Hizi shule za English Medium zimetugeuza Wazazi kuwa Walimu?

Kusema kweli mimi home work sion shida kuwasaidia ila mtihani unakua pale mwanangu wa kwanza wa kike na yuko std5 anakuja na maswali ya ejaculation, menstrual cycle, fertilization,sex na anataka umueleze aelewe ilhali yeye mwenyewe hata kukua bado. Hapo napata shida mno mno maana naona aibu sana,najua natakiwa kuongea nae ila sio mtoto wa miaka 11 dah
 
Watoto kila siku wanarudi na homework mpya mzazi uwasaidie. Ukimuuliza anakuambia mwalimu hajamuelekeza akaelewa.

Sasa nalipia ada zaidi ya milioni ili watoto wapewe homework niwe mwalimu wao?
Kwa nini hawawafundishi wanafunzi wakaelewa ndipo wawape hizo home work wakazifanye!?

Wazazi wengine hatuna hulka ya kufundisha na wengine ndio tuliishia la saba.

Tunatafuta hela na kulipa ada ili walimu wawafundishe sio watuletee homework kuja kutupima ujinga wetu..!! Walimu fanyeni kazi yenu ya kufundisha msihamishe goli.

Mbona kwenye ada hatupunguziwi kwamba tumeshiriki kufundisha watoto hivyo tulipwe stahiki zetu!
Pole mkuu, nilipata mtoto mmoja alikua anakuja nimfundishe class 6.
Shida niliyoona watoto wanakariri zaidi ya umahiri(uelewa)
Nilimuuliza 3X4=?
Akajibu 12
Nikamuuliza hiyo 12/4 ngapi hajui.

Kiingereza napo changamoto, inabidi atafsiri kwa kiswahili atafute jibu then alete jibu kwa kiingereza.

Social science nilikuta amejaza kilimo cha miwa ni morogoro na kapata. Nikamuuliza kwanini anafikiri morogoro ndio jibu na isiwe kisarawe, hana jibu.

Conclusion yangu nikaona changamoto tuliyonayo ni watoto kukosa umahiri zaidi ya kukariri kama kasuku na wazazi ndio tunafurahia kuona 75%and above mtoto anapata kwenye mitihani yake
 
Watoto kila siku wanarudi na homework mpya mzazi uwasaidie. Ukimuuliza anakuambia mwalimu hajamuelekeza akaelewa.

Sasa nalipia ada zaidi ya milioni ili watoto wapewe homework niwe mwalimu wao?
Kwa nini hawawafundishi wanafunzi wakaelewa ndipo wawape hizo home work wakazifanye!?

Wazazi wengine hatuna hulka ya kufundisha na wengine ndio tuliishia la saba.

Tunatafuta hela na kulipa ada ili walimu wawafundishe sio watuletee homework kuja kutupima ujinga wetu..!! Walimu fanyeni kazi yenu ya kufundisha msihamishe goli.

Mbona kwenye ada hatupunguziwi kwamba tumeshiriki kufundisha watoto hivyo tulipwe stahiki zetu!
Fikisha maoni yako kwenye vikao vya wazazi au shuleni. Hizi shule zina watu wengi ambao hawajasomea ualimu, kingereza kizuri tuu hakutoshi kufundisha
 
Ni kuna siku nasolve homework ya maswali 60 siku nyingine 80. Nina watoto watatu mmoja Class 6, mwingine class 3 na mwingine KG 2. Huyo wa Class 6 huja na maswali 40 na Class 3 maswali 20 kwani wanaandaliwa kwa Class 7 na clasa 4 zenye mitihani ya taifa. Taabu tupu Baba narudishwa class kwa ulazima.
Yaani wanakaririshwa wafaulu
 
Back
Top Bottom