Hizi shule za English Medium zimetugeuza Wazazi kuwa Walimu?

Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,507
2,000
Watoto kila siku wanarudi na homework mpya mzazi uwasaidie. Ukimuuliza anakuambia mwalimu hajamuelekeza akaelewa.

Sasa nalipia ada zaidi ya milioni ili watoto wapewe homework niwe mwalimu wao?
Kwa nini hawawafundishi wanafunzi wakaelewa ndipo wawape hizo home work wakazifanye!?

Wazazi wengine hatuna hulka ya kufundisha na wengine ndio tuliishia la sababa.

Tunatafuta hela na kulipa ada ili walimu wawafundishe sio watuletee homework kuja kutupima ujinga wetu..!! Walimu fanyeni kazi yenu ya kufundisha msihamishe goli.

Mbona kwenye ada hatupunguziwi kwamba tumeshiriki kufundisha watoto hivyo tulipwe stahiki zetu!
 
BILGERT

JF-Expert Member
Feb 27, 2015
4,893
2,000
Acha kabisa mkuu, binafsi pia inaniboa mnoo. Hapa dogo kaniletea maswali,nmejibu lakini kuna maswali mawili nmechemka.wajuzi wanisaidie please.

1.Farming involving permanent settlement is called...........
2.Farming with no permanent settlement is called.............

Nmemuambia akalale,namtafutia majibu atajaza alfajiri..nmejaribu ku Google lakini wapi
 
Mnyatiaji

JF-Expert Member
Dec 13, 2018
2,948
2,000
Acha kabisa mkuu, binafsi pia inaniboa mnoo.
Hapa dogo kaniletea maswali,nmejibu lakini kuna maswali mawili nmechemka.wajuzi wanisaidie please.

1.Farming involving permanent settlement is called...........
2.Farming with no permanent settlement is called.............

Nmemuambia akalale,namtafutia majibu atajaza alfajiri..nmejaribu ku Google lakini wapi
Na apo bado ajaleta homework ya kifaransa 😂 😂
 
baby zu

JF-Expert Member
Nov 9, 2015
573
1,000
Hakika umesema kweli yani kwa sasa na mm najiona nipo grade 3 A hahaha maana leo uataulizwa what is th process of changing liquid to gas mara draw coat of arm yan kwa kwel inachosha.

Huwa nawaza vipi kwa wale wazazi ambao hawajafika hata form four hawa watoto wanawasidiaje home work
Bado asubuhi hujakumbushwa kusign diary
 
Mother Confessor

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
18,531
2,000
Acha kabisa mkuu, binafsi pia inaniboa mnoo.
Hapa dogo kaniletea maswali,nmejibu lakini kuna maswali mawili nmechemka.wajuzi wanisaidie please.

1.Farming involving permanent settlement is called...........
2.Farming with no permanent settlement is called.............

Nmemuambia akalale,namtafutia majibu atajaza alfajiri..nmejaribu ku Google lakini wapi
Acha utani bhanaa,..😁😁
 
Said Cosmetics

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
1,603

1.permanent farming
2.normadic farming
 
Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
8,813
2,000
Watoto kila siku wanarudi na homework mpya mzazi uwasaidie. Ukimuuliza anakuambia mwalimu hajamuelekeza akaelewa.
Sasa nalipia ada zaidi ya milioni ili watoto wapewe homework niwe mwalimu wao?
Kwa nini hawawafundishi wanafunzi wakaelewa ndipo wawape hizo home work wakazifanye!?
Wazazi wengine hatuna hulka ya kufundisha na wengine ndio tuliishia la sababa.
Tunatafuta hela na kulipa ada ili walimu wawafundishe sio watuletee homework kuja kuja kutupima ujinga wetu..!!
Walimu fanyeni kazi yenu ya kufundisha msihamishe goli.
Mbona kwenye ada hatupunguziwi kwamba tumeshiriki kufundisha watoto hivyo tulipwe stahiki zetu!?

Hayo ya kuwategemea 100% ndio yaliyotufikisha hapa hivi sasa, hata mwanao akikuuliza kitu unashindwa kujibu kwa kuwa hukufunzwa kujishughulisha!
Japo mimi sina taaluma ya kufundisha lakini kwa sasa bila shaka mfumo wa utoaji elimu umebadilika!

Umetoka kwenye content based hivi sasa ni competence based, ambapo mwanafunzi ndiye anayepaswa kuwajibika zaidi! Mwalimu kazi yake ni kumwelekeza mtoto cha kufanya, hivyo kumtengenezea namna ya kufikiri na kutafiti zaidi!

Binafsi mwanangu anapofika nyumbani na homework ninavyoona anavyopambana kutafuta maelezo, nafurahia sana! Japo mara chache nipatapo nafasi namsaidia kidogo ila ameshazoea, na mara nyingi inabidi kitu kiwe kigumu sana ndio aulize!

Na hiyo ni baada ya kukosa majibu aliyoyaelewa maana hapendi kabisa kuandika kitu ambacho hakielewi!

Hivyo tusiwalaumu waalimu wa watoto wetu hivi sasa kwamba wanawabebesha mizigo, badala yake tuulaumu mfumo tuliopitia sisi ambao zaidi ulitufanya tuwe tegemezi pasipo kupata ujuzi wa kutosha!
 
Said Cosmetics

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
1,603
2,000
Hayo ya kuwategemea 100% ndio yaliyotufikisha hapa hivi sasa, hata mwanao akikuuliza kitu unashindwa kujibu kwa kuwa hukufunzwa kujishughulisha!
Japo mimi sina taaluma ya kufundisha lakini kwa sasa bila shaka mfumo wa utoaji elimu umebadilika! Umetoka kwenye content based hivi sasa ni competence based, ambapo mwanafunzi ndiye anayepaswa kuwajibika zaidi! Mwalimu kazi yake ni kumwelekeza mtoto cha kufanya, hivyo kumtengenezea namna ya kufikiri na kutafiti zaidi! Binafsi mwanangu anapofika nyumbani na homework ninavyoona anavyopambana kutafuta maelezo, nafurahia sana! Japo mara chache nipatapo nafasi namsaidia kidogo ila ameshazoea, na mara nyingi inabidi kitu kiwe kigumu sana ndio aulize! Na hiyo ni baada ya kukosa majibu aliyoyaelewa maana hapendi kabisa kuandika kitu ambacho hakielewi!

Hivyo tusiwalaumu waalimu wa watoto wetu hivi sasa kwamba wanawabebesha mizigo, badala yake tuulaumu mfumo tuliopitia sisi ambao zaidi ulitufanya tuwe tegemezi pasipo kupata ujuzi wa kutosha!
Swadakta mkuu mtoto kama wako ni wa kuigwa
 
kiumbempole

JF-Expert Member
Jan 15, 2016
311
500
na apo bado ajaleta homework ya kifaransa
Masomo kama SOCIAL STUDIES ni magumu kweli kweli. Mtoto darasa la tano anapewa swali la homework utadhani ni A level- "Explain in details the benefits and challenges of Regional integration by siting examples in economic, social and other aspects "!!

Mimi mzazi, I am like...seriously? .

Sijui elimu siku hizi ipoje?
 
Tripo9

JF-Expert Member
Sep 9, 2009
4,183
2,000
Acha kabisa mkuu, binafsi pia inaniboa mnoo.
Hapa dogo kaniletea maswali,nmejibu lakini kuna maswali mawili nmechemka.wajuzi wanisaidie please.

1.Farming involving permanent settlement is called...........
2.Farming with no permanent settlement is called.............

Nmemuambia akalale,namtafutia majibu atajaza alfajiri..nmejaribu ku Google lakini wapi
Mi nimempiga mkwara akija na homework zake aje na text book ya Hilo somo coz majibu lazima yawemo umo. Maana anakawaida ya kuacha vitabu shule. Sitakangi ujinga.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom