Hizi sio ndoto za kawaida

Mkuu ndoto zangu mara nyingi ni kuota mtu amekufa,mda mwingine kweli siku hiyo nitasikia amekufa,mara nyingi naota naongea na watu waliotutangulia mbele ya haki, mara nakimbizwa na mengine ya ajabu mengi,kwakweli huwa nakosa mpaka amani moyoni kuhusu hizi donto nashindwa kuziepuka!
Mkuu mda mwingine naota kama nafukuzwa lakini mara nyingi huwa natesaka sana siwezi kufumbua macho najikuta nahangaika tu hiyo hupelekea nikiamka asubuhi nipo hoi na tumbo linakuwa linaumwa kama nimevimbiwa flani
Hebu tuwasiliane PM
 
Haya matangazo ya biashara ulishayalipia kwa mods?
Hili sio tangazo la biashara,waka sina ruhusa ya kufanya hivyo...
Wala sifanyi hiyo biashara mi nimesoma nimeona faida zake so nashauri anaetaka
Hata akitaka burebanasaidiwa,kukuonyesha kuwa sio biashara
 
Mshana wanangu wanaota kula siku tena sometimes wanaota wanaongea but also uamka na kusimulia alivyoota.

Nini sàbàbu kama
 
Hebu nitafisirie ndoto hii niliyoiota.
Nimeota nipo na Mh Rais,katika ndoto nilikuwa mtu wake wa karibu. Nilimwona alikuwa na nia njema na Mwenye uchungu na watanzania,lakini Watu wenye nia mbaya walikuwa wakikwamisha jitihada zake,alikuwa anakuwa mnyonge sana,anaumia sana mpaka kuugua. Nilimwonea huruma sana. Alihuzunika sana. Ufitini aliokuwa Mkuu anafanyiwa uliniuma sana.
Niliamka na kushtuka kweli sikuwa na Amani.
Maisha nikayakuta kama kawa yamebana,wadogo zangu wamegraduate hawana ajira,Mke Wangu amepanda vyeo lakini mshahara haibadiliki,tena Toka hii awamu ianze na walishawahi andikiwa barua upya baada ya kuandikiwa upya barua za kupanda vyeo bila sababu na kupoteza madai yao .
Kwa ujumla silikubalini na mambo haya.
Mshana hii ndoto imekaaje? Imeniconfuse!
 
Mmh ukisikia ndoto tata ndio hizi ila ndoto nyingi tafsiri yake huja kinyume... Hivyo hayo yote uliyoota yapindue katika kinyume chake
 
Mshana wanangu wanaota kula siku tena sometimes wanaota wanaongea but also uamka na kusimulia alivyoota.

Nini sàbàbu kama
Nadhani kuna mada yake.. Hebu ngoja niitafute ila pia walambishe ndimu ndoto za kula na kujitafuna zitakoma.. Between ndoto ni sehemu muhimu kwa afya ya akili na makuzi ila ziwe ni ndoto halisi na sio zile zinazotokana na matendo mabovu ya kibinadamu
 
Seriously
Usiku wa Leo nilipitiwa na usingiz nimeota mshana ka hackiwa accnt na wasiojulikana!!
Also nikaota nambinu wanayotumia kupata access
 
View attachment 421080Ni usiku mwingine tena tunapojiandaa kupumzika vitandani mwetu ( hata kama ni ugenini gesti house au barabarani kuna dakika chache utalala kidogo na kuota)
Ndoto njozi na kuota ni hitaji la kawaida la mwanadamu, shida ipo ni je unaona ndoto za aina gani?

-unaota ndoto za kawaida kutokana na harakati za kawaida za kimaisha kutokana na fikra mawazo matendo na maono?

-Ama la unaota ndoto taarifa au ndoto ujumbe au ndoto maono? Ndoto zenye ujumbe maalum?

- Au je unaota zile ndoto zile ambazo si ndoto bali ni matendo ya giza? Ndoto za
Kuota umelazwa kwenye jeneza
Kuota unazama/unazamishwa baharini
Kuota unakula/unalishwa nyama

Kuota unang'atwa na mdudu na unapata maumivu mpaka asubuhi
Kuota unakimbizwa au kufukuzwa
Kuota umefungiwa kwenye kiota chupa nk
Ndoto zote hizi huwa live mpaka asubuhi au unapostuka na unakumbuka kila kitu saa nyingine hata uchovu maumivu na Ladha....!

Ndoto za namna hii si ndoto za kawaida na huambatana na mambo yako mengi kuharibika! Hizi ni ndoto za kufanyiwa mambo mabaya na watu wabaya
Ukiweza jitahidi kuchunguza ndoto zako leo na siku zijazo utagundua kitu View attachment 421088

Ndoto ni bayana! Nakuelewa sana Kiongozi! Mzee wa Spiritual realm!
 
Na mimi mara nyingi sana naota kukimbizwa. KAma wiki 2 hivi nimepota nakimbizwa na watu kibao. Ila katika kuota nikawa najipa matumaini kuwa nimevaa viatu vya kazi na nguo sahihi hivyo nitawashinda kwani sitakuwa na kikwazo kwenye kukimbia
 
Vague memories of our speech, thoughts and actions of past present n future
Sawa...tuongelee future thoughts and actions....kwann uote kitu usichokijua, kukiona au kukiexperience.....? Hapo ndipo ugomvi wangu ulipo. Kuna uhusiano upi kati ya ndoto na vitu Mungu alivyoviumba visivyoonekana?
 
Nafikiri hujanipata vema... Iko hivi kila mtu ana ndoto za kuwa fulani katika maisha, kumiliki vitu fulani, kufikia kiwango fulani cha elimu nk
But mind you future thoughts and actions sio lazima zile lini hata lisaa moja lijalo tayari hiyo ni future
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom