( Hii nimeinasa kule Michuzi blog, imepambisha mjadala. Kuna mwenye sehemu ya kwanza atumwagie humu ukumbini!)
HOJA YA HAJA
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
HOJA YA HAJA
Mwibaji na watwana, mlifi ni mwungwana
(sehemu ya pili na ya mwisho)
Ilipopita awamu ya pili ikajiri awamu ya tatu (Awamu kati). Hii kwa hakika ilikuwa awamu ambayo iliingia katikati na kuyaangalia mapungufu na mafanikio ya awamu ya kwanza na awamu ya pili.
Awamu hii ikarudia pale pale kwenye awamu ya kwanza kuhusu swala la demokrasia, na kwamba viongozi wake wakawa wakali kwamba wanataka kurudisha tabia ile ile ya kuogopa watu wasisemeseme hovyo. Hakika viongozi wa awamu ta tatu walikuwa wakali sana na wakatengeza uga ambao ilikuwa si rahisi tu kupenyeza rupia hata penye udhia.
Awamu hii ilisheheni sifa za kujenga uchumi na kwamba pato la taifa likawa limedhibitiwa na ule uholela baada ya RUKSA haukuwepo tena, na zaidi ubinafsi sasa ukarudi na kujilimbikiza kwa hao viongozi wa awamu ya tatu. Kauli mbio hapa ilikuwa na Uongozi Bora. Hakika ulikuwa uongozi bora maana matokeo yake yalikuwa kwamba baadhi ya viongozi walikuwa bora haswaa katika kujizatiti ki-uchumi na kimaendeleo binafsi na siyo kwa kila mwananchi!.
Mengi yamesemwa na bado yataendelea kusemwa kuhusu maazimio yenye madhumini endelezi ya awamu zote tatu na hapatakosa kujiri kasoro zake ambazo baadhi nimezigusia hapo juu.
Haya sasa tupo kwenye awamu ya nne ambayo ilipokelewa kwa vishindo, shangwe na nderemo nah ii kweli iliingia kwa staili yake tofauti kabisa na awamu zote japo ikizingatia kabisa misingi muhimu iliyowekwa na awamu zote ambazo zilizopita. Hapa tukapata utawala wa kwanza kabisa wa uongozi wote wa juu kuwa na safu kubwa ya vijana ambayo wengi waliitafsiri kwa lugha ya kigeni boys to men. Hakika pailikuwa na faraja kubwa na hasa kwa vijana ambao ndiyo tumaini kubwa la maendeleo yeyote katika nchi yeyote.
Hapa pakatokea demokrasia ya uga mpana kabisa kwamba unaweza kusme chochote na hata jambo ambalo si zuri kulisema kwa kumtaja kiongozi yeyote yule wa kitaifa na bado hutafanywa lolote kama vile kupelekwa kuzuizini ama kuitwa muhaini.
Sasa ni hili ndilo limezaa yote haya ya watu kutumia vinywa vyao kusema yanayowakera binafsi na kuyafanya ya kitaifa, kujenga tabaka za makundi ya wafuasi wa kisiasa na mpaka kufikia kuleta makundi ambayo sasa ndiyo yamekuwa maarufu ndani ya serikali na vyama vyao vya kisiasa na hata mpaka kwenye dini!!!! Hakika chombo kinawenda mrama hapa!!!
Nani alisema kwamba unapokuwa na uhuru wa kusema basi unasimama kwenye majukwaa na kuanza kukashifu na kubeza viongozi wa kitafia eti tu kwa sababu nawe ulikuwa kiongozi wa nyadhifa fulani katika awamu zilizopita?
Mbona wapo ambao walikuwa na hata nyadhifa kubwa tu wamekaa kimya na ndiyo sasa wanatumika kama wapatanishi wa malumbano haya!!! Kwa nini hizi taasisi ambazo zina majina makubwa zisijitenge ili kujitofautisha na taasisi shutumu badala ya kuleta maneno ama makongamano ya kushutumu, kukashifu na kudhalilisha viongozi ziungane na waungwana ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuleta suluhu ya matatizo yanayojiri nchi yetu kisiasa na kiuchumi??
Bado ninadirki kusema serikali ya awamu ya nne ni shujaa maana imefungua milango yote ya uhuru na mpaka baadhi ya watu wanadirki sasa kufanya mashambulio ambayo dhahiri yanaonyesha kulenga mtu binafsi??? Kweli tumefikia hapo bila ya kujijua ama kwa makusudi?????(sehemu ya pili na ya mwisho)