#COVID19 Hoja ya Polepole na hoja ya Gwajima juu ya chanjo ya Covid-19

Kuhusu chanjo, Gwajboy anauoigwa mwingi,
Na serikali ya ccm isibinye Uhuru wa kujieleza kuhusiana na Jambo hili!
 
Hoja ya Polepole kuwa virusi vinaweza kuwa vimetengenezwa ina mashiko, virusi vinaweza kutengenezwa na kutumika kama bio-weapons, virusi hivi vinaua kama vile vya asili tu. Lakini kusema unapinga chanjo kwasababu kirusi ni cha kutengenezwa na siyo cha asili ni hoja dhaifu. Kirusi cha kutengeneza na kile cha asili vyote njia ya kupambana navyo ni chanjo. Kukataa chanjo kwa sababu hiyo ni kama kusema, "kama mmeamua kuniua niueni." Kuwa kirusi cha kutengeneza siyo sababu ya kukataa chanjo. Tumuulize, ni kweli kirusi ni cha kutengeneza, na kinaua, tupambane nacho vipi?

Kusema vinabadilika badilika kila mara, hilo linatokea kama kirusi kina hosts wengi sana. Hapa kama kirusi kimeambukiza watu wengi sana lazima kina kuwa na nafasi ya kubadilikabadilika kubwa. Ukipunguza idadi ya watu wanaoambukizwa hata kasi ya kirusi kumutate itapungua. Kama Africa ambayo haichukui tahadhari ya kutosha, itakuwa uwanja wa kirusi kumutate. Hata virusi vya mafua ya kawaida hubadilika badilika na WHO ipo macho sikuzote kufuatilia mutation yake.

Tukizungumzia mafua ya kawaida, mafua ni ugonjwa wa ndege, sasa kirusi kile kikibadilika kinaweza kuambukiza nguruwe na kuleta mafua ya nguruwe, au kikabadilika na kuleta mafua kwa binadamu, na kile kilicholeta mafua ya nguruwe kinaweza ruka tena na kuleta mafua kwa binadamu. Watu wa Afya wako chonjo kwenye machinjio za ndege juu ya kuzuka virusi hivyo. Na vinaibuka mara kwa mara. So jambo la kirusi kubadilika mara kwa mara lipo kwa virusi vingi, vikipata mazingira mazuri vinafanya hivyo kwa kasi kubwa.

Kuhusu chanjo inakulinda kwa muda gani hilo linategemea mambo mengi. Chanjo Inatarget aina ya kirusi kilichopo. Kama kirusi kikibadilika kabisa kiasi cha kufanya kinga iliyozalishwa na chanjo isiweze kukitambua, itakuwa haina kazi tena. Muda wa chanjo kufanya kazi unategemea sana mutation rate ya kirusi. Kama kipo stable, chanjo inaweza kukitokomeza kabisa, kama polio.

Polepole ni muumini wa mwisho wa dunia, 666, new world order na conspiracy kama hizo, hivyo anajaribu kutafsiri jambo hili kwa mtazamo huo. Si sawa.
Na ndio walikua washauri wakuu wa mwendazake. Misimamo yao inafanana
 
Badala ya kujibu hoja zao, hata kama mnaziita dhaifu…. mmechagua kuwafunga midomo.!
Binafsi sioni haja ya ku support malumbano yao tangia swala la chanjo ni hiari ya mtu sasa kwann mjifanye hodari wa kubishana ? Asietaka na anaetaka .
 
Unaweza pata ugonjwa na ukaonyesha dalili au usionyeshe. Ila mara nyingi tunachukulia asiye na dalili hana ugonjwa. Ndiyo maana asiye na dalili si lazima kupima kwanza.
Na unaweza ukapima ikaonekana huna ugonjwa kumbe upo.
 
Mbona kuna mtu alikuwa kachomwa chanjo tena alichomwa mapema kabisa baada ya rais kutangaza chanjo,

Ana umri wa 58, wiki iliyopita alijisikia homa akawa anapumua kwa shida, akalazwa akawekewa oksjen, baadae akafariki!
Na alikuwa kachomwa chanjo!

Hii imetokea kwa mmoja ninayemjua kabisa alichomwa, je wangapi huko wanakufa na corona wakati chanjo walichoma

Swala la kuwekewa Oxygen kuna ndugu yangu kule Njombe aliumwa akashindwa kupumua, baadae akawekewa Oxygen kwa siku kadhaa. Akapona, kurudi mtaani akaanza kuumwa tena kushindwa kupumua. Baada ya muda akafariki(R.I.P), na hiyo ilikua ni mwaka 2017 kabla ya Corona hii.
Kwa hiyo watu kuewekewa mitungi ya Oxygen au kuumwa magonjwa kama hayo yalikuwepo kabla ya ujio wa UVIKO-19.
 
Inaweza kuwa ni sababu ya kirusi kubadilika. Unaweza kuta virusi wanaoweza kudhibitiwa na chanjo kwenye mzunguko wapo 80% lakini 20% ni strain mpya. Na kadri watu wengi wasivyochanjwa ndiyo kasi ya kirusi kumutate inavyokuwa kubwa. Hata magonjwa ambayo tunachanjwa utotoni ingetokea kuna watu wamegoma kuchanja, zingeibuka strains ambazo zingeweza kuambukiza na kuua hata wale waliochanjwa.

Hata hii inayoitwa kuchanja ni hiari ni bomu tunatengeneza. Kirus kitakua hakiishi na kila wakati itakuja new Strain/ variant na kuleta kizaazaa. Kwa kweli Mungu atunusuri kisi mutate na kuleta strain mpya ambazo zitasababisha madhara makubwa.
Kimsingi kuchanjwa kungefanywa ni Mandatory.
 
Chanjo inafanya kazi mtu akiwa hana maambukizi, chanjo ni kinga, siyo tiba. kama amepata tayari ugonjwa haisaidii.

Ndiyo lengo hasa la kusema wenye dalili za korona wasichanjwe. Na kama resources zipo unaweza kuwapima wote kujiridhisha kama wanq korona, lakini ka mtu haonyeshi dalili, halazimiki kupima.

Kama mtu alichanjwa wakati ana vimelea vya virus, maana hakuna sharti la kupima kabla ya chanjo, je kama baadae kwa board immune system virus watakufa, je chanjo itakuwepo au itakua imekufa, na kwa nn?
 
Ni vp maambukizi yanapungua kwa hizo nchi kuwa hizo nchi zilizochanja watu wengi?

Ingia WHO statistcs, huko Ulaya ni kama hawana habari tena na Covid-19, wamejitahidi kuidhibiti na kwa sasa viwanja hujaa sana kwa sababu Corona siyo tishio kubwa tena
 
Swala la kuwekewa Oxygen kuna ndugu yangu kule Njombe aliumwa akashindwa kupumua, baadae akawekewa Oxygen kwa siku kadhaa. Akapona, kurudi mtaani akaanza kuumwa tena kushindwa kupumua. Baada ya muda akafariki(R.I.P), na hiyo ilikua ni mwaka 2017 kabla ya Corona hii.
Kwa hiyo watu kuewekewa mitungi ya Oxygen au kuumwa magonjwa kama hayo yalikuwepo kabla ya ujio wa UVIKO-19.
Acha ujinga, huyu hakuwa mgonjwa, alichomwa kama chanjo, akaendelea na kazi kama wiki tatu zilizopita!
Juzi wiki ilopita ghafla ndo alianza kuonyesha dalili za corona, akapelekwa Hosp. Akabanwa mbavu, akazidiwa, akawekewa oksjen baadae akafariki!

Na alizikwa kwa tahadhari zote za covid hivyo haijulikan chanjo ilifeli wapi
 
Ingia WHO statistcs, huko Ulaya ni kama hawana habari tena na Covid-19, wamejitahidi kuidhibiti na kwa sasa viwanja hujaa sana kwa sababu Corona siyo tishio kubwa tena
Sawa mkuu ila nilichokiuliza umekielewa?
 
Kupima variants, tuna uwezo au tunafanya hivyo? Hiyo ndiyo inakuonyesha level ya mutation. Maana hata kupima tu nchi nyingi ni shida.

Pia elewa kuwa mtu mwenye chanjo si rahisi kumuambukiza mwingine sababu virusi havizaliani ndani yake. Na kwa sababu virusi havizaliani si rahisi kumutate. Na si rahisi kuambukizwa kwasababu kirusi kikiingia kinakutana na kinga ya mwili.

Kuzuia kirusi kumutate unatakiwa kuzuia kizizaliane. Hivyo basi, chanjo na kujikinga ndizo njia.
Mkuu haya unayoeleza umeyapata wapi kama huko kusema kwamba aliyechanjwa si rahisi kupata maambukizi na kuambukiza?
 
Ingia WHO statistcs, huko Ulaya ni kama hawana habari tena na Covid-19, wamejitahidi kuidhibiti na kwa sasa viwanja hujaa sana kwa sababu Corona siyo tishio kubwa tena
Ushahidi wa nguvu ya chanjo upo wazi kabisa.
 
Ndungu leta hoja yako nasio kusema haina mashiko for what?
Nikuulize wewe unaelewa nini huu ya chanjo?
Then Red Giant ....
Nikukumvushe chanjo sio Tiba wala suluhisho ya kufukuza covid na kwamba hutaambukizwa.
Unaeza chanja zaidi ya awam moja for how?
Unaposema suruhisho ni kuchanja leta hoja yenye ushawishi
So what's solution ....

Yaaani kirusi kinabadilika kwahiyo unataka kusema kirusi hicho kinakuwa kama kinyonga come back

Hoja ya Polepole kuwa virusi vinaweza kuwa vimetengenezwa ina mashiko, virusi vinaweza kutengenezwa na kutumika kama bio-weapons, virusi hivi vinaua kama vile vya asili tu. Lakini kusema unapinga chanjo kwasababu kirusi ni cha kutengenezwa na siyo cha asili ni hoja dhaifu. Kirusi cha kutengeneza na kile cha asili vyote njia ya kupambana navyo ni chanjo. Kukataa chanjo kwa sababu hiyo ni kama kusema, "kama mmeamua kuniua niueni." Kuwa kirusi cha kutengeneza siyo sababu ya kukataa chanjo. Tumuulize, ni kweli kirusi ni cha kutengeneza, na kinaua, tupambane nacho vipi?

Kusema vinabadilika badilika kila mara, hilo linatokea kama kirusi kina hosts wengi sana. Hapa kama kirusi kimeambukiza watu wengi sana lazima kina kuwa na nafasi ya kubadilikabadilika kubwa. Ukipunguza idadi ya watu wanaoambukizwa hata kasi ya kirusi kumutate itapungua. Kama Africa ambayo haichukui tahadhari ya kutosha, itakuwa uwanja wa kirusi kumutate. Hata virusi vya mafua ya kawaida hubadilika badilika na WHO ipo macho sikuzote kufuatilia mutation yake.

Tukizungumzia mafua ya kawaida, mafua ni ugonjwa wa ndege, sasa kirusi kile kikibadilika kinaweza kuambukiza nguruwe na kuleta mafua ya nguruwe, au kikabadilika na kuleta mafua kwa binadamu, na kile kilicholeta mafua ya nguruwe kinaweza ruka tena na kuleta mafua kwa binadamu. Watu wa Afya wako chonjo kwenye machinjio za ndege juu ya kuzuka virusi hivyo. Na vinaibuka mara kwa mara. So jambo la kirusi kubadilika mara kwa mara lipo kwa virusi vingi, vikipata mazingira mazuri vinafanya hivyo kwa kasi kubwa.

Kuhusu chanjo inakulinda kwa muda gani hilo linategemea mambo mengi. Chanjo Inatarget aina ya kirusi kilichopo. Kama kirusi kikibadilika kabisa kiasi cha kufanya kinga iliyozalishwa na chanjo isiweze kukitambua, itakuwa haina kazi tena. Muda wa chanjo kufanya kazi unategemea sana mutation rate ya kirusi. Kama kipo stable, chanjo inaweza kukitokomeza kabisa, kama polio.

Polepole ni muumini wa mwisho wa dunia, 666, new world order na conspiracy kama hizo, hivyo anajaribu kutafsiri jambo hili kwa mtazamo huo. Si sawa.
 
Polepole: Moja, Polepole yeye anasema kuwa corona ni ugonjwa uliotengenezwa na big pharma ili yapige pesa. Kuwa mabeberu wanaachana na kuvamia nchi kuiba mafuta na sasa wanatengeneza magonjwa ili kupiga pesa.

Pili, Anasema kuwa kasi ya kirusi kubadilika(ku-mutate) inatia shaka, si ya kawaida.

Tatu, anauliza chanjo hiyo itamkinga kwa muda gani? Akatolea mfano kuwa chanjo zingine hudumu maisha yote ya mtu, je hii inadumu muda gani? Hapo anamaanisha kuwa atahitajika kuinunua mara ngapi?

Gwajima yeye anasema kuwa chanjo zile zina serial number, kuwa ukichanja zinakusajili. Kwamba ipo kama barcode, itafika wakikuwekea detector itasoma iwapo umechanja au haujachanja. Kuna mahali amewahi husisha chanjo hii na habari za 666 na ujio wa mfumo mpya, ndiyo maana anasema kuwa watu waananunua dhahabu kwa wingi ili kujiandaa na mfumo mpya, mfumo ambao pengine pesa za makaratasi zisiwe na thamani.

Pia anahoji kuwa kama ukichanja bado utatakiwa kuvaa barako, kutumia sanitizer, utaugua na utaambukiza wengine, ya nini kuchanja?

Amewahi kusema kuwa chanjo ya mRNA inabadilisha watu na kuwafanya mazombie, hivyo akashauri kuwa wanajeshi wasichanjwe.

Kifupi hizi ndizo hoja za hawa wabunge wawili walio mbele kupinga uchanjaji.

Mi kwa maoni yangu ni kuwa hawa jamaa hawana hoja za msingi bali ni Conspiracy theorist tu.
Nakubaliana na wewe ila pia tykumbuke..Gwiji boy alipata ubunge kifavour..hali kadhalika Polex2. Hawakuwahi kuwa maarufu ktk siasa kwa nguvu zao...hivyo mi naona hapa tunatafuta kick kwa kupandia mahali ambapo watu wengi walijengewa hofu tangu enzi za Jiwe...sasa wanajaribu kuwadaka wawe waumini wa siasa zao. Haya ni maoni yangu tu!
 
Mbona kuna mtu alikuwa kachomwa chanjo tena alichomwa mapema kabisa baada ya rais kutangaza chanjo,

Ana umri wa 58, wiki iliyopita alijisikia homa akawa anapumua kwa shida, akalazwa akawekewa oksjen, baadae akafariki!
Na alikuwa kachomwa chanjo!

Hii imetokea kwa mmoja ninayemjua kabisa alichomwa, je wangapi huko wanakufa na corona wakati chanjo walichoma
Hii haiondoi usalama wa chanjo,
 
Polepole: Moja, Polepole yeye anasema kuwa corona ni ugonjwa uliotengenezwa na big pharma ili yapige pesa. Kuwa mabeberu wanaachana na kuvamia nchi kuiba mafuta na sasa wanatengeneza magonjwa ili kupiga pesa.

Pili, Anasema kuwa kasi ya kirusi kubadilika(ku-mutate) inatia shaka, si ya kawaida.

Tatu, anauliza chanjo hiyo itamkinga kwa muda gani? Akatolea mfano kuwa chanjo zingine hudumu maisha yote ya mtu, je hii inadumu muda gani? Hapo anamaanisha kuwa atahitajika kuinunua mara ngapi?

Gwajima yeye anasema kuwa chanjo zile zina serial number, kuwa ukichanja zinakusajili. Kwamba ipo kama barcode, itafika wakikuwekea detector itasoma iwapo umechanja au haujachanja. Kuna mahali amewahi husisha chanjo hii na habari za 666 na ujio wa mfumo mpya, ndiyo maana anasema kuwa watu waananunua dhahabu kwa wingi ili kujiandaa na mfumo mpya, mfumo ambao pengine pesa za makaratasi zisiwe na thamani.

Pia anahoji kuwa kama ukichanja bado utatakiwa kuvaa barako, kutumia sanitizer, utaugua na utaambukiza wengine, ya nini kuchanja?

Amewahi kusema kuwa chanjo ya mRNA inabadilisha watu na kuwafanya mazombie, hivyo akashauri kuwa wanajeshi wasichanjwe.

Kifupi hizi ndizo hoja za hawa wabunge wawili walio mbele kupinga uchanjaji.

Mi kwa maoni yangu ni kuwa hawa jamaa hawana hoja za msingi bali ni Conspiracy theorist tu.
Chanjo kuwa ya muda na sio ya kudumu sio jambo jipya . Kila mwaka wazungu wanachanjwa flu shot mpya kwani virusi wa flu wanabadilika kila Mara kiasi chanjo ya zamani haifanyi kazi. Ni aibu kwa viongozi kama hawa waliopewa dhamana kushindwa kuongoza watu kwenye maamuzi sahihi kwa maisha yao.
 
Back
Top Bottom