Hoja funga mwaka: Ni kitu gani kisifanyike 2017 ndani ya utawala wa Rais Magufuli?

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
9,980
2,000
Wakuu nataka mfunguke tukielekea kumaliza mwaka nadhani rais Magufuli atapitia hapa na achukue maoni kwa ajiri ya kuanza mwaka mpya 2017.

Nini kinakuchukiza ndani ya utawala wa rais magufuli ambacho unataka ajirekebishe mwaka 2017?.

Binafisi Mimi swala lililonichanganya mwaka huu ni kitendo cha kubadilisha matumizi ya Rambi rambi ya wahanga wa bukoba hili swala limeniuma sana, likitokea janga jingine naona kama itakuwa ngumu watu kuchangia.

Je kwako ni nini?

Iwe ni mambo anayoyafanya yeye au wateule wake au serikali kwa ujumla hata ikiwezekana huko uliko mtaani au kijijini ongea kwa Uhuru..

Sema mambo usiyapenda yaendelee mwaka mpya 2017 hapa .

NB: Tuondoe uchama katika mada hii

Lengo langu Rais apitie hapa na kuchukua maoni ya wananchi wanachokitaka kuelekea 2017 maana sasa hivi hata waliopo vijijini tupo nao humu wengi.
 

Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,114
2,000
Mkuu nnaomba uache uchochezi wako kwa Wananchi dhidi ya Serikali yao takatifu inayoongozwa na Malaika..

Wewe hauoni kila inachofanya chapendeza na ni sahihi ?...
 

Mwanzi1

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
5,724
2,000
Kwangu mimi, ningependa viongozi wote wa serikali na sio rais tuu, kuwapa watu muda wa kujirekebisha au muda wa kujipanga kufanya mambo mengine. Nitatoa mfano ili unielewe zaidi. Unapoona mkuu wa mkoa au wilaya anasema "kunazia leo, ni marufuku kupita njia hii" au "ni marifuku kuweka biashara yako hapa" Huyu unaempa hizi amri ni binadamu, ana malengo yake. Ukimzimia kibatali ghafla ni umezima kibatali kwa familia nzima inayo mtegemea.
Kwa hiyo ningependa viongozi wawe na sura ya utu japo natumia sana msemo wa kuwa Sheria Ni Sheria, lakini na utu una nafasi yake katika jamii.
 

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
2,968
2,000
Tutawezaje kuweka mambo tusiyoyapenda yaendelee wakati yeye anapenda yaendelee?

Tutawezaje kumshauri ilihali yeye hataki kusikiliza ushauri badala yake anapenda kusikia yale anayoyapenda kuyasikia.
 

Yohana Kilimba

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
8,116
2,000
Aacha kutughasi humu jf,atwache tutoe stress zetu ili maisha yasonge!
And by the way,sijaona mwenye uwezo wa kupindua serikali yake "kwa maneno au maandishi humu jf"!
Kwahyo a-chill na atawale kwa raha zake!
Atuachie tufanye siasa,awaachie wakina Tundu Lissu na akina Bashe wajimwaye mwaye,wawe huru kufanya mikutano ya kisiasa!
Tumechoka kusikia siasa za upande mmoja!
Yeye,mhe Rais kama kasi haiwezi,basi akae pembeni,siasa atuachie,na yeye abaki na Urais,Uenyekiti wa Chama awaachie wengine ndani ya Chama chake,wenye kuweza mikimiki ya siasa wakiendeshe!
Atoe ajira kwa wote,maana aliaahidi,na kodi tunalipa!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom