Hoja nzito: Tuwe wawazi na tufunguke

Hoja nzito: Tuwe wawazi na tufunguke

Ifungwe na nani na kwanini ifungwe? Wewe funguka ukweli wako na JF haiwezi kufungwa hata siku moja. Acha uwoga, hakuna anayekujua humu ndani. Tuambie, utendaji wa Rais umekuathiri vipi wewe kama wewe?
We nawe! Unauliza nazi kisiju?Una lako jambo si bure.Ambaye amejiandaa kwa. kazi ngumu asogee huku achangie hii hoja.Inaonyesha mwenzetu ana shamba la sukari .Hata kama anatumia asali bei ya mizinga iko pale pale?
 
siki zote mzunguko wa pesa unaanzi serikalini kama rais mwenyewe alilamika kwamba hali ni mbaya na w watu wameficha hela. na benki mengine nayo yatatangaza kifilisika. ivi unafikiri kwa mwananchi wa kawaida ataponea wapi?
 
Tumemaliza mwaka mmoja sasa tangu Rais Magufuli aapishwe na kuwa Rais wa tano wa nchi yetu Tanzania. Tokea Rais Magufuli aingie madarakani, amekuwa akichukua hatua mbali mbali za kusafisha nchi kwa kutumia mtindo alioupachika jina la "kutumbua majipu".

Wote tumeshuhudia Rais akichukua maamuzi "magumu" na bila uwoga wala kupepesa macho amefanya mambo ambayo watangulizi wake hawakuthubutu kufanya ama hata hawakuota kufanya hivyo. Mambo yote aliyoyafanya Rais Magufuli wote tunayafahamu na sina haja ya kuyarudia kuandika hapa sababu nitajaza tu page bila sababu. Sasa twende kwenye hoja yenyewe.

Kumekuwa na malalamiko mengi sana, hasa kwenye vyombo vya habari, hasa vile ambavyo vinamilikiwa na watu ambao naweza kusema wako "mlengo wa kushoto" na pia kwenye mitandao ya kijamii hasa humu JF, kuwa Rais Magufuli amelitumbukiza taifa kwenye "ukata" mkubwa sana wa fedha. Malalamiko mengi ni kuwa eti, Wananchi hawana pesa mifukoni, biashara zinashindwa kujiendesha, mabenki yanafilisika, watu wanafukuzwa kazi, mzunguko wa pesa umekuwa mdogo na mengine mengi.

Nafikiri umefika wakati sasa kila mmoja aliyemo humu JF "afunguke" bila woga na atueleze ni jinsi gani na kwa namna gani ameathirika moja kwa moja na maamuzi yaliyokwisha chukuliwa na Rais Magufuli. Nataka tufunguke na kila mtu anayelalamika humu JF aseme namna alivyoguswa na Mheshimiwa Rais, kiasi kwamba sasa anaona "maisha ni machungu". Tusilalamike kijumla jumla tu, kila mmoja, "as an individual" aseme kilichomsibu kama ni kutumbuliwa yeye au kama ni kutumbuliwa mtu aliyekuwa anamtegemea. Na sio lazima iwe kutumbuliwa, labda kuna kodi fulani imekuwa mzigo kwako, labda biashara imeyumba, tuwe wawazi ili tujue kama ni kweli malalamiko ya watu ni "genuine".

Binafsi naweza kusema mimi sijaathirika na hatua zote zote alizochukua Rais na maamuzi yake hayajanigusa kwa namna yoyote ile. Nathubutu kusema kuwa maisha yangu hayana tofauti kabla na baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani. Zaidi sana naona kama bidhaa zimeshuka bei na upatikanaji wa vyakula, viwanja vya kujenga nyumba, na huduma zimeboreka zaidi.

Naomba sasa kila mmoja aseme yake ya moyoni na tujadili bila matusi, wala kashfa.
ila hayo maswali umeuliza kikejeli.
kwasababu unauliza kitu ambacho unakifahamu.
 
We nawe! Unauliza nazi kisiju?Una lako jambo si bure.Ambaye amejiandaa kwa. kazi ngumu asogee huku achangie hii hoja.Inaonyesha mwenzetu ana shamba la sukari .Hata kama anatumia asali bei ya mizinga iko pale pale?
Nimecheka sana, kumbe kuna waoga humu JF! Sikia mkuu, kinachonikera ni kusikia watu wanalalamika eti, maisha magumu sababu ya maamuzi aliyochukua Rais Magufuli, kitu ambacho sio kweli hata kidogo. Kama wewe ulikuwa unaendesha maisha yako kwa njia halali sasa kwanini useme maisha yamekuwa magumu? Mimi ninavyojua Rais amefanya makubwa sana ndani ya mwaka mmoja kupambana na wakwepa kodi, wala rushwa, wapiga dili, wafanyakazi hewa, wanafunzi hewa, matumizi mabovu ya pesa za umma, uzembe kwa watumishi wa umma, na mengine mengi tu. Sasa hatua hizi zenye lengo zuri kabisa kwa mustakabali wa Taifa letu zimekuathiri vipi wewe?
Wengine wanalalamikia Rais kufufua shirika letu la ndege kwa kununua ndege mpya! sasa tujiulize, Rais Magufuli, asingenunua ndege hizo mpya, Je, wao wangekuwa na hizo pesa mifukoni mwao? au ndio maisha yao yangekuwa mazuri?
 
ila hayo maswali umeuliza kikejeli.
kwasababu unauliza kitu ambacho unakifahamu.
Ninachofahamu mimi ni kwamba maisha yangu hayajaathirika hata kidogo kutokana na utendaji kazi wa Rais Magufuli. Ndio maana nikasema tuwe wawazi, tufunguke, kama wewe umeathirika na utendaji wa Rais, tuambie ni kwa namna gani. Tusilalamike kijumla jumla tu na kishabiki.
 
Naunga mkono t="DAFU NA NDIMU, post: 18735060, member: 382003"]Kupungua kwa mbs za kubishania kwenye mitandao[/QUOTE]
Naybga
 
siki zote mzunguko wa pesa unaanzi serikalii kama rais mwenyewe alilamika kwamba hali ni mbaya na w watu wameficha hela. na benki mengine nayo yatatangaza kifilisika. ivi unafikiri kwa mwananchi wa kawaida ataponea wapi?
Hapo kwa wananchi wa kawaida ndio ningependa kusikia mtu akisema, kwa mfano; labda alikuwa anauza duka na alikuwa anafunga hesabu kwa siku laki moja, lakini sasa hivi anafunga hesabu kwa siku elfu ishirini, na hali hii imesababishwa na sababu moja, mbili, na kuendelea. Sio kusema tu, Magufuli, Magufuli, hapana.
 
Rambi rambi za kagera.inatia simanz kweli
Unataka kutuambia kwamba kabla ya hizo "rambirambi za kagera" maisha yako yalikuwa mazuri? Kwa mfano; wewe ungekuwa "muathirika wa tetemeko la ardhi kule Kagera" na ungepewa hiyo rambirambi labda shilingi laki moja au mbili, je kiasi hicho kingefanya leo wewe uwe na maisha mzuri? Halafu shule, hospitali na miundo mbinu mingine ikakosa pesa za ukarabati wewe ungeona ni sawa tu?
 
Naunga mkono t="DAFU NA NDIMU, post: 18735060, member: 382003"]Kupungua kwa mbs za kubishania kwenye mitandao
Naybga[/QUOTE]
Sasa hivi kila vocha ya simu unayonunua inakatwa kodi. Hivyo usiwe na wasiwasi pia inawezekana mb zikapungua, lakini haujatuambia wewe umeathirika vipi na utendaji wa Rais Magufuli. Binafsi, kukatwa kwa kodi kwenye vocha za simu, naona kutaongeza sana pato la taifa na hivyo mwisho wa siku Watanzania wengi watanufaika na maendeleo ya nchi yao. Au wewe unasemaje?
 
Ninachofahamu mimi ni kwamba maisha yangu hayajaathirika hata kidogo kutokana na utendaji kazi wa Rais Magufuli. Ndio maana nikasema tuwe wawazi, tufunguke, kama wewe umeathirika na utendaji wa Rais, tuambie ni kwa namna gani. Tusilalamike kijumla jumla tu na kishabiki.
ww unaweza ukasema haujaathilika kivyovyo kwasababu ni muajiliwa serikalini ww hata hali iwe mbaya vipi mtaani ww huwezi kujua kwasabu mshahara wako unakuwa uko pale pale.
au kama sio muajiliwa basi ww haufanyi biashara yoyote ambayo unalipa mapato serikalini.
 
Mimi binafsi nimefaidika sana maana urasimu umepungua na kule kijijini nilikokua nashinda huku nikiwaeleza kila siku nakusanya malalamiko yenu na yatafika kwa wahusika na kushughulikiwa, kweli malalamiko baadhi yameshapatiwa ufumbuzi na wale ndugu zangu wamekua wananipa mrejesho wa shukrani as if ni kweli mimi nimewasaidia kumbe ni serikali ya JPM ambayo kwa njia zake iliyapata hayo malalamiko na kushugulikia.

Hakuna raha kama kuona kwamba serikali inasikia kilio chako na kwamba ikitokea ukaonewa kuna pakukimbilia...Hii mimi inanipa raha na amani ambayo siwezi kuieleza.
 
ww unaweza ukasema haujaathika kivyovyo kwasababu ni muajiliwa serikalini ww hata hali iwe mbaya vipi mtaani ww huwezi kujua kwasabu mshahara wako unakuwa uko pale pale.
au kama sio muajiliwa basi ww haufanyi biashara yoyote ambayo unalipa mapato serikalini.
Kwani kulipa mapato Serikalini(kodi) ni dhambi? Huoni kama nchi ilikuwa inaelekea pabaya sana kwa wafanya biashara kukwepa kodi? Je, ulipaji kodi ndio umefanya maisha yawe magumu? Kwenye hilo sitaki kuamini.
 
Mimi binafsi nimefaidika sana maana urasimu umepungua na kule kijijini nilikokua nashinda huku nikiwaeleza kila siku nakusanya malalamiko yenu na yatafika kwa wahusika na kushughulikiwa, kweli malalamiko baadhi yameshapatiwa ufumbuzi na wale ndugu zangu wamekua wananipa mrejesho wa shukrani as if ni kweli mimi nimewasaidia kumbe ni serikali ya JPM ambayo kwa njia zake iliyapata hayo malalamiko na kushugulikia.

Hakuna raha kama kuona kwamba serikali inasikia kilio chako na kwamba ikitokea ukaonewa kuna pakukimbilia...Hii mimi inanipa raha na amani ambayo siwezi kuieleza.
Na maisha yako yanaendelea kama kawaida, na mwisho wa siku Wananchi wote watanufaika na maendeleo badala ya wajanja wachache.
 
Na maisha yako yanaendelea kama kawaida, na mwisho wa siku Wananchi wote watanufaika na maendeleo badala ya wajanja wachache.

Mshahara siku hizi napata tarehe 24 ya mwezi badala ya kati ya tarehe 5-11 ya mwezi wa ambao nimeshaufanyia kazi...yaani tarehe ya 40...Pia mshahara wangu ulipanda mara mbili ya ulivyokuwa kwani baada ya harmonization ilionekana nakuwa under paid...tatizo moja tu increament ya mwaka sijapata...ni hayo tu!
 
Unataka kutuambia kwamba tatizo lako wewe ni chama na sio utendaji wa Rais? Kama tatizo ni ccm, hicho chama kimeathiri vipi maisha yako wewe kama wewe sasa hivi, sababu chama hicho hicho ndio kilikuwa madarakani miaka yote iliyopita. Tuambie wewe binafsi, utendaji wa Rais Magufuli umeakuathiri vipi? Usiwaongelee watu wengine.
Namna gani wewe ndugu?.....serikali ya Mgufuli inafuata ilani za fisiemu hujui hata hili? Anaowateuwa nao makada wa chama chake.... nalo hujui?

Siasa siasa tu hakuna lolote la maana.
 
ughwee ulinndemalema
ukuti tujobhe syakutuka po ubhobhoke lero!!
po tukuntila bhabha gwako tutikujobha!!!!
 
Enzi hizo watumishi walipandishwa mishahara kila julai lkn tangu aingie mshahara haujapanda bali tumefanya uhakiki zaidi ya mara tano kwa garama zetu za nauli,chakula na udulufishaji.aidha ilikuwa rahisi ukilima vitunguu majira haya ni 1500 mpaka 2000,leo ni 600 mpaka800.
Hata hivyo mtumishi ukiaagizwa nje ya kituo ulikuwa unalipwa ila sasa hulipwi,kulikuwa na semina mafunzo kazini ambapo watu walilipwa na hata fedha za usimamizi zimepungua,
Shambani kupata kibarua sasa sii rahsi tena,kumbuka kulikuwa na mikutano ya vyama vya siasa wakati wa mkutano watu husafiri,hula na kulala hvo wenyeji hunufaika sasa hakuna movements.dawa zahanati mara nyingi hukosa unaagizwa ukanunue hata kama una bima na kila mwezi unakatwa nasikia hivi karibuni 15% ya mshahara itakatwa.ss madhala hapo hayatakuwepi?
 
Kwani kulipa mapato Serikalini(kodi) ni dhambi? Huoni kama nchi ilikuwa inaelekea pabaya sana kwa wafanya biashara kukwepa kodi? Je, ulipaji kodi ndio umefanya maisha yawe magumu? Kwenye hilo sitaki kuamini.
siku zote wafanya biashara huwa wanalipa kodi na ndio maana mpaka leo nchi ipo.
ila hii serikali ya mwaka huu imekuja kivingine kwanza imejitahidi kujenga uadui na wafanya biashara wakati huo hilo ni kosa kubwa sana. nchi haiwezi kuendelea bila kwenda sawa na wafanya biashara.
 
Back
Top Bottom