HOJA MBADALA: Tuhamasishe CCM imsimamishe Membe 2015?

HOJA MBADALA: Tuhamasishe CCM imsimamishe Membe 2015?

Ukiangalia sana kati ya viongozi wengi wa CCM na walioko serrikalini Membe ndiye anayeonekana kuja kuweza kumudu kuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama hicho. Ukimlinganisha na wagombea wengine (hasa Lowassa aliyejiuzulu kwa kashfa) ni Membe tu ambaye anaonekana kulindwa na mlolongo mkubwa wa kashfa mbalimbali na japo - kama nilivyosema wiki kadhaa nyuma - hajajiandaa kuwa Rais ni wazi miaka hii miwili iliyobakia inaweza kumsaidia kujitengenezea na kuwa a true "presidential candidate"

CCM ikimsimamisha Membe kama mgombea wake inaweza kuwa na nafasi ya kushinda tena kiti cha Urais; wakimsimamisha mtu mwingine yeyote itakuwa ni mwisho wa utawala wa CCM.

Ni kweli?
MZEE MWANAKIJIJI, umeamua ku swing kivyako siku mbili hizi, umepima malaria? huyu ni bora tukamchukue HEADBOY wa BENJAMINI MKAPA atatufaa kuliko pendekezo lako. kwanini uhangaike kuwawazia hao walioko ccm wakati jamii ya watanzania wame wachoka? huoni walivyo taka kutuingiza kwenye vita vya kidini? huoni walivyo iyumbisha serikali mpaka watu hawajui wafanye nini? huoni wanavyo baguana wao kwa wao? huoni wanavyo halalisha rushwa mpaka PCCB hawajui wasimamie nini maana walio iasisi ndio watoaji na wapokeaji wakubwa wa rushwa.huko hakuna msafi, wamebaki wanao penda ngumi mkononi, udini, visasi, ubaguzi na kila baya ulijualo.
 
kutumika kumbe hakutaisha?? hii ya leo kutoka kwa MM ni kali. USIANGALIE HUKO, CHAGUO LA WENGI LIKO CHADEMA.Hawana papara, wako focused, wanatambua ngano na magugu ni yapi, wanamvuto na nj tegemeo la vijana. achana na hao wazee wa nyumba inayo bomoka haina wa kuirekebisha.
 
Membe ni dhaifu mno kuliko hata JK. Hon. Edward Ngoyai Lowassa ndio mtu pekee ndani ya CCM anayefaa kuwa rais wa Tanzania 2015.
 
Magamba INATOSHA, kwani wanahatimiliki? Si wakubali wakati wa kuwa chama cha upinzani umefika
 
Mzee Mwanakijiji,
Sintopendekeza mtu isipokuwa kwa manufaa ya taifa na japokuwa Membe ni kichwa, muweza ukiachana na habari za Ufisadi wake maana huko CCM hakuna msafi kihivyo. Wayahudi walilaaniwa tena na Mungu mwenyewe lakini bado wanaitawala dunia.

Hivyo pamoja na utetezi wako bado nakuhakikishia kwamba CCM wataweza tu kushindana ikiwa watamsimamisha Asha Rose Migiro na hii itatokana na WANAWAKE kutumia kauli mbiu ya TUKIWEZESHWA TUNAWEZA. Itakuwa sio swala la chama bali wanawake against the rest...Na amini maneno yangu watu hawatatazama tena nyuma wala kutazama uwezo wa AshaRose isipokuwa ni mageuzi ambayo kwao yatawalemaza akili..

Kwa upande wa ushindani na hasa Chadema wanatakiwa kuanza mapema sana kumtafuta na kumwandaa mgombea japo kwa siri lakini nawatahadharisha mapema - KAZI IPO 2015 wajipange mapema na vizuri sana laa sivyo itakuwa aibu maana elimu ya Uraia haijazama vichwani mwa wananchi hivyo SHIDA na MATATIZO yanatangulia Mapenzi yao..

Kaka amini amini nakwambia.

CDM hawawezi kushinda urais 2015. Believe me.
 
Ni ukweli Usiopingika kuwa Mhe. Membe ndo Rais Ajaye Tanzania, ndio atamrithi JK maana historia inamlinda kila awaye Waziri Mambo ya Nje ndo Rais Ajaye toka 1995
 
Afadhari ungesema Wasila au Anah kilango ningeshawishika. Kama hao haiwezekani basi ujue hakuna tena chichiemu zaidi ya danchi:bange:
 
Ni kweli anaweza akawa rais. Wizara ya Mambo ya nje inafaa mtu ombaomba anayeweza akaomba neti kwa ekari laki 6 za ardhi yenye madini na gesi. Tukijaribu kumpa Membe urais basi tutakamilisha zoezi la kuuza ardhi yote ya watanzania na sisi tutakua wapangaji wakulipa kodi ya ardhi kwa wazungu. Membe na JK bora JK mara 10 aendelee kuwa rais mpaka 2025! Membe ni wakala wa wazungu na waarabu. Tatizo la watanzania tunapenda sn misaada ya shanga. Ukiwa na rais anayeamini kwamba misaada ni misaada hata kama itatoka kwa shetani tutaipokea ,huyo hafai ni janga kubwa ! Lazima tuwe na rais mwenye uwezo wa kuwatumia wawekezaji wa ndani zaidi . Anayeweza akawaunganisha wafanyabiashara wa ndani wakasukuma maendeleo ya nji! Mkapa katika safu yake ya majembe ya kuchimbua visiki na kujenga uchumi imara hakumchagua Membe kuwa hata naibu waziri. Mimi mwaka 200 akati Membe anagombea ubunge jimboni kwake nilikuwepo, ni mtoa rushwa mzuri sana. Alipata kwa sababu ya utajiri alokua nao tofauti na wagombea wa vyama vingine! Ni bingwa wa kununua wapinzani wake! Kwa kifupi tuache kumtaja Membe kwny nafasi kubwa kama hiyo kwa sababu tu ya sifa yake ya kuwathamini wazungu na misaada ya shetani! Ufisadi unaotajwa hawezi kukwepa hasa wa Richmond na Buzwagi ambao waziri wa Mambo ya nje anahusika kuliko waziri mkuu. Hivi hamjagundua kuwa rais anayekuwa madarakani siku zote anataka amweke mtu dhaifu ili anapokua pembeni amkontro kwa urahisi! Membe ni mzungu mweusi hana hata chembe ya kufanya kazi Vijjini. Tutafute sasa mwekezaji mzungu kamili ili awekeze pale magogoni kuliko huyo mzungu mweusi kwn mawaziri watashndna kutafuta misaada ya vyandarua.
 
Any research and evidence? Kampeni nyingine ni za kipuuzi. Hivi mnatumwa au kujipendekeza ili wawatumie? Statement yako ni urongo na umbea from the outset mwanangu. Je hii inatokana na ujinga ulimbukeni ua kukosa muda wa kufanya utafiti na busara? Kama utaengemea kuwa Mkapa na Kikwete waliwahi kuwa mawaziri wa mambo ya nje unakosea. Maana Kambarage, Mwinyi hawajawahi kuwa mawaziri wa mambo ya nje. Try to come with something sensible and conceivable instead of ballyhoos made by yahoos.
 
Kama ni hivyo watanzania wengi watakuwa hawajui wanahitaji Tanzania ya aina gani kwa kutokujua aina ya kiongozi wa kutuongoza.Tunahitaji Tanzania yenye amani,isiyokuwa na rushwa,yenye utawala wa sheria,uchumi unaokuwa,yenye ajira,isiyokuwa na ufisadi,yenye siasa safi,yenye uongozi safi.yenye vipao mbele.isiyokuwa na udini udini,yenye kuwekawananchi wake mbele.tutahitaji Tanzania yenye maendeleo ya kweli.
 
Ni ukweli Usiopingika kuwa Mhe. Membe ndo Rais Ajaye Tanzania, ndio atamrithi JK maana historia inamlinda kila awaye Waziri Mambo ya Nje ndo Rais Ajaye toka 1995

nachukia vilaza JF. Yaani wewe unaongzwa na historia kujua nani rais ajeye wa tanzania badala ya kuangalia uwezo wa mtu ukilinganisha na kipindi ambapo huyo mtu atakuwa rais. membe ameshindwa kutatua mgogoro wa ziwa nyasa aje awe rais wa taifa lenye changamoto za ufisadi na udini unaoibuka kwa kasi? umetumwa kupima upepo wewe, nenda kapige mswaki uje upya JF
 
UPEPO TU HUO UNAPITA Hamna jipya hapo, akipewa na basi Sheikh PONDA atakuwa waziri mkuu.
 
CCM Is no more.... Kwisha habari yao... Wadanganyikao na historia tunaweza waita vilaza kwa kushindwa kufikiri.
 
Ni ukweli Usiopingika kuwa Mhe. Membe ndo Rais Ajaye Tanzania, ndio atamrithi JK maana historia inamlinda kila awaye Waziri Mambo ya Nje ndo Rais Ajaye toka 1995

Hivi na wewe, hapo ume_stretch thinking and analysis yako hadi mwisho?..
Kwani toka huo mwaka 1995 hadi leo wamwkuwepo mawaziri wangapi wa Nje?!..Au umezaliwa juzi hapa, hujui unachokiongea?

Halafu ni Membe gani huyu unayemuongelea?..Yule mwenye kusaini mikataba kiholela?...Mkuu yaelekea hujui watanzania wameamkaje kwa sasa!
 
Ukiona mtu mzima ameguna,basi ujue ukuni unaoweka motoni haufai kupika kande!
 
Back
Top Bottom