Ujumbe wa Tanzania Watembelea Ubalozi Misri

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

WAZIRI DKT. NDUMBARO AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA WATEMBELEA UBALOZI MISRI KATIKA KUPIGA KURA NCHI MWENYEJI MASHINDANO YA AFCON 2027

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Septemba 25, 2023 ameongoza ujumbe wa Tanzania kutembelea Ubalozi Cairo nchini Misri kabla ya siku ya kupiga kura ya kupata nchi mwenyeji wa Mashindano ya Afrika (AFCON 2027) itakayopigwa Septemba 27, 2023 nchini humo.

Dkt. Ndumbaro amesema Tanzania, Kenya na Uganda kupitia Marais wa nchi hizo wako tayari kwa ajili ya mashindano hayo kwa kuwa zina mazingira mazuri ikiwemo miundombinu ya michezo ambayo ipo na inakidhi mashindano hayo, usafiri na malazi ya kutosha katika nchi hizo unaochagizwa na maeneo mazuri ya Utalii.

Naye Mhe. Balozi wa Tanzania nchini humo Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema atahakikisha anawashawishi Mabalozi wa nchi mbalimbali kuunga mkono fursa hiyo adhimu kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Aidha, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Wallace Karia amesema nchi hizo zinayo nafasi ya kushinda kwakua hazijawahi kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ambapo amesema viwanja tisa vitatumika katika nchi hizo.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha amesema wanaendelea kushirikiana na wajumbe watakaopiga kura ili kuzipa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki nafasi ya kuandaa kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa michuano hiyo mwaka 1957.

Tanzania, Kenya na Uganda zimeungana kupitia maombi ya EA Pamoja Bid 2027 ili kutimiza azma ya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo makubwa Afrika.

F637lHMWMAAw5oq.jpg
F637lUdX0AAv-i-.jpg
F637ljfW8AA6R_m.jpg
 
Back
Top Bottom