ZILLAHENDER MPEMA
JF-Expert Member
- Apr 4, 2015
- 2,055
- 4,241
Mwaka 2017 tubadilishe wimbo wa Taifa,badala ya "Mungu ibariki.......", tutumie ule wimbo wa CCM" acha waisome namba eeeee......CCM mbele kwa mbeleeee......."
Atatoka tu hata yeye nihoja hapa tumpiganie pia...Huogopi kuitwa lile jina la yule mheshimiwa analia sikukuu gizani?
Hivi wakina Sioi Sumari walishatoka gerezani?Wasimsumbue tena Max na JF kwa ujumla.
Watuache tu tuendelee mambo yetu na wao wafanye ya kwao.
Mapambano yaendelee dhidi ya wapiga dili mpaka wanyooke,bila kujali kelele za wanafiki !Wakuu nataka mfunguke tukielekea kumaliza mwaka nadhani rais Magufuli atapitia hapa na achukue maoni kwa ajiri ya kuanza mwaka mpya 2017.
Nini kinakuchukiza ndani ya utawala wa rais magufuli ambacho unataka ajirekebishe mwaka 2017?.
Binafisi Mimi swala lililonichanganya mwaka huu ni kitendo cha kubadilisha matumizi ya Rambi rambi ya wahanga wa bukoba hili swala limeniuma sana, likitokea janga jingine naona kama itakuwa ngumu watu kuchangia.
Je kwako ni nini?
Iwe ni mambo anayoyafanya yeye au wateule wake au serikali kwa ujumla hata ikiwezekana huko uliko mtaani au kijijini ongea kwa Uhuru..
Sema mambo usiyapenda yaendelee mwaka mpya 2017 hapa .
NB : Mod naomba mfatilie mjadala na kuondoa threads yeyote itakayoletwa hapa kukiuka na kutoka nje malengo ya tunacho discuss,ili wasilete hapa uchama ni kwa maslahi ya taifa tu.
Lengo langu Rais apitie hapa na kuchukua maoni ya wananchi wanachokitaka kuelekea 2017 maana sasa hivi hata waliopo vijijini tupo nao humu wengi.