Mkuu huo ndiyo ukweli wenyewe, sounds crazy but kila government funds kama hizi ndiyo moja ya mchango wa wafanyakazi kwenye bajeti zao. Real talk wala sina nia ya kumuudhi mtu.kumbe we kobello una mtindio....huwezi kuwa sawa...
Sheria hii ni ya kinyama na ni ugaidi wa wazi kwa wafanyakazi wa Tanzania.For sure nichanganyikiwa kwanza ndio nina miaka 26 nilikuwa nategemea NSSF yangu inisaidie nirudi shule sasa ndoto zangu zote zimevulugika nafuu kuingia vitani kuliko kuvumilia manyanyaso haya.
Wafanyakazi wajue maana ya Social Security au wasijue is irrelevant. Jambo la muhimu ni kuwa hela hiyo ni michango ya wafanyakazi. Namna gani itawasaidia, wao ndiyo wanaojua, na serikali haina haki yeyote kuifanya hela ya wafanyakazi kuwa mfuko wa kutekelezea miradi ya maendeleo. No way. Nadhani serikalini bado kuna watu ambao wapo kwenye usingizi mnono wa kukosa fikra, wakifanya kazi ya ku-copy mambo machache kutoka mataifa mengine bila ya kujifunza na kutambua mambo hayo yatafanya kazi vipi katika mazingira yao.
Wewe katika nchi yako, watu wenye ajira rasmi hawafikii hata 10% halafu unasema mfanyakazi asipate mafao mpaka afikishe umri wa miaka 60, wewe una akili au tahira? Nchi ambayo mfumko wa bei ni zaidi ya 20% halafu umwambie mfanyakazi aliyeachishwa kazi akiwa na umri 30, halafu eti asubiri kwenda kuchukua mafao yake mpaka baada ya miaka 30, kweli anayefikiria hivyo ana akili au ni kichaa?
Hiyo link sio sahihi. Ni ya watumishi wa serikali ambao kwa hapa Tanzania wapo chini ya GEPF. Kuna tofauti kubwa sana kati ya Pension fund and provident fund. Kwa wenzetu hata watumishi wa serikali hawapeleki michango provident kwa vile mafao ni madogo wanapeleka pension scheme maalum ndio maana ina hizo sheria. Kama hufahamu serikali huwa haipeleki michango kwenye pension scheme licha ya makato ila wanalipa kwa fungu la bajeti wakishajua idadi ya watu wanaostaafu mwaka huo.Nijuavyo mimi huwezi ku retire kazi ukataka kuchukua fedha yako NSSF unapopenda. Kuna mashatri ya Umri wako na miaka ulolitumikia..Kama mfanyakazi haja qualify ktk makundi haya tuseme unaaxcha kazi ukiwa na umri wa miaka 45 na hujalitumikia taifa kwa miaka inayotakiwa - Huwezi kuchukua hata kama ukienda mahakama gani. Muhimu sana tuelewe vifungu vya sheria za NSSF kabla hatujaunga mkono maana unapojaza makaratasi na kujiunga kuna vipengele ambavyo watu wengi sana huwa hawavisomi..
Ebu pitieni site hii muone mfano.. Bofya
Hauwi mzigo kwa yeyote.
Social security funds si kwa ajili yako, ni kwa ajili ya serikali.... Once you have that in your head, utaona haya malalamiko hayana nguvu kimataifa.
Mnajua maana ya Social Security?
Safi sana LHRC, maana mimi nafikiria kuacha kazi kabla hata ya kufukisha hiyo miaka 55 ili nifanye mambo yangu sasa kwanini PPF wasinipe fedha yangu. Mimi nafanye shirika la umma kwa hiyo mfuko wangu ni PPF, ila mifuko yote kwa sasa inasimamiwa na mamlaka ya SSRAKituo cha kutetea haki za binadamu nchini Tanzania kimesema kinaandaa taratibu za kuiburuza serikali mahakamani kwani kumkatalia mwanachama kuchukua hela zake kwa vile hajafikisha miaka 60 ni ukiukwaji wa haki za binadamu.Hii ni kwa sababu hakuna makubaliano yaliyofanyika kati ya mifuko husika na wanachama ili kuleta sheria hii ambayo ni mbaya na haramu hasa kwa wafanyakazi wa sekta binafsi.
HLRC imeomba ushirikano wa wafanyakazi wote kufanikisha azma hii.
Source:Habari BBC Jioni.
My take:
Sheria hii ya NSSF ni kitanzi kwa wafanyakazi kote nchini hasa wa sekta binafsi kutokana na ukweli kwamba makampuni mengi binafsi yamekuwa yakiwaachisha mara kwa mara wafanyakazi wake huku kukiwa hakuna utetezi wowote wa serikali.Ni vigumu sana wafanyakazi kuunga mkono sheria hii kutokana na ukweli kwamba mtu akiacha kazi akiwa na miaka 30 itampasa kusubiri miaka 25 ili apate mafao yake.Huo ni uendawazimu.
unafikiria kwa kutumia masaburi! ninakuwa wa private coz jamii haitahusihwa we mbwiga! ni mimi na familia yangu! kwani kikwete anajua babu yangu anaishi vipi? peleka umajinuni wako baharini!ukiwa 65yrs old, na umeshakula mafao yako unakuwa mzigo kwa private sector au jamii?