Hoja nzito: Tuwe wawazi na tufunguke

Ki ukweli umeongea vizuri sana na mimi binafsi sijaathirika na kitu chochote zaidi ya kuona dawa zimepungua bei, viwanja vimepungua bei na nikienda katika hosptali na office za serikali napata huduma kwa urahisi zaidi ya zamani
Hospital kuna dawa??
 
Kwa Mimi sijaathirika na utumbuaji Wa hao waliotumbuliwa na mh, Rais kwani ukiona umetumbuliwa ujue ridhiki yako hapo ndo mwisho wake kwenye hiyo kazi tafuta kwingine, pia Kwa hao waliotumbuliwa walishawafukuza watu kazi hasa watumishi wadogo na maisha yakasonga
 
Hizo ni chuki tu binafsi ndio zinakusumbua, huna hoja ya maana. Magufuli amebakiza miaka "9" ya kuendelea kuwa Rais wako, ukatae ama ukubali.
Mbona umeanza kuwa mkali? Taratibu hii kauli yako ya "ukatae ama ukubali"mmh!!! Si bure!!!
 
Ndugu yangu nimefurahia namna unavo jibu hoja nakutoa hoja ila umekosea kidogo ulivo sema mh rahasi kabakisha miaka 9.Nimiaka minne (4) iliyo baki la cvyo utaharibu hoja zako zote zikawa kama ulivokosea kwenye ishu ya miaka iliyo baki kwa mh rais kututumikia.OMBI TENGUA MANENO YAKO ILI TUENDE PAMOJA.
Mi pia nimemshangaa!!!
 
Ukweli huu hapa:
Whether unaijua sababu au la, ila ukweli ni kwamba hela ya kutosha haipo kwenye mzunguko. Na hii inasababisha wale wasio na ajira rasmi kuteseka. Mfano, muosha magari, muuza bidhaa luxury, mfanyakazi ngumu, vibarua, etc.
Hivyo pia waliopo kwenye ajira isiyo rasmi ndo wanaolalamika.
So whether you give a shit or not, these people are really suffering. Tena hao hao wanyonge.
Remember... You cant fool all people all the time
 
Tumemaliza mwaka mmoja sasa tangu Rais Magufuli aapishwe na kuwa Rais wa tano wa nchi yetu Tanzania. Tokea Rais Magufuli aingie madarakani, amekuwa akichukua hatua mbali mbali za kusafisha nchi kwa kutumia mtindo alioupachika jina la "kutumbua majipu".

Wote tumeshuhudia Rais akichukua maamuzi "magumu" na bila uwoga wala kupepesa macho amefanya mambo ambayo watangulizi wake hawakuthubutu kufanya ama hata hawakuota kufanya hivyo. Mambo yote aliyoyafanya Rais Magufuli wote tunayafahamu na sina haja ya kuyarudia kuandika hapa sababu nitajaza tu page bila sababu. Sasa twende kwenye hoja yenyewe.

Kumekuwa na malalamiko mengi sana, hasa kwenye vyombo vya habari, hasa vile ambavyo vinamilikiwa na watu ambao naweza kusema wako "mlengo wa kushoto" na pia kwenye mitandao ya kijamii hasa humu JF, kuwa Rais Magufuli amelitumbukiza taifa kwenye "ukata" mkubwa sana wa fedha. Malalamiko mengi ni kuwa eti, Wananchi hawana pesa mifukoni, biashara zinashindwa kujiendesha, mabenki yanafilisika, watu wanafukuzwa kazi, mzunguko wa pesa umekuwa mdogo na mengine mengi.

Nafikiri umefika wakati sasa kila mmoja aliyemo humu JF "afunguke" bila woga na atueleze ni jinsi gani na kwa namna gani ameathirika moja kwa moja na maamuzi yaliyokwisha chukuliwa na Rais Magufuli. Nataka tufunguke na kila mtu anayelalamika humu JF aseme namna alivyoguswa na Mheshimiwa Rais, kiasi kwamba sasa anaona "maisha ni machungu". Tusilalamike kijumla jumla tu, kila mmoja, "as an individual" aseme kilichomsibu kama ni kutumbuliwa yeye au kama ni kutumbuliwa mtu aliyekuwa anamtegemea. Na sio lazima iwe kutumbuliwa, labda kuna kodi fulani imekuwa mzigo kwako, labda biashara imeyumba, tuwe wawazi ili tujue kama ni kweli malalamiko ya watu ni "genuine".

Binafsi naweza kusema mimi sijaathirika na hatua zote zote alizochukua Rais na maamuzi yake hayajanigusa kwa namna yoyote ile. Nathubutu kusema kuwa maisha yangu hayana tofauti kabla na baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani. Zaidi sana naona kama bidhaa zimeshuka bei na upatikanaji wa vyakula, viwanja vya kujenga nyumba, na huduma zimeboreka zaidi.

Naomba sasa kila mmoja aseme yake ya moyoni na tujadili bila matusi, wala kashfa.
Muachieni kwanza kiongozi wa JF,halafu ndio tuendelee na mjadala
 
Kwa kuzuia kuuza mchele nje ya nchi kumesababisha soko la ndani kujaa mchele hivo kusababisha bei kushuka wafanyabiashara wa kati wametukimbia nimeleta mchele hapo mjini kwenu dar nimekuta umejaa wanadai hamna mzunguko wa pesa matokeo yake nimeuza kwa hasara msimu kwetu tumeanaza kulima hatuna uhakika wa soko na ndani nini gunia 4elfu za mpunga najiuliza nipunguze heka au niongeze napata wakati mgumu nikifikiria serikali hainisaidii katika kilimo changu lakini kwenye kuuza inaniwekea vikwazo waacheni hao wanunuzi wa nje waje kwetu huku mashambani huyo raisi yeye atumbue akusanye kodi abane matumizi apige vita rushwa hiyo naunga mkono lakini kwa sisi wakulima wa mpunga atupe uhuru wa kuuza popote hata kama ni italia kama anatudai haina shida lakini kutupangia lazima tuuze ndani hio ni shida matokeo yake walanguzi wanatuumiza zamani wanunuzi wa nje walikua wanakuja kwetu na mlanguzi alikua hapati kitu
 
Back
Top Bottom