Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,162
Pengine mtu mbaye anabeba vichwa vya habari kwa sasa kuliko mtu mwingine yoyote hapa nchini kwa sasa ni Paul Makonda aka Bashite.
Watu wanajiuliza maswali mengi, iweje mtu huyu huyu, kwenye utawala wa awamu ya 5, chini ya Mwendazake, alionekana kuwa ni mhalifu mkubwa, leo hii kwenye utawala wa awamu ya 6 aonekane kama shujaa na mtetezi wa wanyonge?
Kabla sijalijibu swali hilo, hebu tuangalie harakati anazofanya Katibu huyu wa uenezi wa CCM, katika kipindi hiki.
Anaitisha mikutano ya hadhara kwenye maeneo mbalimbali nchini na kusikiliza kero za wananchi na kujaribu kuzitatua papo kwa papo
Amekuwa ni mwiba kwa viongozi wa serikali hii ya CCM, ambao wameonekana wazi kuwa hawatatui matatizo ya wananchi kwa wakati na badala yake hao viongozi kila uchao, wamebaki kumsifia kinafiki Rais Samia Suluhu Hassan!
Hebu tujaribu kuangalia matatizo sugu ambayo watanzania hivi sasa wanakabiliana nayo:-
1. Tatizo la kukatika katika kwa umeme, kusiko na ratiba maalum, licha ya viongozi waliopo madarakani kutuhakikishia sisi wananchi kuwa tatizo hilo linatokana na mabwawa yetu yanayozalisha umeme kukauka.
Mungu naye amewaheleleza viongozi wa serikali hii ya CCM, kwa kuleta mvua ya El nino hadi mabwawa hayo yanayozalisha huo umeme wetu kufurika maji, lakini tunaendelea kushuhudia mgao wa umeme mkali kuliko wakati wowote, tokea nchi yetu ipate uhuru wake!
2. Kuna tatizo la kupaa kwa bei ya sukari, ambayo hivi sasa kuna baadhi ya maeneo hapa nchini, bidhaa hiyo inapatikana kwa bei ya mara dufu ya bei elekezi ya shilingi elfu 3 kwa kilo moja
3. Upandaji mkubwa wa nauli za daladala na mabasi yaendayo mikoani, ambako kumeleta maisha magumu sana kwa wananchi wanyonge wa nchi hii, kwa kisingizio cha upandaji wa bei ya mafuta ya petroli duniani, wakati katika hali halisi, mafuta hayo yameendelea kushuka kwa mwezi wa 3 mfululizo!
Nimemsikia Makonda katika hotuba yake ya majuzi huko mkoani Iringa, akiwaambia wananchi wa huko kuwa viongozi wengi wa serikali hii, wanapenda kumsifia Rais Samia, wakati kivitendo hawamsaidii Rais huyo, kutokana na kutoshughulikia matatizo yao ya msingi wanayokabiliana nayo hao wananchi
Hayo ni baadhi tu ya matatizo sugu wanayokabiliana nayo wananchi, huku viongozi wao hawachukui hatua yoyote ya kuyatatua na badala yake, wamekuwa wakiendelea kumpa sifa zilizopitiliza kwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan, kuwa anaupiga mwingi katika awamu yake na wengine wakitia "chumvi" kuwa ni Rais ambaye amefanya makubwa, kuliko Rais yeyote katika awamu zilizopita!
Hivi kiongozi unapata wali ujasiri wa kumsifu Rais Samia, kuwa amefanya makubwa kuliko Rais yeyote wa awamu zilizopita, wakati katika hali halisi, yeye Samia ndiye amefeli pakubwa kuliko Rais yeyote wa awamu zilizopita??
Lakini jibu ni moja tu, hao viongozi wanakuwa wanafiki na kujipendekeza kwa Rais Samia, kutokana na ubovu wa Katiba yetu, ambayo imempa madaraka makubwa mno ya kimungu-mtu Rais wetu, ambapo kila kiongozi a serikali hii, inabidi ajipenddkeze kwake ili asimsahau katika teuzi za maelfu ya ajira za serikalini!
Sasa swali kubwa wanalojiuliza wananchi, je huyu ni ndiye Bashite ambaye tulimzoea wa wakati wa awamu ya 5, ambaye alikuwa anazivunja sheria za nchi waziwazi, kwa mfano kuvamia kituo cha televisheni cha Clouds na askari wenye hunduko na vitendo vingine vingi vya uvunjaji wa sheria au huyu Makonda wa uongozi wa awamu ya 6, amekuja kivingine kabisa?
Jibu ambalo mimi naweza kulitoa, baada ya kutafakari kwa kina kwa muda mrefu, ni kuwa huyu Makonda wa sasa ni kiumbe kipya, ambaye ametubu madhambi aliyoyafanya hapo siku za nyuma na hivi sasa amezaliwa upya kwa mara ya pili!
Hata kwenye mafundisho ya dini, yanasema mtu ambaye anatubu dhambi zake za awali na kuamua kuwa ni kiumbe kipya, basi hata Mungu atakuwa amemsamehe dhambi zake