Hizi shule za English Medium zimetugeuza Wazazi kuwa Walimu?

Primary255

Member
Mar 23, 2021
16
45
Hii mishule imefikia hatua watoto wanamwambia mama wewe hujui kila ukitupa majibu tunakosa, wanamwambia mama yao si umesoma hadi form 4 wewe sasa tatizo nini, mi nipo ndani nawasikiliza nacheka tuu

Tulipo ambiwa elimu sio lazima uajiliwe tuliahangaa sana.sasa ona madhala yake.
 

Masanja

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
4,430
2,000
Masomo kama SOCIAL STUDIES ni magumu kweli kweli. Mtoto darasa la tano anapewa swali la homework utadhani ni A level- "Explain in details the benefits and challenges of Regional integration by siting examples in economic, social and other aspects "!!

Mimi mzazi, I am like...seriously? .

Sijui elimu siku hizi ipoje?

Wacha vijana wasome..hatutaki kuzalisha akina SABAYA wengine...hahahahahahah
 

Mlandula Jr

JF-Expert Member
Jan 3, 2016
1,754
2,000
Watoto kila siku wanarudi na homework mpya mzazi uwasaidie. Ukimuuliza anakuambia mwalimu hajamuelekeza akaelewa.

Sasa nalipia ada zaidi ya milioni ili watoto wapewe homework niwe mwalimu wao?
Kwa nini hawawafundishi wanafunzi wakaelewa ndipo wawape hizo home work wakazifanye!?

Wazazi wengine hatuna hulka ya kufundisha na wengine ndio tuliishia la sababa.

Tunatafuta hela na kulipa ada ili walimu wawafundishe sio watuletee homework kuja kutupima ujinga wetu..!! Walimu fanyeni kazi yenu ya kufundisha msihamishe goli.

Mbona kwenye ada hatupunguziwi kwamba tumeshiriki kufundisha watoto hivyo tulipwe stahiki zetu!
Kwakweli mkuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom