Dam55
JF-Expert Member
- Oct 8, 2015
- 5,592
- 11,831
Nasikitika kusema kwamba sera hii sasa inakosa mashiko kabisa kwa hiki kilichotokea leo hii.
Ni ngumu sana kuamini watu wanao pigania Uhuru wa vyombo vya habari kushindwa kuwa wavumilivu na kuviacha vyombo hivyo vifanye kazi kwa Uhuru na utashi wao.
Kama kweli CHADEMA inapigania Uhuru wa Vyombo vya Habari basi wangeacha TBC warushe mkutano wao kwa Uhuru bila ya kushinikizwa kufanya hivyo kwa matakwa ya CHADEMA.
Ifahamike kuwa TBC ni chombo Cha habari Cha Taifa hivyo basi hakiwezi kurusha matamko yoyote yenye viashiria vya kueneza Chuki na uvunjifu wa amani. Ni lazima wafanye uchambuzi wa kipi kinayakiwa kiwafikie watanzania sasa matamko ya viongozi wa CHADEMA hayakuwa mazuri.
Mfano ni Tundu Lissu alikuwa akisema haya.
"Kama wanategemea tutajitoa kwenye Uchaguzi huu, hilo wasahau. Kwenye kila mkutano wetu wa kampeni, wananchi nchi nzima muanze mikutano kwa maandamano ya amani kudai wagombea wetu warudishwe bila masharti yoyote. Watanzania msikubali kukaa kimya tena,"
"Tunaziomba Jumuiya za Kimataifa zituunge mkono katika jambo hili la kupigania wagombea wa vyama vya upinzani ambao wameunguliwa kwasababu za kihuni maana jambo hili ni kinyume pia na sheria za kimataifa.."
Rais Magufuli aliwaambia wasimamizi wa Tume ya uchaguzi, ambao ni wateule wake, “Siwezi kuwalipa mishahara mikubwa na magari mazuri, halafu mkatangaze wapinzani kuwa washindi kwenye uchaguzi.” Haya ni matokeo ya maelekezo hayo!
Sasa Chombo Cha habari Cha Taifa hakiwezi kutangaza kauli za namna hiyo popote pale dunia sio kwa Tanzania tu pekee.
Mhe Mbowe alienda mbali zaidi na kusema kuwa hawana haja ya kunadi Ilani ya uchaguzi badala yake wanatakiwa wananchi wakadai haki, alipoanza kudai kuwauliza watu kuwa wangapi wapo tayari kwenda kudai haki ndipo hapo TBC wakakata matangazo walipo rudi hewani mhe Mbowe akawapa dk 15 waondoke kwenye mkutano wao.
Je huu Uhuru wa vyombo vya habari tunao upogania ni upi hapa ikiwa hawataka kuviacha vyombo vya habari vitangaze kulingana na weledi wao ? Kwanini walitaka TBC watangaze kwa matakwa ya CHADEMA tu?.
Katika hili CHADEMA mnajiharibia wenyewe.
Je hiki walicho kifanya leo CHADEMA hakijawanyima haki watanzania kupata habari? Huu sio ukandamizaji wa vyombo vya habari?