Hoja binafsi kwa Polisi Mikumi na unyanyasaji

Marathon day

JF-Expert Member
Jan 31, 2020
573
893
Nakuja kwenye hoja, nimeona na kusikia kuhusu unyanyasaji na ushamba wa madaraka kwa polisi wa Mikumi wakiongozwa na DTO wao.

Nimefatilia na kupewa habari za pale mikumi, wanakama raia hovyo, kubambikiwa kesi na wengine kukaa / kulala vituona kwa zaidi ya siku 3 bila huduma muhimu kama chakula na maji. DTO wa pale anakamata abiria waliozidi kwenye mabasi hata kama amezidi abiria mmoja, lengo ni zuri lakini usafiri wa usiku ni watabu hakuna raia anaependa kusimama kwenye mabasi wakati analipa nauli halai, nimeshuhudia Abiria wakishuswa mbugani usiku wa manane kusubiri kuvushwa na bodaboda, tusishangae watu kuliwa na simba kwa utashi wa mtu mmoja anaepbambania cheo, nimeshuhudia abiria wakiingizwa kwenye mabuti ya mabasi ili kuvuka mikumi, hiili ni tatizo kwa watu wenyetamaa ya vyeo na sifa.

Muheshimiwa IGP na RPC wa Morogoro hebubtiuondolee huyu msumbufu hapo mikumi, kama shida yake ni cheo akatafutie sehemu nyingine na sio mikumi sehemu hatari kwa anachokifanya, rushwa imezidi pale, pangua pangua watu pale, anazunguka na kagi kake kabovu (CARINA Ti ) ipo siku malori watamtupa mtaroni ndio atajua !!
 
. DTO wa pale anakamata abiria waliozidi kwenye mabasi hata kama amezidi abiria mmoja, lengo ni zuri lakini usafiri wa usiku ni watabu hakuna raia anaependa kusimama kwenye mabasi wakati analipa nauli halai, nimeshuhudia Abiria wakishuswa mbugani usiku
Ningekuwa rais ningempandisha cheo huyo DTO,anajua kuchapa kazi,sheria inakataza kuzidisha abiria haijasema mmoja au kumi,polisi wanatekereza sheria wewe unaleta kelele.

Siwapendi polisi ila kwa hili nawatetea,wapige kazi kweli kweli
 
Abiria wanateseka ndg hatujafikia huko, watu wengi wanadharura nyingi na mabasi ya usiku bado ni machache, hujakutana na adha hii, labda unatiririka na ka IST kako na hujajua taabu na mahangaiko ya kusafiri ukiwa na dharura
 
Ningekuwa rais ningempandisha cheo huyo DTO,anajua kuchapa kazi,sheria inakataza kuzidisha abiria haijasema mmoja au kumi,polisi wanatekereza sheria wewe unaleta kelele.

Siwapendi polisi ila kwa hili nawatetea,wapige kazi kweli kweli
Mimi nawapenda sana polisi wetu ila kwahili siwasaport hasa hizi siku za chrismass na mwaka mpya , fare inahitajika usafiri ni mgumubwandugu
 
Back
Top Bottom