HOJA: Je, umahiri wa lugha ya kigeni ni kipimo cha akili?

darubin ya mbao

JF-Expert Member
Aug 3, 2016
1,508
2,000
Ni kweli. Kuwa na uwezo wa kumudu lugha za kigeni ambazo hukuzaliwa nazo ni ishara ya uwezo mkubwa wa kiakili.

Sio tu Kiingereza, bali lugha yoyote ile.

Maana yake ubongo wako una uwezo mkubwa wa kuchakata taarifa na mawazo katika lugha tofauti tofauti kwa wakati mmoja na ukaweza kuzungumza bila kubabaika ama kuchanganyikiwa.

Ni ufundi. Ukiwa goigoi wa akili huwezi kuzungumza lugha zaidi ya mbili.

Ndio maana wengine mpaka leo hawawezi kutamka Kiswahili kikaeleweka maana bongo zao zimeelemewa na tope zito la lugha mama.
Waambie waelewe.
 

Mnyatiaji

JF-Expert Member
Dec 13, 2018
2,269
2,000
Twende mbele turudi nyuma jamani kujua lugha ya kigeni ni raha ila kuhusiana na uwezo wa akili hii haikubaliani moja kwa moja ila ina uhusiano flani
 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,406
2,000
Kumekuwa na hoja miongoni mwetu Watanzania kuhusu matumizi ya lugha za kigeni hasa Kiingereza kutumika kama kipimo cha mtu mwenye uwezo mkubwa wa akili. Je, hoja hii ikoje? na ina ukweli kiasi gani?
Kama sio akili kwa nini vipanga wa darasani ndio waliokuwa wanakuwa mahiri pia kwenye somo la Kiingererza?

Sijaona mtu anapata 15% somo la Biology, History au Geograpghy, halafu 95% kwenye English.
 

Mr What

JF-Expert Member
Oct 22, 2016
857
1,000
Inategemea na elimu yako, elimu ya juu Tanzania inafundishwa kwa Kiingereza. Kuanzia A level unaandaliwa kwa insha na mijadala kujenga uwezo wa kutoa hoja.

Shahada pia inajumlisha uwezo wa kuandika na kuongea. Unapopata cheti kinathibitisha ukifundishwa kwa Kiingereza na una uwezo wa kuandika na kuongea kwa ufasaha.
Ndiyo maana kunakuwa na si ntofahamu pale MTU anapofundishwa kwa Kiingereza miaka mingi tu mpaka akapata PHD halafu asijue Kiingereza.....
 

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
5,411
2,000
Mimi Kingereza sijui, lakini kiakili nina uwezo mkubwa sana.
Sasa hiyo ndo hoja niliyoibua hapa mkuu...ukweli ni kwamba kumekuwa na upotoshaji miongoni mwetu kwamba mtu asipofahamu kuzungumza au kuandika vema kiingereza basi eti hana akili kamili. Huu ni 'upopoma' (samahani kwa hilo neno mapopoma) kudhani kwamba kiingereza ndio kipimio cha akili ya mtu.
 

Krav Maga

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
4,626
2,000
Actually, kwa mtanzania kuweza kumudu Kiingereza ni kipimo cha uwezo wa juu wa kiakili.

Ndivyo hivyo hivyo, unapomuona mzungu kama Bongozozo anazungumza Kiswahili fasaha, utambue ana uwezo mkubwa wa kumudu lugha (linguistic intelligence).

Kwa mtu goigoi wa akili sio rahisi kumudu lugha ngeni. Ni ngumu sana tena sana.

Ubongo wako unahitaji kuwa sharp kuweza kuchakata lugha mpya usiyoitambua.

Ni cognitive ability ya hali ya juu ya ubongo katika kuchakata mawazo na kuyawakilisha kwa kutumia lugha tofauti tofauti.
Nikipata sababu ya Kisayansi zaidi juu ya hili naweza Kukuelewa ila kwa sasa na ulichokiandika hapa sijakuelewa japo nina wajibu wa Kuheshimu mtizamo na mchango wako huu pia.
 

Kamukhm

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,652
2,000
Ni kweli. Kuwa na uwezo wa kumudu lugha za kigeni ambazo hukuzaliwa nazo ni ishara ya uwezo mkubwa wa kiakili.

Sio tu Kiingereza, bali lugha yoyote ile.

Maana yake ubongo wako una uwezo mkubwa wa kuchakata taarifa na mawazo katika lugha tofauti tofauti kwa wakati mmoja na ukaweza kuzungumza bila kubabaika ama kuchanganyikiwa.

Ni ufundi. Ukiwa goigoi wa akili huwezi kuzungumza lugha zaidi ya mbili.

Ndio maana wengine mpaka leo hawawezi kutamka Kiswahili kikaeleweka maana bongo zao zimeelemewa na tope zito la lugha mama.
Hivi ukijua kiingereza.. unapokuwa unawaza kimoyo moyo .. huwa unawaza kwa kiingereza!? Au unawaza kwa Kiswahili.. :)??
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom