Hizi shule za English Medium zimetugeuza Wazazi kuwa Walimu?

Wasipo wapa homework, mnazidai kwa nguvu, eti walimu hawafundishi! Kwa hiyo huku uswazi homework ndiyo swali ya mtaani. Wewe, nanirhiu, leo umepewa homework?
 
Masomo kama SOCIAL STUDIES ni magumu kweli kweli. Mtoto darasa la tano anapewa swali la homework utadhani ni A level- "Explain in details the benefits and challenges of Regional integration by siting examples in economic, social and other aspects "!!

Mimi mzazi, I am like...seriously? .

Sijui elimu siku hizi ipoje?
afu ukute ulkua unamwambiaga wewe ndiyo ulkuwa kichwa darasani kwenu 😂 😂
 
Niliwahi kumfanyia dogo homework akaenda akakosa yote
Hebu kila mtu afanye kazi yake wasee mi na stress zangu za pesa na kujipiga na nyundo kwenye vidole badala mwalimu ufanye kaz yako unaniongezea mzigo na mm tena?
 
Acha kabisa mkuu, binafsi pia inaniboa mnoo.
Hapa dogo kaniletea maswali,nmejibu lakini kuna maswali mawili nmechemka.wajuzi wanisaidie please.

1.Farming involving permanent settlement is called...........
2.Farming with no permanent settlement is called.............

Nmemuambia akalale,namtafutia majibu atajaza alfajiri..nmejaribu ku Google lakini wapi
1. Permanent farming
2. Shifting farming

Kama nimekosea wadau watanisahihisha maana mimi mwenyewe elimu yangu ni ya form 4 ya kufeli tena QT
 
Acha kabisa mkuu, binafsi pia inaniboa mnoo.
Hapa dogo kaniletea maswali,nmejibu lakini kuna maswali mawili nmechemka.wajuzi wanisaidie please.

1.Farming involving permanent settlement is called...........
2.Farming with no permanent settlement is called.............

Nmemuambia akalale,namtafutia majibu atajaza alfajiri..nmejaribu ku Google lakini wapi

nilitaka kwenda kinyume na mleta mada ila kwa comment yako hii, Nimehairisha mkuu 😂😂😂
 
Aisee hii ni shida mwanangu maswali ya darasa la pili uafikir form3 du watamuua mwanangu, kweli mtoto wa std 2 una muuliza swali la mention four symptoms of tuberculosis kweli, mpaka nikampigia rafiki yanyu doctor mana mimi nilikua najua 2 tu. Sasa sijui nasoma mimi au mwanangu
Mkuu hii ID yako naionaga kule kwenye group letu la forex au siyo hii?
 
Hakika umesema kweli yani kwa sasa na mm najiona nipo grade 3 A hahaha maana leo uataulizwa what is th process of changing liquid to gas mara draw coat of arm yan kwa kwel inachosha.

Huwa nawaza vipi kwa wale wazazi ambao hawajafika hata form four hawa watoto wanawasidiaje home work
Bado asubuhi hujakumbushwa kusign diary
Yaani inaumiza Sana.
Lengo lao ni kuwaonesha watoto wetu kuwa sisi hatujui!?
Maana akikosa mmekosa wewe na mwanao.!!
Huu ni unyonyaji.
Yaani unalipia ada kubwa aafu uje kuanza kumfundisha mwanao kupanga sentence??
Kwa nini anaenda shule Kama ni hivyo.
Na Mimi nitapata wapi muda wa kuwaza kutafuta pesa ili nilipe hiyo ada!?
 
Watoto kila siku wanarudi na homework mpya mzazi uwasaidie. Ukimuuliza anakuambia mwalimu hajamuelekeza akaelewa.

Sasa nalipia ada zaidi ya milioni ili watoto wapewe homework niwe mwalimu wao?
Kwa nini hawawafundishi wanafunzi wakaelewa ndipo wawape hizo home work wakazifanye!?

Wazazi wengine hatuna hulka ya kufundisha na wengine ndio tuliishia la sababa.

Tunatafuta hela na kulipa ada ili walimu wawafundishe sio watuletee homework kuja kutupima ujinga wetu..!! Walimu fanyeni kazi yenu ya kufundisha msihamishe goli.

Mbona kwenye ada hatupunguziwi kwamba tumeshiriki kufundisha watoto hivyo tulipwe stahiki zetu!?
Ni hulka ya wanafunzi kusema hakuelewa au Mwalimu hakuelezea vizuri.

Wajibu wako kama mzazi sio kushiriki kumfundisha mtoto bali ni kuhakikisha mtoto anafanya kazi zake. Ugonjwa wa kutofanya kazi ni mkubwa.
 
Punguza jazba huwo ni wajibu wako
Wajibu wangu sio kumfundisha vitu ambavyo walimu wake hawajamfundisha.
Wanatakiwa kumfundisha ndipo wampe home work kumpima kama kaelewa.
Sio wampe kazi aje kutafuta majibu ili kesho ndio walimu wamuelekeze.
Sisi tulioishia la 7b tutawaelekeza Nini Hawa watoto.
Mimi naangalia madaftari Kama anafanya kazi na kuandika.
Kama Ana makosa zaidi maana yake haelewi.
Unakagua daftari la mtoto sehemu anayofundishwa ni ndogo kuliko homework unazofanya naye wewe.
Sasa walimu kazi yao Nini!?
 
Back
Top Bottom