Hoja nzito: Tuwe wawazi na tufunguke

Hoja nzito: Tuwe wawazi na tufunguke

Tatizo la nchi hii sio watu kukataa kulipa kodi ila watu wanakwepa kulipa kodi zisizo na ulazima ambazo mwishowake ukizilipa kama mfanyabiashara lazima ufirisike au upate hasara...
Inakuaje landrover discovery 3 used kodi yake hapa bongo ni zaidi ya milion 25 wakati hapo msumbiji/malawi haifiki milion 10,ajabu sana.
 
Ukisoma andiko lako ni rahisi kubaini kuwa haukuwa huru wakati ukiandika, na hilo ndilo kosa lako la kwanza. Kwenye hoja yangu hakuna mahali nimeandika "kuzuiwa kufanya kazi", mimi nilitumia neno "kudhibitiwa",niliandika hivyo kwa sababu maalum ingawa ukweli ambao hata wewe unaufahamu ni kwamba kuna taasisi ambazo zimezuiliwa kufanya kazi zake kwa ukamilifu hadi mwaka 2020, unataka na hili upewe facts za namna gani?

Unasema wewe binafsi hujaathirika, ok sawa! Lakini unafikiri utakuwa umeandika ukweli iwapo kuna maelfu ya wanafunzi wameshindwa kupewa mikopo licha ya kuwa walistahili kupata? (kumbuka kuna wanafunzi wa mwaka wa pili ambao walipewa mkopo mwaka jana leo wanapigwa danadana), huku ikizingatiwa wakati wa kampeni Rais wetu aliahidi hakuna mwanafunzi atakayekosa mkopo, tena kwa msisitizo mkubwa. Hata vilio vya wanafunzi hawa vinashindwa kukugusa? Kuna makampuni yanafunga shughuli zake, hivyo kuna idadi kubwa ya watu wamegeuka ghafla kuwa wategemezi kwa ndugu na jamaa zao-hili nalo halikugusi wewe? Kama unafikiri sawa sawa unadhani nini matokeo hasi ya idadi kubwa ya watu ambao wanaondoka kwenye ajira kutokana na kufungwa kwa biashara?

Ni vigumu kujadiliana na wewe kwa kuwa from the beginning umevaa miwani ya mbao na kujificha katika "ubinafsi" ambao umekuwa sababisho kubwa la matatizo mengi katika jamii zetu. Wewe hapo unadai hujaathiriwa hata kidogo na utendaji wa serikali wakati kuna maeneo mengi hayajakaa vizuri yanahitaji kuwekwa sawa! Sijui katika andiko lako na majibu ya wachangiaji mbalimbali ni nani amejidhihirisha kuwa na ushabiki na bendera fuata upepo. Ni amini wanasoma michango yako na ya wengine watakuwa katika nafasi ya kutoa jibu!
Ndugu, ndio maana nimesema huu ni ushabiki tu, Tukianza na swala la baadhi ya taasisi "kudhibitiwa" hilo sio kweli, rejea hotuba ya Rais Magufuli akiwa Singida kama sikosei, alisema "hajazui siasa, isipokuwa tu kila mbunge afanye siasa kwenye jimbo lake". Alichofanya Rais na Serikali yake ni "kudhibiti" maandamano ya kisiasa ambayo hayana tija kwa ustawi wa taifa letu. Na sheria zinaliruhusu jeshi la polisi kuzuia kufanyika kwa maandamano ambayo yanaonekana yanaweza kuhatarisha amani. By the way, Watanzania ili tuendelee hatuhitaji maandamano, tunahitaji kufanya kazi kwa bidii na kulipa kodi stahiki.

Rais aliahidi ndio kuwa hakuna mwanafunzi atakayekosa mkopo, lakini kwa kumbukumbu zangu, hakuna mahali Rais aliahidi kuwapa mkopo wanafunzi wasiokuwa na vigezo. Tukubali ukweli na itatusaidia sana, wanafunzi walionyimwa mikopo hawana vigezo vya kupata hiyo mikopo, ama wameshindwa kutimiza taratibu zilizowekwa na bodi ya mikopo. Ndio maana nasema tena tuache ushabiki wa kijinga. Let say, mwanafunzi wa mwaka wa pili amekosa mkopo. Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa hawa wanafunzi wa mwaka wa pili, mwaka jana walipewa mikopo "kimagumashi" tu, na imegundulika sasa kuwa kumbe hata mwaka jana hawakushahili kupewa hiyo mikopo. Sasa kwa mawazo yako unataka kusema sababu mwaka jana bodi ilikosea ikawapa mikopo na mwaka huu irudie kosa hilo hilo, iwape tu huo mkopo wasiostahili kupewa??

Unasema eti kuna kampuni zinafunga biashara; sasa kama zilikuwa hazilipi kodi na zilizoea kufanya biashara kiujanja ujanja tu, kwanini sasa hivi zisifunge biashara? Huu ndio wakati ambao tutajua kampuni zilizokuwa na utamaduni wa kujiendesha kihalali na zile zilizokuwa zinategemea mitaji ya pesa za "dili". Hapo kwenye biashara wala tusidanganyane kabisa. Wafanya biashara wengi walikuwa wanakwepa kodi sana na ndio maana sasa hivi wanalia lia. Wacha wafunge waondoke zao, watabakia wale wenye kuheshimu sheria za nchi na maisha yataendelea. Serikali haiwezi kuacha kusimamia sheria zake kwa kisingizio cha kuwaonea huruma watu. Hata siku moja, ukiona Serikali inafanya hivyo, basi ujue kuwa hiyo Serikali ni dhaifu sana.

Fahamu pia kwamba Serikali ya Rais Magufuli haiwezi kumaliza kero zote za wananchi ndani ya mwaka mmoja. Ni kweli kwamba kuna mambo ambayo bado hayajakaa sawa na hili linahitaji muda. Alichokifanya Rais Magufuli ni kama vile Daktari anavyomfanyia mtu upasuaji wa kuondoa uvimbe tumboni, mtu huyu haponi siku hiyo hiyo baada ya kufanyiwa upasuaji. Inachukua muda mrefu kupona na mtu huyu ataendelea kusikia maumivu ile sehemu aliyopasuliwa. Ndicho kinachotokea kwa baadhi ya Watanzania leo, watasikia maumivu lakini baadae wakipona watamshukuru Rais Magufuli, It's just a matter of time.
 
Me tenda za kujenga sijapata kabisa tokea Mradi Wa manji coco beach anyang'anywe, na makontena hayaji tena kwenye dry port yetu dah na tenda iliyobakia ya kushona uniform za magereza deal kwishnei..
 
kuwa na raisi muoga alafu kiburi jeuri roho mbaya
Uwoga wake ni upi? Kiburi chake ni kipi? Roho mbaya yake ni ipi? Kukusanya kodi, kupambana na wala rushwa, kubana matumizi ya hovyo ya pesa za umma, Kununua ndege, kusomesha watoto bure mpaka form 4, kuhamasisha utengenezaji wa madawati, kuwaondoa wafanyakazi hewa na kuwatumbua wapiga dili ndio amekuwa na roho mbaya?? Fafanua mkuu, mimi binafsi sioni roho mbaya yake iko wapi. Lakini kama wewe ulikuwa ni mmoja wa wapiga dili, au mfanyakazi hewa au mla rushwa na mkwepa kodi, lazima utasema Rais ana roho mbaya.
 
Kiujumla naweza kusema kiongizi wetu hajui vizur falsafa za uchumi na maendeleo.
Ukusanyaji wa kodi sana afu kukosa njia ya kuzipeleka hela kwa wananchi kumeathiri sana mzunguko wa uchumi.
Mm binafsi ninaathirika na vitu vifuatavyo.
Kupanda kwa bei ya vyakula hasa unga wa mahindi na sukari hii imesababishwa na ushuru mkubwa uliowekwa kwenye bidhaa hizi mhimu.
Kwasasa kg25 ya unga inauzwa 30000 kutoka 18000 ya mwaka jana hii imepelekea pumba tu kuuzwa 25000 kwa gunia,
Madhara yake kwangu ni kuwa kwasasa nimeamua kusitisha ufugaji wa kuku kwasababu gharama imeongrzeka sana kiasi cha kukosa faida kabisa.
Kukosekana kwa pesa mtaani kumefanya niwe na kundi kubwa la ndugu hasa wazazi wanaohitaji msaada najikuta ata kama Nina 500000 nashindwa kuifanyia chochote.
Kama unasema maamzi ya rais hayajakuathiri kwa chochote basi utakuwa mnafiki mkubwa au unategemea mshahara wa mwisho wa mwezi na haupo kwenye mifumo ya kibiashara.

Kiongozi wetu ameshindwa kubalance kabisa kati ya import na export, na akiendelea hivi miaka miwili ijayo Tanzania itakuwa soko la ombaomba.
 
Tumemaliza mwaka mmoja sasa tangu Rais Magufuli aapishwe na kuwa Rais wa tano wa nchi yetu Tanzania. Tokea Rais Magufuli aingie madarakani, amekuwa akichukua hatua mbali mbali za kusafisha nchi kwa kutumia mtindo alioupachika jina la "kutumbua majipu".

Wote tumeshuhudia Rais akichukua maamuzi "magumu" na bila uwoga wala kupepesa macho amefanya mambo ambayo watangulizi wake hawakuthubutu kufanya ama hata hawakuota kufanya hivyo. Mambo yote aliyoyafanya Rais Magufuli wote tunayafahamu na sina haja ya kuyarudia kuandika hapa sababu nitajaza tu page bila sababu. Sasa twende kwenye hoja yenyewe.

Kumekuwa na malalamiko mengi sana, hasa kwenye vyombo vya habari, hasa vile ambavyo vinamilikiwa na watu ambao naweza kusema wako "mlengo wa kushoto" na pia kwenye mitandao ya kijamii hasa humu JF, kuwa Rais Magufuli amelitumbukiza taifa kwenye "ukata" mkubwa sana wa fedha. Malalamiko mengi ni kuwa eti, Wananchi hawana pesa mifukoni, biashara zinashindwa kujiendesha, mabenki yanafilisika, watu wanafukuzwa kazi, mzunguko wa pesa umekuwa mdogo na mengine mengi.

Nafikiri umefika wakati sasa kila mmoja aliyemo humu JF "afunguke" bila woga na atueleze ni jinsi gani na kwa namna gani ameathirika moja kwa moja na maamuzi yaliyokwisha chukuliwa na Rais Magufuli. Nataka tufunguke na kila mtu anayelalamika humu JF aseme namna alivyoguswa na Mheshimiwa Rais, kiasi kwamba sasa anaona "maisha ni machungu". Tusilalamike kijumla jumla tu, kila mmoja, "as an individual" aseme kilichomsibu kama ni kutumbuliwa yeye au kama ni kutumbuliwa mtu aliyekuwa anamtegemea. Na sio lazima iwe kutumbuliwa, labda kuna kodi fulani imekuwa mzigo kwako, labda biashara imeyumba, tuwe wawazi ili tujue kama ni kweli malalamiko ya watu ni "genuine".

Binafsi naweza kusema mimi sijaathirika na hatua zote zote alizochukua Rais na maamuzi yake hayajanigusa kwa namna yoyote ile. Nathubutu kusema kuwa maisha yangu hayana tofauti kabla na baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani. Zaidi sana naona kama bidhaa zimeshuka bei na upatikanaji wa vyakula, viwanja vya kujenga nyumba, na huduma zimeboreka zaidi.

Naomba sasa kila mmoja aseme yake ya moyoni na tujadili bila matusi, wala kashfa.
Yaani umekuja kutoa Feedback ya shughuli zako sio ?
 
na
Uwoga wake ni upi? Kiburi chake ni kipi? Roho mbaya yake ni ipi? Kukusanya kodi, kupambana na wala rushwa, kubana matumizi ya hovyo ya pesa za umma, Kununua ndege, kusomesha watoto bure mpaka form 4, kuhamasisha utengenezaji wa madawati, kuwaondoa wafanyakazi hewa na kuwatumbua wapiga dili ndio amekuwa na roho mbaya?? Fafanua mkuu, mimi binafsi sioni roho mbaya yake iko wapi. Lakini kama wewe ulikuwa ni mmoja wa wapiga dili, au mfanyakazi hewa au mla rushwa na mkwepa kodi, lazima utasema Rais ana roho mbaya.
nataka unambie kapambana na rushwa ipi,sasa unauliza maswali unajijibu wewe huwezi kupata majibu
 
na

nataka unambie kapambana na rushwa ipi,sasa unauliza maswali unajijibu wewe huwezi kupata majibu
Jitihada zake zote anazofanya wewe huzioni? Hatua zote alizochukua mpaka sasa wewe huzijui??
 
Sijakuelewa mkuu, picha yako inamaanisha nini? Au ni wewe huyo unayepigwa na hao askari kanzu? Ulifanya nini ndugu, ulikwepa kulipa kodi? Au na wewe uliota maono? Funguka ndugu, tujadili.
Kama una kejeli flan hivi.
Mtu asipolipa kodi ndio anapigwa hivyo?
Tuweke wazi kama wewe ni kada au bavicha?
Hawa watu wawili ni wafia vyama, sio vema kubishana nao
 
Maisha hayana tatizo ila tatizo ni rais asiyejari. Magufuli hajari si kwa jema tu hata kwa baya, yeye hajari. Ni arrogant, careless na negligent
 
Nafunguka
Mtani tolea dhamana.??

Kwa nini wezi wanajikusanya?? Kwa nn anawakusanya watu wasio na uadilifu. Alafu anaidhinisha fedha atakavyo?

Eti hataki wafanya biashara wawe na pesa!!
Sasa watafanyaje business?
 
Sichangii tena hii thread
Mnafuta my idea why ? Mod
 
Ki ukweli umeongea vizuri sana na mimi binafsi sijaathirika na kitu chochote zaidi ya kuona dawa zimepungua bei, viwanja vimepungua bei na nikienda katika hosptali na office za serikali napata huduma kwa urahisi zaidi ya zamani
Mkuu kwaiyo vile viwanja vya mil 300 saiv havipo tena sio?? Bongo raha sana saiv kwa kweli basi..
 
Back
Top Bottom