Hizi shule binafsi dawa yao ni moja tu kulipa madeni yao halafu kuhamisha mtoto kwenda shule ya umma hata kwa mwaka mmoja tu

Tatizo kubwa siyo ada. Ni gharama za chakula na usafiri kubaki kama zilivyo licha ya kwamba siku za kusoma zimepungua. Naona serikali imeshatoa mwongozo wa gharama za chakula na usafiri. Tuishukuru kwa kuliona hilo!
Garama za usafiri na chakula Hakuna shule iliyokuwa inaziitaji huo ni uongo hakuna shule ambayo ilikuwa inahitaji hizo hela Sema mnatafuta kichaka cha kujificha watu wanauliza swala la Ada sio chakula, kwa hiyo wewe unaweza kufikiri kuwa kuna mtu angekuomba hela Ya chakula? Basi huyo alipaswa akapelekwe milembe
 
Nadhani cha muhimu ni kuangalia shule nyingine yenye ubora na unafuu pia isiyo na vibweka hivyo basi muhamishie mtoto huko. Kumrudisha kayumba kwa muda ni kumfrustrate mtoto.
Kwanza haiwezekani kabisa kurudi public school baada ya kuhamia private
 
Garama za usafiri na chakula Hakuna shule iliyokuwa inaziitaji huo ni uongo hakuna shule ambayo ilikuwa inahitaji hizo hela Sema mnatafuta kichaka cha kujificha watu wanauliza swala la Ada sio chakula, kwa hiyo wewe unaweza kufikiri kuwa kuna mtu angekuomba hela Ya chakula? Basi huyo alipaswa akapelekwe milembe

Hujanielewa. kwenye hizi shule hizi mara nyingi kuna malipo ya aina mbili i.e ada na usafiri. Ndani ya ada kuna gharama za chakula. Ina maana wakiziondoa(kwa zile siku zinazopungua) ada itashuka na hiki ndicho kinachotakiwa kufanywa. Pia gharama za usafiri zipungue maana siku za kusoma zimepungua.
 
Kwanza haiwezekani kabisa kurudi public school baada ya kuhamia private
Sio kweli, uhamisho unawezekana kwa shule za msingi, ila sekondari hawaruhusu. Mwaka 2016 baada ya Magu kuingia madarakani watoto wengi ninaowafahamu , waliokuwa English medium walihamishiwa public schools. Siku hizi utaratibu wa uhamisho ni mmoja kwa shule zote , iwe anatoka private to private au private to public .Unaanza kujaziwa form shule anayotoka, then unaenda kata, halafu wilayani. Kama anahamia wilaya nyingine unamalizia mkoani .
 
Hili la kuongeza masaa ya kusoma sikubaliani nalo hata kidogo.. Watoto wengi hawana stamina ya ku concentrate kwa muda mrefu ( mie ndio mbovu kabisa... Sina uwezo wa kuconcentrate hata kwa masaa mawili).
Kuwaweka darasani kwa muda mrefu kwaweza kuwasababishia matatizo ya kisaikolojia kama vile ADD kwa kirefu Attention Deficit Disorder.
 
Tuanze mwaka huu kuwapeleka watoto wetu waliochaguliwa form five kwenye public schools.
Juzi naona mzazi mwanae amepangiwa public schools lakini bado anataka kumpeleka mwanaye kwenye private ambayo hata uwezo wake ni chini ya ile aliyopangiwa na serikali.wazazi wengi tunakumbwa na upepo wa sifa na kutoelewa.

kwa hali ilivyo sasa na uwekezaji wa serikali kwenye shule za kidato cha tano.ni mjinga pekee na mpenda sifa ndiyo ataendelea kushobokea hizo private. kwa sasa private zibaki kwa primary schools tuu baadhi kwa o-level.Lkn high leveltupeleke watoto wetu gov.halafu tuendelee kuomba Jafo apate ubunge na aendelee na Tamisemi.Pia Ndalichako aendelee na ubunge na uwaziri wa Elimu
 
Sasa una maana Walimu wasiendelee pale walipoishia kwa kuwa hawajalipwa. Na kwa sasa waendelee na walipotakiwa kuwepo.
Then Hilo gep mtoto atacover vipi?

Yaan kama alifundishwa kuhesabu Mpka 4 the aendelee na 8 hizo 5,6 na 7 katiasifundishwe?

By the way hakuna anayesurutishwa kumpeleka mtoto kusoma poppte. Ni mfuko wako tu
 
Tatizo lenu wazazi mnaishi kwa kuridhisha jamii. Uwezo wako mtu ni mdogo; nyumba umepanga, ila unalazimisha kumpeleka mwanao shule za milioni na kuacha shule za bure, ili majirani wakuone unapenda wanao.

Kama kweli unampenda mwanao, tumia pesa yako vizuri maana elimu ya bure ipo na watu wanafaulu na kufikia malengo yao.

Ni bora umsomeshe mwanao shule ya bure na kumlipia tution kwa walimu wake ili wamsimamie vizuri. Hizo milioni unazomlipia Tusiime mjengee vyumba vya kupanga, nina imani mwanao akiwa mkubwa atakuja kukushukuru.

Kuliko kumlipia mamilioni huku hujamwachia asset yeyote.

Maana elimu ya Tanzania hailipi sana ukubwani kiasi cha kuiwekezea mamilioni. Huku wewe maisha unaunga unga
Nakuunga mkono asilia mia. Watanzania tunashindwa hata kuiona kesho yetu, watu wamehitimu vyuo vikuu na vyeti vyao mtaani wanakomaa na bodaboda hamna ajira lkn bado wapo wanaojitutumua kulipa mamilioni ya shida ili tu na yeye jamii imuone na mwanaye yuko shule za kishua. Sikatai watoto wasome hizo shule km upo na uwezo lkn ukijiona uchumi wako sio mzure tafuta shule ya bei nafuu mpeleke mtoto ila focus hatima ya mwanao baada ya kuhitimu masomo hasahasa ishu ya kujiajiri mwanao atakuja kukushukuru sn
 
Tatizo lenu wazazi mnaishi kwa kuridhisha jamii. Uwezo wako mtu ni mdogo; nyumba umepanga, ila unalazimisha kumpeleka mwanao shule za milioni na kuacha shule za bure, ili majirani wakuone unapenda wanao.

Kama kweli unampenda mwanao, tumia pesa yako vizuri maana elimu ya bure ipo na watu wanafaulu na kufikia malengo yao.

Ni bora umsomeshe mwanao shule ya bure na kumlipia tution kwa walimu wake ili wamsimamie vizuri. Hizo milioni unazomlipia Tusiime mjengee vyumba vya kupanga, nina imani mwanao akiwa mkubwa atakuja kukushukuru.

Kuliko kumlipia mamilioni huku hujamwachia asset yeyote.

Maana elimu ya Tanzania hailipi sana ukubwani kiasi cha kuiwekezea mamilioni. Huku wewe maisha unaunga unga
Kuishi maisha ya kufurahisha wengine while unao wafurahisha au kuwarusha hawana mpango na wewe. Wanapambana na hali zao.
 
Tatizo lenu wazazi mnaishi kwa kuridhisha jamii. Uwezo wako mtu ni mdogo; nyumba umepanga, ila unalazimisha kumpeleka mwanao shule za milioni na kuacha shule za bure, ili majirani wakuone unapenda wanao.

Kama kweli unampenda mwanao, tumia pesa yako vizuri maana elimu ya bure ipo na watu wanafaulu na kufikia malengo yao.

Ni bora umsomeshe mwanao shule ya bure na kumlipia tution kwa walimu wake ili wamsimamie vizuri. Hizo milioni unazomlipia Tusiime mjengee vyumba vya kupanga, nina imani mwanao akiwa mkubwa atakuja kukushukuru.

Kuliko kumlipia mamilioni huku hujamwachia asset yeyote.

Maana elimu ya Tanzania hailipi sana ukubwani kiasi cha kuiwekezea mamilioni. Huku wewe maisha unaunga unga
Nani kakudanganya fedha za kusomeshea English medium zinaweza kujenga?
 
Sipendagi kabisa kubishana hoja na wanawake.. sababu najua mnatumia hisia kufanya decisions.. huku wanaume tunatumia akili.. ndio maana kwenye uzi wangu umechagua vya kujibu, huku point za muhimu kama tutions umeziruka.

Kama unaamini kumsomesha mtoto private kuanzia chekechea hadi high school ni urithi mkubwa kuliko kumnunulia assets kama viwana au kujenga nyumba nyingi. Endelea na kuamini hivyo hivyo, time will tell.

Ishi maisha kutokana na kipato chako, kama kinaruhusu kumsomesha IST somesha sio dhambi. Hata kina dewji walisomesha IST na vyuo Marekani, ila bado wakapewa urithi wa kampuni yenye mtaji wa mabilioni.

Ila sio huna kitu, mshahara laki 5. Unalazimisha kusomesha Tusiime, unakopa kila siku, stress za madeni , nyumba umepanga, unalazimisha kusomesha tusiime badala ya kuwekeza, mwanao atakuja kukulaumu siku moja.
Ndugu umevuliwa nguo. Ulitakiwa kuchutama na siyo kuendelea kukimbizana.
 
Mimi ninawajua walimu wa secondary wa shule binafsi wamemaliza Chuo kikuu kile Morogoro muma kile cha waislam wako secondary wanafundisha Lakini ukimsimamisha mbele huyo Mwalimu mwambie aongee kiingereza hata kuadhithia kitu Fulani hata Dk mbili hawez kuongea na akijaribu anaunga maneno had aibu nawajua watatu hawawez kuongea kiingereza ila wanafundisha secondary Ya bure ni majanga Sana
Magufuli alikuwa hivyo hivyo lakini leo ndio mkuu wako wa Nchi. Kiingereza sio lugha yetu
 
Baada ya kufungua thread kinachofuata sasa ni kutufungulia thread ya kuuza assets kwa bei cheee, ili ada ipatikane, kama una kiwanja karibu pm mkuu.
 
Tatizo lenu wazazi mnaishi kwa kuridhisha jamii. Uwezo wako mtu ni mdogo; nyumba umepanga, ila unalazimisha kumpeleka mwanao shule za milioni na kuacha shule za bure, ili majirani wakuone unapenda wanao.

Kama kweli unampenda mwanao, tumia pesa yako vizuri maana elimu ya bure ipo na watu wanafaulu na kufikia malengo yao.

Ni bora umsomeshe mwanao shule ya bure na kumlipia tution kwa walimu wake ili wamsimamie vizuri. Hizo milioni unazomlipia Tusiime mjengee vyumba vya kupanga, nina imani mwanao akiwa mkubwa atakuja kukushukuru.

Kuliko kumlipia mamilioni huku hujamwachia asset yeyote.

Maana elimu ya Tanzania hailipi sana ukubwani kiasi cha kuiwekezea mamilioni. Huku wewe maisha unaunga unga
Bure is more expensive than hiyo milioni mbili au tatu za ada kilaza wangu.Wewe Kama unaona elimu ni ghali jaribu ujinga kwenye shule za bure.o
The only thing naweza kukuhakishia Ni kuwa acha sisi tuendelee kupanga huku tukisomesha watoto wetu mwenye shule nzuri,wewe Jenga nyumba huku umisomesha wanao shule za bure.The only thing naweza kukuhakishia ni kuwa watoto wetu watainunua hiyo nyumba na wanao ndo watageuka wapangaji maisha yao yote.hiyo ndo maana ya bure is expensive my kilaza
 
Badala ya kuongeza masaa ya kusoma, ratiba ya kawaida ifuatwe na hii itafanya miula ambayo ilitakiwa kuisha by Dec, kusogezwa mbele hivyo kumalizika January.. After that kuwe na mapumziko ya wk mbili ili by mid February muhula wa kwanza wa mwaka mwingine wa masomo uanze.
 
JamiiForums806319218.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom