Hizi sio ndoto za kawaida

Hizi sio ndoto za kawaida

View attachment 421080Ni usiku mwingine tena tunapojiandaa kupumzika vitandani mwetu ( hata kama ni ugenini gesti house au barabarani kuna dakika chache utalala kidogo na kuota)
Ndoto njozi na kuota ni hitaji la kawaida la mwanadamu, shida ipo ni je unaona ndoto za aina gani?

-unaota ndoto za kawaida kutokana na harakati za kawaida za kimaisha kutokana na fikra mawazo matendo na maono?

-Ama la unaota ndoto taarifa au ndoto ujumbe au ndoto maono? Ndoto zenye ujumbe maalum?

- Au je unaota zile ndoto zile ambazo si ndoto bali ni matendo ya giza? Ndoto za
Kuota umelazwa kwenye jeneza
Kuota unazama/unazamishwa baharini
Kuota unakula/unalishwa nyama

Kuota unang'atwa na mdudu na unapata maumivu mpaka asubuhi
Kuota unakimbizwa au kufukuzwa
Kuota umefungiwa kwenye kiota chupa nk
Ndoto zote hizi huwa live mpaka asubuhi au unapostuka na unakumbuka kila kitu saa nyingine hata uchovu maumivu na Ladha....!

Ndoto za namna hii si ndoto za kawaida na huambatana na mambo yako mengi kuharibika! Hizi ni ndoto za kufanyiwa mambo mabaya na watu wabaya
Ukiweza jitahidi kuchunguza ndoto zako leo na siku zijazo utagundua kitu View attachment 421088
Habari mkuu, ndoto ni mkusanyiko wa mambo ulokutana nayo siku nzima kabla hujalala labda kwa kutenda, kufikiri, kuona kuona n.k Na hayo sio lazima yawe ya leo tu, inaeza ikawa siku nyingi imepita lakini ukaota leo. Nakuelewa sana mkuu. Upo vizuri. Nisaidie ndoto yangu inamaana gani. Huwa naotaga naanguka kutoka angani. Huwa inajirudia mara kwa mara kwa vipindi tofauti. Inaeza ikapita hata mwaka au miezi kadhaa then inajirudia. Maana ya hii ndoto ni nn hasa...
 
Brother mshana Mimi nimemalza shule hasa kidato cha nne tangu mwaka 2012 ila sasa nmekuwa nikiota ndoto npo shule alafu Naota tumefanya mtihani mfano wakuvuka kidato alafu Mimi inatokea nimefeli kuvuka kidato... dah kwakweli uwainaniumiza sana msaada wako plz.. Bro
Changamoto za maisha.. Kuna mambo unataka kuyafanikisha lakini hayafanikiwi
 
Ngojaaa nimalize hii ndoto
Maana nimeishia pale wamefika gogoni nikashangaa kuona kokoto imepandishwa ndinga kwenda sege
 
Habari mkuu, ndoto ni mkusanyiko wa mambo ulokutana nayo siku nzima kabla hujalala labda kwa kutenda, kufikiri, kuona kuona n.k Na hayo sio lazima yawe ya leo tu, inaeza ikawa siku nyingi imepita lakini ukaota leo. Nakuelewa sana mkuu. Upo vizuri. Nisaidie ndoto yangu inamaana gani. Huwa naotaga naanguka kutoka angani. Huwa inajirudia mara kwa mara kwa vipindi tofauti. Inaeza ikapita hata mwaka au miezi kadhaa then inajirudia. Maana ya hii ndoto ni nn hasa...
Ukiachana na udenda ule wa kutoka mdomoni na ile ndoto ya kuanguka kuna hii hali ya mapambano katika maisha... Kiroho juu ni alama ya mafanikio na chini ni alama ya kushindwa hivyo unapoota unaanguka maana yake kuna mambo yanashindwa kutimia
 
Kuota unafanya mapenzi na mwanamke ambaye humjui wa humuelewi,nini maana ya hii ndoto?
 
Ndoto zishakuwa sehemu ya maisha yangu ya kila siku, hakuna siku nitakayolala niamke bila kuota.
 
Nilitoka kidogo salazar ila nimerejea
Mkuu ndoto zangu mara nyingi ni kuota mtu amekufa,mda mwingine kweli siku hiyo nitasikia amekufa,mara nyingi naota naongea na watu waliotutangulia mbele ya haki, mara nakimbizwa na mengine ya ajabu mengi,kwakweli huwa nakosa mpaka amani moyoni kuhusu hizi donto nashindwa kuziepuka!
 
Baadhi ya ndoto tafsiri yake ni kinyume
Kwa kawaida mwanadamu hutembea kwenda mbele sio kinyume nyume kama kifurukobe
Mkuu mda mwingine naota kama nafukuzwa lakini mara nyingi huwa natesaka sana siwezi kufumbua macho najikuta nahangaika tu hiyo hupelekea nikiamka asubuhi nipo hoi na tumbo linakuwa linaumwa kama nimevimbiwa flani
 
Nipe muda
 
Ukiachana na udenda ule wa kutoka mdomoni na ile ndoto ya kuanguka kuna hii hali ya mapambano katika maisha... Kiroho juu ni alama ya mafanikio na chini ni alama ya kushindwa hivyo unapoota unaanguka maana yake kuna mambo yanashindwa kutimia
Okay...na ugumu unakuja kwenye kuanguka huko sifiki chini. Rafiki yangu mmoja nilishawahi kumtel kuhusiana na ndoto hii akanambia ndoto ya aina hiyo ni mbaya kwa maana ya siku utakayoruhusu kufika chini ujue ndo kifo chako. aaaaghh....ndoto zingine nafirikiri hazipaswi kutimia
 
Ni kweli kabisa siku ukifika chini ndio kwaheri
 
Mshana Jr anajifanya anajua tafsiri ya ndoto. Mwongo.....
Huwezi kujua tafsiri ya ndoto wakati una elimu ya upande mmoja tu.
 
Back
Top Bottom