Hoja nzito: Tuwe wawazi na tufunguke

Hoja nzito: Tuwe wawazi na tufunguke

Nafunguka
Mtani tolea dhamana.??

Kwa nini wezi wanajikusanya?? Kwa nn anawakusanya watu wasio na uadilifu. Alafu anaidhinisha fedha atakavyo?

Eti hataki wafanya biashara wawe na pesa!!
Sasa watafanyaje business?
Wezi gani wamejikusanya? Kumbuka Serikali inaongozwa na wanadamu, haiwezekani wote wakawa waadilifu 100%, lakini tukiwa na wachache waadilifu akiwemo kiongozi wetu wa nchi Rais Magufuli, atawanyoosha hawa ambao sio waadilifu.
Rais hajakataa wafanya biashara kuwa na pesa, wawe na mapesa lakini yawe ni ya halali na walipe kodi. Tatizo lenu watu kama ninyi mlifikiri biashara ni ujanja ujanja na uhuni wa kukwepa kodi. Badilisheni mind set zenu na mtaona maisha ni mazuri tu.
 
zipi wakati iptl kila siku inavuta milioni400,lugumi inapeta,meremeta nako kimya wadanganye magamba wenzio wenye jina kama lako
Rais alishasema hafukui makaburi. Isitoshe mkataba wa IPTL hauwezi kuvunjwa, hata wewe unajua hilo vizuri. Mikataba mibovu iliyoingiwa na awamu zilizopita tusimuhusishe Rais Magufuli, yeye hakuwa Rais kipindi hicho. Mbaya zaidi mikataba hiyo inalindwa kwa sheria za biashara za kimataifa, akisema aivunjilie mbali, taifa litaingia katika hasara kubwa.
Tumia akili zako kufikiri japo kidogo tu itakusaidia. Acha ushabiki!
 
Maisha hayana tatizo ila tatizo ni rais asiyejari. Magufuli hajari si kwa jema tu hata kwa baya, yeye hajari. Ni arrogant, careless na negligent
Hizo ni chuki tu binafsi ndio zinakusumbua, huna hoja ya maana. Magufuli amebakiza miaka "9" ya kuendelea kuwa Rais wako, ukatae ama ukubali.
 
Teh teh teh teh, nataka walikua wakiishi kama maraika waishi kama mashetani jibu hilo
Ni sawa ndio, kama pesa walizokuwa wanapata zilikuwa ni zawizi na ukwepaji kodi ndizo zilikuwa zinawapa kiburi ya kuishi kama malaika, kwanini sasa hivi wasiishi kama mashetani? Kama kuna mtu alikuwa anapata pesa yake ya halali na alikuwa anaishi kama malaika ataendelea kuishi kama malaika.
 
Kama una kejeli flan hivi.
Mtu asipolipa kodi ndio anapigwa hivyo?
Tuweke wazi kama wewe ni kada au bavicha?
Hawa watu wawili ni wafia vyama, sio vema kubishana nao
Sina kadi ya chama chochote kile cha siasa, isipokuwa napenda kutii mamlaka iliyopo, na ikitokea pia CHADOMO wakashika madaraka pia nitawatii na kuwaheshimu.
 
Tumemaliza mwaka mmoja sasa tangu Rais Magufuli aapishwe na kuwa Rais wa tano wa nchi yetu Tanzania. Tokea Rais Magufuli aingie madarakani, amekuwa akichukua hatua mbali mbali za kusafisha nchi kwa kutumia mtindo alioupachika jina la "kutumbua majipu".

Wote tumeshuhudia Rais akichukua maamuzi "magumu" na bila uwoga wala kupepesa macho amefanya mambo ambayo watangulizi wake hawakuthubutu kufanya ama hata hawakuota kufanya hivyo. Mambo yote aliyoyafanya Rais Magufuli wote tunayafahamu na sina haja ya kuyarudia kuandika hapa sababu nitajaza tu page bila sababu. Sasa twende kwenye hoja yenyewe.

Kumekuwa na malalamiko mengi sana, hasa kwenye vyombo vya habari, hasa vile ambavyo vinamilikiwa na watu ambao naweza kusema wako "mlengo wa kushoto" na pia kwenye mitandao ya kijamii hasa humu JF, kuwa Rais Magufuli amelitumbukiza taifa kwenye "ukata" mkubwa sana wa fedha. Malalamiko mengi ni kuwa eti, Wananchi hawana pesa mifukoni, biashara zinashindwa kujiendesha, mabenki yanafilisika, watu wanafukuzwa kazi, mzunguko wa pesa umekuwa mdogo na mengine mengi.

Nafikiri umefika wakati sasa kila mmoja aliyemo humu JF "afunguke" bila woga na atueleze ni jinsi gani na kwa namna gani ameathirika moja kwa moja na maamuzi yaliyokwisha chukuliwa na Rais Magufuli. Nataka tufunguke na kila mtu anayelalamika humu JF aseme namna alivyoguswa na Mheshimiwa Rais, kiasi kwamba sasa anaona "maisha ni machungu". Tusilalamike kijumla jumla tu, kila mmoja, "as an individual" aseme kilichomsibu kama ni kutumbuliwa yeye au kama ni kutumbuliwa mtu aliyekuwa anamtegemea. Na sio lazima iwe kutumbuliwa, labda kuna kodi fulani imekuwa mzigo kwako, labda biashara imeyumba, tuwe wawazi ili tujue kama ni kweli malalamiko ya watu ni "genuine".

Binafsi naweza kusema mimi sijaathirika na hatua zote zote alizochukua Rais na maamuzi yake hayajanigusa kwa namna yoyote ile. Nathubutu kusema kuwa maisha yangu hayana tofauti kabla na baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani. Zaidi sana naona kama bidhaa zimeshuka bei na upatikanaji wa vyakula, viwanja vya kujenga nyumba, na huduma zimeboreka zaidi.

Naomba sasa kila mmoja aseme yake ya moyoni na tujadili bila matusi, wala kashfa.
Kila mmoja wetu akileta humu yanayomsibu ndio utaamini??

Unaonaje ikitosha tu kusema kuwa mtazamo wako unatosha sana kuwakilisha kilio cha Watanzania mil 50!!

Kifupi naomba uamini kuwa wote hatujaathirika! Hongera mama
 
Sawa inawezekana hayo yamekutokea wewe, lakini bado kuna maswali ya kukuuliza, Mtoto wako amekosa mkopo kwa kuonewa tu, ama hajakidhi vigezo vilivyowekwa? Ninavyojua mimi wanafunzi waliokidhi vigezo wamepata mikopo. Kuhusu biashara kuwa ngumu na wateja kukosekana, labda nikuulize, hivi unafikiri ni sahihi watu waachiwe waendelee kupiga dili ili sisi wafanya biashara tunufaike? Unafikiri ni sahihi uchumi wa nchi yetu ukishikiliwa na wakwepa kodi na wapiga dili?
 
Rais alishasema hafukui makaburi. Isitoshe mkataba wa IPTL hauwezi kuvunjwa, hata wewe unajua hilo vizuri. Mikataba mibovu iliyoingiwa na awamu zilizopita tusimuhusishe Rais Magufuli, yeye hakuwa Rais kipindi hicho. Mbaya zaidi mikataba hiyo inalindwa kwa sheria za biashara za kimataifa, akisema aivunjilie mbali, taifa litaingia katika hasara kubwa.
Tumia akili zako kufikiri japo kidogo tu itakusaidia. Acha ushabiki!
pinochet alihukumiwa kwa mabaya aliyo yafanya kipindi cha utawala wake kuwalinda walio pita kwa msingi wakuto fukua makaburi ni ujinga uleule wa miaka nenda rudi,
 
Enzi hizo watumishi walipandishwa mishahara kila julai lkn tangu aingie mshahara haujapanda bali tumefanya uhakiki zaidi ya mara tano kwa garama zetu za nauli,chakula na udulufishaji.aidha ilikuwa rahisi ukilima vitunguu majira haya ni 1500 mpaka 2000,leo ni 600 mpaka800.
Hata hivyo mtumishi ukiaagizwa nje ya kituo ulikuwa unalipwa ila sasa hulipwi,kulikuwa na semina mafunzo kazini ambapo watu walilipwa na hata fedha za usimamizi zimepungua,
Shambani kupata kibarua sasa sii rahsi tena,kumbuka kulikuwa na mikutano ya vyama vya siasa wakati wa mkutano watu husafiri,hula na kulala hvo wenyeji hunufaika sasa hakuna movements.dawa zahanati mara nyingi hukosa unaagizwa ukanunue hata kama una bima na kila mwezi unakatwa nasikia hivi karibuni 15% ya mshahara itakatwa.ss madhala hapo hayatakuwepi?
Usiseme wafanyakazi sema mimi na wengine . . . . Ukiniuliza mimi wangu haukuwahi kupanda for more than 5 years na wengine kama mimi . . .
 
Tumemaliza mwaka mmoja sasa tangu Rais Magufuli aapishwe na kuwa Rais wa tano wa nchi yetu Tanzania. Tokea Rais Magufuli aingie madarakani, amekuwa akichukua hatua mbali mbali za kusafisha nchi kwa kutumia mtindo alioupachika jina la "kutumbua majipu".

Wote tumeshuhudia Rais akichukua maamuzi "magumu" na bila uwoga wala kupepesa macho amefanya mambo ambayo watangulizi wake hawakuthubutu kufanya ama hata hawakuota kufanya hivyo. Mambo yote aliyoyafanya Rais Magufuli wote tunayafahamu na sina haja ya kuyarudia kuandika hapa sababu nitajaza tu page bila sababu. Sasa twende kwenye hoja yenyewe.

Kumekuwa na malalamiko mengi sana, hasa kwenye vyombo vya habari, hasa vile ambavyo vinamilikiwa na watu ambao naweza kusema wako "mlengo wa kushoto" na pia kwenye mitandao ya kijamii hasa humu JF, kuwa Rais Magufuli amelitumbukiza taifa kwenye "ukata" mkubwa sana wa fedha. Malalamiko mengi ni kuwa eti, Wananchi hawana pesa mifukoni, biashara zinashindwa kujiendesha, mabenki yanafilisika, watu wanafukuzwa kazi, mzunguko wa pesa umekuwa mdogo na mengine mengi.

Nafikiri umefika wakati sasa kila mmoja aliyemo humu JF "afunguke" bila woga na atueleze ni jinsi gani na kwa namna gani ameathirika moja kwa moja na maamuzi yaliyokwisha chukuliwa na Rais Magufuli. Nataka tufunguke na kila mtu anayelalamika humu JF aseme namna alivyoguswa na Mheshimiwa Rais, kiasi kwamba sasa anaona "maisha ni machungu". Tusilalamike kijumla jumla tu, kila mmoja, "as an individual" aseme kilichomsibu kama ni kutumbuliwa yeye au kama ni kutumbuliwa mtu aliyekuwa anamtegemea. Na sio lazima iwe kutumbuliwa, labda kuna kodi fulani imekuwa mzigo kwako, labda biashara imeyumba, tuwe wawazi ili tujue kama ni kweli malalamiko ya watu ni "genuine".

Binafsi naweza kusema mimi sijaathirika na hatua zote zote alizochukua Rais na maamuzi yake hayajanigusa kwa namna yoyote ile. Nathubutu kusema kuwa maisha yangu hayana tofauti kabla na baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani. Zaidi sana naona kama bidhaa zimeshuka bei na upatikanaji wa vyakula, viwanja vya kujenga nyumba, na huduma zimeboreka zaidi.

Naomba sasa kila mmoja aseme yake ya moyoni na tujadili bila matusi, wala kashfa.
Mimi teyali nimeshajadili moyoni nimetosheka na moyo umejaa
 
Walioahidi mabadiliko ndio wa kwanza kuwaibia wananchi.

Mbowe lini unalipa kodi zetu za Nhc?
 
mmmmmmh nimesoma coment sijaona hata alie toa jibu la maswali uliyouliza. wanazunguka zunguka tu.
kwa kifupi upinzani uchwara usio kua na sera ndo unaowapoteza watu wenye ushabiki tu usio na tija. hawajui wakitakacho.
 
Hizo ni chuki tu binafsi ndio zinakusumbua, huna hoja ya maana. Magufuli amebakiza miaka "9" ya kuendelea kuwa Rais wako, ukatae ama ukubali.
Ndugu yangu nimefurahia namna unavo jibu hoja nakutoa hoja ila umekosea kidogo ulivo sema mh rahasi kabakisha miaka 9.Nimiaka minne (4) iliyo baki la cvyo utaharibu hoja zako zote zikawa kama ulivokosea kwenye ishu ya miaka iliyo baki kwa mh rais kututumikia.OMBI TENGUA MANENO YAKO ILI TUENDE PAMOJA.
 
Ntombi,Majuha wanajihesabia kuishi milele madarakani,wanasahau kilichomkuta raisi wa Gambia wiki hii
 
Kutumia kwake vyombo vya dola kumekuathiri vipi wewe kimaisha? Umelala njaa? Umeshindwa kupeleka watoto shule? Kuvaa kwake sare za jeshi ndio kumefanya wewe usiwe na pesa mfukoni? Tuambie kinaga ubaga ndugu yetu, umeathirika vipi?
imekuwa rais km kwa jirani wa mzee wa upako.Unamwita mlevi sirini anatoka hadharani akiwa kalewa na kathibitisha mwenyewe.Unamwiata dictator uchwara anatoa majeshi hadharani, unasema umeota ndoto anakimbizana na ndoto.
 
Back
Top Bottom