Joyce joyce
JF-Expert Member
- May 23, 2020
- 457
- 1,973
Hawa washule binafsi wanajifanya wajanja na kutaka kudhulumu wazazi kwa kigezo cha kuwa serikali imeongeza muda wa masaaa wa wanafunzi kusoma had saa 11 jioni hivyo kunonesha kama ndio sababu ya kutaka wazazi tulipe ada za muhula ambao watoto wetu hawakusoma, labda wamejotoa ufahamu kuwa hayo masaa yameongezwa kwa kuangalia shule za umma kwani shule zote za private zilikuwa zinafundisha hadi saa 11jioni na zingne had saa kumi na mbili jioni, shule za serikali ndizo zilizokuwa zinaishia saa nane mchana na saa tisa.
Hivyo wanatafuta tu uchochoro wa kututapeli, sasa dawa yao ni moja tu; wazazi kuwalipa hiyo hela ya kitapeli tuwape halafu tunahamishia watoto shule za umma za bure hizi za serikali hata Mwaka mmoja tu halafu kama vipi mtu ukikaa vizuri unamrudisha mtoto shule za private lakini shule nyingine kabisa.
Wamemwaga mboga sisi wazazi tutamwaga ugali ili kama ni kuumia tuumie wote.