Hizi tabia hazivumiliki

Huyo kijana akiendelea hivyo mleaji ndiye atakayepata lawama maana hakumwonesha njia sahihi ya maisha.
why apate lawama yaani hiyo njia sahihi ya maisha hajaonyeshwa na baba yake,wajomba zake na kaka zake na dada zake..eti aje alaumiwe shemeji.! vipi kama asingemuoa huyo dada yake.na hapo ukute huyo shemeji anao ndugu zake kibao hawana njia sahihi ya maisha na wala yeye halaumiwi na hao ndugu zake alafu eti ndio alaumiwe kwa shemeji.! hata kama unao uwezo wa kumpa maisha basi wanyanyue ndugu zako kwanza wanaokuhusu habari za shemeji sio wajibu wako.
 
Fukuza unasubiri nn
 
Yes, naona bora afurumushwe tu na shemeji, au siyo?
 
Anataka aoe hana hata shuka
Hahaha kubabek haya maneno ungemwambia usoni kavu kavu sijui angekuonaje yaan angesepa siku hio hio na ugomvi na mama mkwe usingeisha, usijaribu jikaze ipo siku yake atajipambanua na kujipambania mkuu usimkatie tamaa kiasi hicho, mnunulie walau hata bajaj basi awe anapiga misele kula vichwa 1000 akizichanga hawezi kukosa hela ya kununua shuka kwani shuka si zipo mpaka buku 7,8,9,10 na kuendelea, muonyeshee upendo mpe Channel
 
Kwa hii Kesi wewe ndio Tatizo mkuu
 
Mleta mada unaonekana umetawaliwa sana na upande wa familia ya mkeo,
Simama kama kichwa cha familia,wewe ndiye mwenye mamlaka na hapo kwako,
Weka misingi na kanuni za maisha hapo kwako,atakayeshindwa kufuata hiyo misingi timua hata kama ni mkeo,

Kuna muda,Mwanaume unatakiwa usimame kama Mwanaume.
 
Kama hakuna changamoto ya msosi, mahali pa kulala papo, acha akae tu.

Angekua wa kike ungehofia kukuletea mimba, ila wa kiume atasepa tu mwenyewe.

Weka misingi mkeo aifate, hujamuoq huyo shemeji yako we dili na mkeo. Kumpa msosi na malazi tu ni msaada tosha mambo ya mtaji ni yeye kujiongeza sio jukumu lako hilo.
 
πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ Mkuu mie ngumi siwezi.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Sasa habari za kukuna nazi mwambie mwachiluwi hukooo
Mi kwanza sina kibao cha nazi mkuu ebu kua na staha
 
Jamaa yangu ww sauti hauna kabisa ndani ya nyumba yako.

Yaani mkeo ni mvivu, shemejiyo mvivu..

Mpaka inafika muda unaingia jikoni mwenyewe? Are u serious?

Kwanza shemejiyo anakujaje kwako bila ratiba maalumu? Shemeji anapaswa kuja kusalimia tu, siyo kukaa.

Weka msimamo wa maisha yanavyotakiwa kuwa ndani ya nyumba yako angali mapeema kabla haijawa too late, kama hawawezi WAONDOKE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…