#COVID19 Hoja ya Polepole na hoja ya Gwajima juu ya chanjo ya Covid-19

Mbona kuna mtu alikuwa kachomwa chanjo tena alichomwa mapema kabisa baada ya rais kutangaza chanjo,

Ana umri wa 58, wiki iliyopita alijisikia homa akawa anapumua kwa shida, akalazwa akawekewa oksjen, baadae akafariki!
Na alikuwa kachomwa chanjo!

Hii imetokea kwa mmoja ninayemjua kabisa alichomwa, je wangapi huko wanakufa na corona wakati chanjo walichoma
Wataalamu wanasema kama kirusi kimekupata halafu ukaenda kuchanja haitakusaidia. Unashauriwa upime kwanza na ndipo uchanje, ili kwamba kama umeambukizwa itabidi utibiwe hadi upone halafu ndipo uchanjwe.

Na J&J inazalisha kinga kwa 70%. Inamaana uwezekano wa kukinga sio 100%. So possibility ya kuambukizwa na pengine kupoteza maisha bado ipo kwasababu vaccine siyo kinga ya kifo.

Nadhani nimekujibu kitu.
 
Umeona eenhh???!!!.Mimi sichanji km ni kufa nitakufa kifo kilichoamriwa na Mwenyezi MUNGU.
Hauko peke yako, mpo wengi. Hata chanjo za zamani pia ni wengi tu hawakuchanja. Ila corona ukimpeleka nyumbani kwako si rahisi kumalizana na wewe peke yako. Atakamata na wengine pia.
 
Hoja ya Polepole kuwa virusi vinaweza kuwa vimetengenezwa ina mashiko, virusi vinaweza kutengenezwa na kutumika kama bio-weapons, virusi hivi vinaua kama vile vya asili tu. Lakini kusema unapinga chanjo kwasababu kirusi ni cha kutengenezwa na siyo cha asili ni hoja dhaifu. Kirusi cha kutengeneza na kile cha asili vyote njia ya kupambana navyo ni chanjo. Kukataa chanjo kwa sababu hiyo ni kama kusema, "kama mmeamua kuniua niueni." Kuwa kirusi cha kutengeneza siyo sababu ya kukataa chanjo. Tumuulize, ni kweli kirusi ni cha kutengeneza, na kinaua, tupambane nacho vipi?

Kusema vinabadilika badilika kila mara, hilo linatokea kama kirusi kina hosts wengi sana. Hapa kama kirusi kimeambukiza watu wengi sana lazima kina kuwa na nafasi ya kubadilikabadilika kubwa. Ukipunguza idadi ya watu wanaoambukizwa hata kasi ya kirusi kumutate itapungua. Kama Africa ambayo haichukui tahadhari ya kutosha, itakuwa uwanja wa kirusi kumutate. Hata virusi vya mafua ya kawaida hubadilika badilika na WHO ipo macho sikuzote kufuatilia mutation yake.

Tukizungumzia mafua ya kawaida, mafua ni ugonjwa wa ndege, sasa kirusi kile kikibadilika kinaweza kuambukiza nguruwe na kuleta mafua ya nguruwe, au kikabadilika na kuleta mafua kwa binadamu, na kile kilicholeta mafua ya nguruwe kinaweza ruka tena na kuleta mafua kwa binadamu. Watu wa Afya wako chonjo kwenye machinjio za ndege juu ya kuzuka virusi hivyo. Na vinaibuka mara kwa mara. So jambo la kirusi kubadilika mara kwa mara lipo kwa virusi vingi, vikipata mazingira mazuri vinafanya hivyo kwa kasi kubwa.

Kuhusu chanjo inakulinda kwa muda gani hilo linategemea mambo mengi. Chanjo Inatarget aina ya kirusi kilichopo. Kama kirusi kikibadilika kabisa kiasi cha kufanya kinga iliyozalishwa na chanjo isiweze kukitambua, itakuwa haina kazi tena. Muda wa chanjo kufanya kazi unategemea sana mutation rate ya kirusi. Kama kipo stable, chanjo inaweza kukitokomeza kabisa, kama polio.

Polepole ni muumini wa mwisho wa dunia, 666, new world order na conspiracy kama hizo, hivyo anajaribu kutafsiri jambo hili kwa mtazamo huo. Si sawa.
Hata kama chanjo ni ya majaribio?
 
Wataalamu wanasema kama kirusi kimekupata halafu ukaenda kuchanja haitakusaidia. Unashauriwa upime kwanza na ndipo uchanje, ili kwamba kama umeambukizwa itabidi utibiwe hadi upone halafu ndipo uchanjwe.

Na J&J inazalisha kinga kwa 70%. Inamaana uwezekano wa kukinga sio 100%. So possibility ya kuambukizwa na pengine kupoteza maisha bado ipo kwasababu vaccine siyo kinga ya kifo.

Nadhani nimekujibu kitu.
Yani kwamba hata mtu ambaye hana dalili zozote za corona akitaka kuchanja anashauriwa akapime kwanza na akionekana hana corona ndio aje kuchanjwa?
 
Hauko peke yako, mpo wengi. Hata chanjo za zamani pia ni wengi tu hawakuchanja. Ila corona ukimpeleka nyumbani kwako si rahisi kumalizana na wewe peke yako. Atakamata na wengine pia.
Kwa hiyo nikichanja siwezi kuambukizwa corona?,je siwezi kuambukiza wengine?,Je nikichanjwa sitalazimika kuvaa barakoa?,Je, nikichanjwa sitalazimika kujizuia na mikusanyiko?,Je, nikichanjwa sitalazimika kuchanja tena chanjo ya COVID-19?.Ukinijibu hoja hizi vizuri, naenda kuchanja hata Sasa hivi.
 
Hata kama chanjo ni ya majaribio?
Ngoja tuanze na hii chanjo ya J&J. Hii chanjo inatumia teknolojia ya zamani. Teknolojia ambayo usalama wake na makandokando yake unajulikana vema. Hivyo chanjo kama hii haihitaji utafiti au majaribio ya muda mrefu kujua madhara na ufanisi wake.

Chanjo hii ni aina ya Viral vector. Hapa kirusi aliyepunguzwa nguvu au aliyeuwawa huchomwa ndani ya mtu. Mwili unagundua uvamizi na kutengeneza kinga. Siku nyingine kirusi chenyewe kikija, kinga inakuwepo tayari. Teknolojia hii inajulikana vema. Wanasema, "hakuna haja ya kugundua gurudumu kwa mara ya pili." Teknolojia imekuwa, vitu vingi vinajulikana. Mambo yanaweza kwenda fasta. Hivyo siyo majaribio, watu wanauhakika wa asilimia nyingi ya kile kinachofanyika.
 
Inatakiwa kujenga hoja kwa kuchambua taarifa na maarifa yaliyopo. Si kwa kukisia-kisia.

Na hata hivyo nimesema kuwa hata kama kirusi ni cha kutengeneza, njia ya kukidhibiti ni chanjo na kujilinda. Huwezi pinga chanjo kwasababu kirusi ni cha kutengeneza. Ni sawa mtu aweke virusi kwenye kompyuta yako halafu useme, "hizi ni njama, sitengenezi."
Njia nzuri ni kujenga uwezo wa wataalam katika kufanya utafiti ili kupunguza utegemezi
 
[
Kwa hiyo nikichanja siwezi kuambukizwa corona?,je siwezi kuambukiza wengine?,Je nikichanjwa sitalazimika kuvaa barakoa?,Je, nikichanjwa sitalazimika kujizuia na mikusanyiko?,Je, nikichanjwa sitalazimika kuchanja tena chanjo ya COVID-19?.Ukinijibu hoja hizi vizuri, naenda kuchanja hata Sasa hivi.
Hata Gwajima ana hoja hiyo. Nenda post number nne usome paragraph ya mwisho.
 
Ngoja tuanze na hii chanjo ya J&J. Hii chanjo inatumia teknolojia ya zamani. Teknolojia ambayo usalama wake na makandokando yake unajulikana vema. Hivyo chanjo kama hii haihitaji utafiti au majaribio ya muda mrefu kujua madhara na ufanisi wake.

Chanjo hii ni aina ya Viral vector. Hapa kirusi aliyepunguzwa nguvu au aliyeuwawa huchomwa ndani ya mtu. Mwili unagundua uvamizi na kutengeneza kinga. Siku nyingine kirusi chenyewe kikija, kinga inakuwepo tayari. Teknolojia hii inajulikana vema. Wanasema, "hakuna haja ya kugundua gurudumu kwa mara ya pili." Teknolojia imekuwa, vitu vingi vinajulikana. Mambo yanaweza kwenda fasta. Hivyo siyo majaribio, watu wanauhakika wa asilimia nyingi ya kile kinachofanyika.
Wewe nenda kachanje
 
Utajiandaa kuchanja mara ngapi maana kama wanatengeneza wataendelea kutengeneza zaidi na zaidi
Kama kirusi kitaendelea kubadilika badilika itatubidi kuchanja mara nyingi tuwezavyo. Chanjo ya Typhoid huchanjwa kila baada ya miaka 5 kamq sijakosea.

Lakini watu wengi wakichanjwa, tunapunguza mazalia ya virusi kubadilikabadilika, na inawezekana kukitokomeza kamq polio au ndui.
 
Yap, kama hivyo. Kuwa delta, Mu nk.
Sasa mbona chanjo pia hazizuii kupata maambukizi na kuambukiza? sasa hapo tutazuia vp hiyo hali ya virusi kubadilika badilika? na kuhusu afrika je kwanini mpaka sasa haijawa kuwa ndio uwanja wa virusi Kumutate kwa sababu tuko nyuma kwenye kuzuia maambukizi na hata kasi ya kuchanja chanjo?
 
Back
Top Bottom