naandika ili nipate nini au hilo bandiko lilete matokeo gani chanya.

Sasa from now on nitakuwa na share na nyinyi the motive behind ya baadhi ya mabandiko yangu na the intended consequences ya mabandiko hayo na kuitumia hiyo consequences au matokeo hayo as the drive force behind me kuendelea kuandika kwa kuthibitisha sifanyi kazi bure na kazi iendelee!.

Hapa kwenye bandiko kuu nitaweka line up only halafu uchambuzi utafuata kwenye individual posts.

  1. Madudu ya Ajabu ya Ubatili wa Katiba Yetu, Mabadiliko Fake ya Sheria na Tume ya Uchaguzi, Rais Samia Asilaumiwe Kwasababu Yeye Sio Mwanasheria!.
  2. Tujifunze kuwa na Shukrani kwa Madogo ili Tupatiwe Makubwa!. Japo Tulitaka Kikubwa, Tumepewa Kiduchu!, Tukipokee Tushukuru, au Tususe Kudai Kikubwa?.
  3. Lile fupa lililowashinda marais wanaume 4, rais mwanamke 1 aligegeda kama mlenda!. Miswada 3 ya ukombozi mpya wa taifa letu yatua bungeni asubuhi hii
  4. Ushauri kwa Rais Samia: Kwenye mabadiliko ya Cabinet kufuatia Ripoti ya CAG, tumia wazoefu; Fedha mpe Dkt. Kimei, Biashara Uwekezaji mpe Deo Mwanyika
  5. Kinyang'anyiro cha Urais 2025 kwa tiketi ya CCM: Dkt Mwinyi kuwania Urais wa Muungano?
  6. Mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi: Je Tupige Ndege Wawili kwa Jiwe Moja kwa Uchaguzi Serikali za Mitaa/Mkuu, Ufanyike Siku Moja au Tuendeleze Mazoea?.
  7. Kupigwa billioni 75 ni ujinga au upumbavu? Tutaendelea kukubali kufanywa kichwa cha mwendawazimu hadi lini?
  8. Hongera Rais Samia kwa Ph.D Nyingine ya Heshima, Akemee Kuitwa Dr? Kuna Haja TCU/MCT/Maelezo Kutoa Ufafanuzi/Muongozo kwa Media Kuita Watu Dr?
  9. Kuongezeka Ph.D za Heshima: Kuna haja TCU watoe ufafanuzi wa matumizi ya title ya Dr. kwa Ph.D za heshima na Ph.D za ukweli?
  10. LIVE - Mjadala kupinga adhabu ya kifo nchini. TLS yajali utu, yaonesha njia. Adhabu hii ifutwe
Inaendelea ...

Paskali
Yaani Pascal Mayalla uko vizuri sana, ila punguza kujipendekeza, wewe ni mtu wa juu sana hutakiwi kuwa CHAWA.
Huo uchawa waachie low minded class kama Lucas mwashambwa na johnthebaptist
 
Bandiko hili Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli ni la mwaka 2014, mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wa 2015.
Hili ni bandiko la kuuanda umma kisaikolojia iwapo JPM angeteuliwa na CCM kuwa mgombea wake kwa kueleza what to expect, and everything happened as stated.
1. Ni kweli JPM akaja kuwa mgombea wa CCM
2. Niliahidi kuzitaja sababu za kwanini ni JPM, lakini sikuzitaja.
3. Nilisema atakuja kuwa dikiteta, ni kweli akawa
4. Nikamention the consequences, and the consequences happened!.
P
 
Wanabodi

Mimi ni mwana JF mwenzenu humu JF na ni verified tangu 2008, katika miaka hii zaidi ya 15, nimepandisha mabandiko mengi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Hili ni bandiko la kufanya assessment, jee hoja zangu zina mashiko?, zimesaidia kitu au ninaandika for nothing kupoteza tuu muda?.

Wakati ukitafakari na mimi pia najifanyia self assessment, kuna baadhi ya mada zangu huwa zinaandamana na ushauri wa a way forward na baadhi zina onyesha the consequences za kitakachotokea.

Kwa vile mwandishi ni mimi, karibu kila bandiko langu lina the drive force, the motives behind and the intended consequences, yaani naandika ili nipate nini au hilo bandiko lilete matokeo gani chanya.

Sasa from now on nitakuwa na share na nyinyi the motive behind ya baadhi ya mabandiko yangu na the intended consequences ya mabandiko hayo na kuitumia hiyo consequences au matokeo hayo as the drive force behind me kuendelea kuandika kwa kuthibitisha sifanyi kazi bure na kazi iendelee!.

Hapa kwenye bandiko kuu nitaweka line up ya mabandiko yenye big impact only halafu uchambuzi utafuata kwenye individual posts.
- Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Na hii ni lineup ya mabandiko yote

Inaendelea
Paskali
Kama nchi Bado ni maskini na ujinga miongoni mwa watu umeongezeka kuliko ilivyokuwa kabla Yako unadhani hoja zimesaidia???
 
Back
Top Bottom