HOJA:Ukiritimba uondolewe kuandaa Miss Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HOJA:Ukiritimba uondolewe kuandaa Miss Tanzania

Discussion in 'Entertainment' started by Phillemon Mikael, Feb 17, 2010.

 1. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #1
  Feb 17, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 9,285
  Likes Received: 2,988
  Trophy Points: 280
  Naomba kupendekeza kuwa fursa ...ya kuandaa Mashindano ya Miss Tanzania itolewe kiushindani...,kwa kuzingatia kuwa :-

  ...mrembo anayepatikana anaenda kutuwakilisha watanzania wote ni vema tuwe na uhakika na kampuni inayoandaa mashindano imepita kwenye vigezo vya ushindani......

  ..hakuna mtu mwenye hatimiliki ya jina Tanzania...kama mtu anataka kuandaa mashindano ya urembo miaka nenda rudi basi anaweza kuamua kuyaita kwa jina lolote lakini sio jina letu wote....halafu vigezo unavyotumia sio wazi!!!

  ..sishangai watanzania kuwa wasindikizaji kwenye michuano hiii ..kwani kuna mataifa mengi duniani hayashindi..na ni haki tuendelee kushiriki ...sio lazima tushinde leo wala kesho...TATIZO LANGU LIPO KWA AINA YA WAREMBO WANAOPATIKANA NA TABIA ZAO ZA KUTUAIBISHA.....hilo naona wazi linatokana na kukabidhi jukumu la kuandaa mashindano hayo kwa watu bila kutoa fursa ya watu wengine wenye uwezo...inawezzekana ..uwezo wa waandaaji umeishia hapo ....sasa umefika wakati na watu wengine wapewe fusra ya kuandaa...

  nashauri wizara ya michezo ,idara ya sanaa..na maonyesho iweke mchakato ...wa kutangaza zabuni ya kuandaa mashindano ya aina hii..hatukatai kuwa kutokana na investment inayotakiwa sio vibaya ..mtu atakayeshinda zabuni hiii ...akapewa fursa ya kuandaa miaka mitatu at least...lakini sio kuandaa indefinately....

  ni wazi kuwa waandaaji wa miss tanzania wamejeuka mafisadi wa pesa za wadhamini vodacom ...na mafisadi wa ngono..ndio maana wanashindwa kusimamia maadili ya waremmbo wao,,wanawajibika..kwani tunajuuwa kuwa wengi wa hawa wanoshinda wanakuwa vijana wadogo...ambao lazima waandaliwe baada ya kushinda kukabiliana na matokeo ya umaarufu wao..bahati mbaya sana pamoja na mapesa wanayopata wanashindwa hata kuajiri maafisa ushauri nasaha na uhusiano wa kuwaongoza warembo....ili kuweka hadhi ya taifa,wadhamini..na watanzania..

  ni wazi kuwa vodacom na wadhamini wengine they dont get value for money kwa kutumia bilioni moja kudhamini mashindano haya chini ya sheddy company ...inayoandaa mashindano haya!!
   
 2. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
 3. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,851
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Good idea ila njaaaaaaaaa ndo inasababisha haya kutokea kwa sababu tunasema tunajifunza kutokana na makosa SASA kila mwaka uozo huo huo waandaji,wizara zimelala tu...........
  Hopefully ten percent za wdhamini zinafanya kazi ndo maaana no action taken....lol!!
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,625
  Likes Received: 23,787
  Trophy Points: 280
  Hakuna haja, kuandaa u-miss Tanzania ni private entity, hiyo ndio biashara ya kampuni ya Lino Agencies, hivyo ni biashara halali na registered kama biashara/shughuli nyingine yoyote na ukiritimba haupo only kwenye names registration, ndio maana kuna miss utalii, miss bantu, miss tourism, miss earth, face of africa ets, hata ikiamuliwa ianzishwe miss JF, miss mabinti-wa, kihangaza, kihaya, watoto wa kitanga, nk.

  Kuna watu wanadhani miss Tanzania ni ya kiserikali na hao waandaaji wamepewa tuu kuandaa hivyo kuna ikiritimba. no way.

  Kitu kimoja nakubali, kushindanisha morphological beauty kwa madada zetu, huu sio utamaduni wa kiafrika, ndio maana wengine wakishaona hayo mapaja, wanashawishika hata kuonja hali inayopelekea baadhi ya madada zetu kuishia kumegwa na kuachwa na bado ushindi kukosa.

  Cha msingi ni waandaaji wa haya mashindano mbaimbali ya urembo pia kuwaandaa hawa mamiss kisaikolojia kuhusiana na dhamana wanazobeba wakiwa mamiss, wakifanya vitendo vya ajabu ajabu wakati bado wana crown vichwani mwao, wanavuliwa. Miss South Africa mmoja alivuliwa taji baada ya kuthibitika alitoa matamshi fulani ya kibaguzi dhidi ya mshiriki mwenzake wakati wa hatua za awali.

  Naamini hata Lundenga, anasubiria tuu matokeo ya kesi, kama mahakama itadhitisha hatia, miss anavuliwa taji mara moja!.
   
 5. RR

  RR JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,760
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 160
  Bro Hashim is out of ideas...we need a change!
  Kupewa leseni na Miss World isiwe ndo kigezo cha yeye kutupa mamiss incompetent kila mwaka....
   
 6. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #6
  Feb 17, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 9,285
  Likes Received: 2,988
  Trophy Points: 280
  ...kama ni biashara halali na registered basi aaandae MISS LINO ARGENCY...thats all hata akichagua bata ....sisi hatutauliza neno...lakini haiwezekani anatumia jina Miss Tanzania...mrembo huyo akienda anatakiwa awe kioo cha mabinti aliowaacha nyumbani..na hata kama hatashinda tujivunie utumishi wake.....lakini huu utaratibu usioeleweka ni lazima uwekewe mipaka ...

  kuna yule mwingine anayeandaa miss utalii kuna wakati alipewa pesa na miss tourism world aandae mashindano na akapata na wadhamini wengi...lakini mwisho wa siku dakika za mwisho ikadhibitika kuwa maandalizi ni hafifu na pesa hazionekani......kama si muheshimiwa rais kutoa milioni 900 kwenye fungu la ku market utalii na kugharamia yale mashindano...Taifa lingeingia aibu kubwa ....na cha ajabu pamoja na ufujaji uliofanyika jamaa hawakuchukuliwa hatua.....hawa Lino kwa zaidi ya miaka kumi wamekuwa wakifanya usanii ,ipo siku mashindano yatakosa udhamini...kwani inavyoonekana sasa wanapata huo udhamini kwa ajili ya ten percents wanazowapa wakuu wa marketings ..kwa kashfa hizi ipo siku wenye makampuni watakataa kudhamini na kama ambavyo Miss Utalii ..siku hizi ilivyokosa wadhamini....
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...