SoC02 Tanzania ni nchi moja yenye Serikali mbili

Stories of Change - 2022 Competition

kirelau360

New Member
Aug 29, 2022
1
0
Tanzania ni nchi moja yenye serikali mbili tofauti…!!!Serikali hizi hutofautiana kwa lugha,muongozo na hata wananchi wake ila cha ajabu wote ni Watanzania na Rais wao ni mmoja. Serikali A hutumia lugha ya kiswahili ili kuwasiliana na wananchi wake walakini serikali B hutumia lugha ya kingereza kuwasilianan na wananchi wake.Je ni hadi lini serikali hizi zitavunjwa na kutengeneza serikali moja yenye mafanikio ya kudumu kwa Taifa letu?

Ndani ya serikali A waliopo huku ni wananchi kutoka katika mataifa yenye hali ngumu.Wakati serikali B huundwa na wananchi kutoka mataifa yenye uwezo mkubwa.

Suala la ajabu zaidi kwa serikali hizi ni pale tu linapokuja muda wa kunufahika na huduma za kijamaii kwan wananchi toka Serikali zote hupewa kipaumbele sawa yawezekna wananchi wa serikali B kunufaika zaid ya wananchi wa serikal A kutokana na utofauti wa kodi wanazotozwa wananchi wa serikali hizi mbili.

Elimu katika nchi yangu pendwa sasa hivi elimu imetoka kuwa huduma hadi kuwa biashara.Shule nyingi hufunguliwa bila utaratibu maalumu imechangia kiasi kikubwa kuzorota kwa elimu katika nchi yangu.Elimu ya Tanzania hunipa huzuni kwani ndani ya nchi moja kuna mifumo miwili ya elimu hapa,nazungumzia mfumo wa CAMBRIDGE(International schools) na mfumo wetu wa NECTA maarufu kama St kayumba.

Swali:Kwa nini elimu hii igawanye Tanzania katika makundi mawili?

Mbaya zaidi aliyesoma shule za International schools na yule wa st kayumba wote hushindania mkopo wa elimu ya juu mbaya zaid yule wa kimataifa anaweza akapata na yule wa kitaifa akakosa.Hii hupelekea kuziharibu ndoto za waliowengi haswa wale waliosoma shule za kitaifa maarufu kama St Kayumba.Asilimia kubwa za wanafunzi hawa hukimbilia kozi zenye gharama nafuu kusudi kuweza kuendana na uhalisia wa kipato chao ingali wao target yao ni kusoma kozi ya maono yao.Mfano mzuri mwaanafunzi wa shule za kitaifa anaweza akawa na ndoto ya kusomea kozi za udaktar lakin baada ya kukosa mkopo inamlazimu asomee kozi nyingne ambayo ni tofaut na maono yake.

Swali:Je unadhani huyo mwanafunzi atakuwa bora kwenye hio kozi ambayo si ya maono yake?

Pamoja na misukosuko yote mwanafunzi huyo wa shule za Kayumba akimaliza chuo hukosa ajira na kupelekea kuwa mzigo kwa wazazi wao ambao wamejinyima na kuuza baadhi ya mavuno kusudi mwanae asome ili aje kuwakomboa matokeo yake mtoto anarudi nyumbani na makaratasi ambayo huitwa vyeti.Hii hupelekea kuzikandamiza sana jamii za wakulima kwani hawaoni faida ya kumsomesha mtoto wao kama bado ni tegemeo kwao na mwishowe badala ya elimu kuwa ufunguo wa Maisha unakua kifungo cha Maisha.

Swali:Je,baada ya muda tunatengeneza taifa la watu gani?

Mazingira duni ya kufanyia kazi kwa walimu wetu,asilimia kubwa ya walimu hufanya kazi kwenye mazingira magumu sana achana na umbali mrefu kwenda mashuleni kufundisha hupokea mishahara duni ukilinganisha na watumishi wengine wa serikali na katika mshahara huo huenda akanufaika kwa asilimia chache kwa sababu ya tozo ambazo anatakiwa kulipa kwa serikali.Pia,katika jamii ya huyo mwalimu wapo baadhi ya wazazi wenye roho za kulipa kisasi mfano,wapo walimu wanaotishiwa maisha kisa kumuadhibu mwanafunzi kwa utomvu wa nidhamu.

Swali:Je kwa hizo changamoto huyo mwalimu atakuwa na ubora kwenye kazi yake?

Adhabu zitolewazo mashuleni baada ya mwanafunzi kufeli zimekuwa ni za kuwafubaza na kuwakomaza wanafunzi kuna muda wanafunzi wanachapwa viboko ambapo hupelekea kuwa na chuki kati ya mwanafunzi na mwalimu wa somo au kupewa adhabu ya kulima kipande cha shamba,mtoto akimaliza shule baada ya kukosa ajira serikali inamshauri ajiajiri kupitia kilimo.

Swali:Je huyo mwanafunzi ataweza kufanya vizuri ingali anachuki binafsi na mwalimu wake,Pia ataweza kujiajiri kupitia kilimo wakati akili yake inamuambia kilimo ni adhabu kwa waliofanya makosa?

Mahusiano hafifu kati ya mzazi na mwalimu hii hupelekea kurudisha nyuma sekta ya elimu hapa nchini.Kuaribikia au kutokuwepo kwa mahusiano hayo hutokana na uelewa mdogo wa wazazi kujua kwamba ni wajibu wao kujua maendeleo ya mtoto,lakini jambo hili kwa nchi yangu limekua ni la walimu hivyo kuwapa wakati mgumu walimu kufuatilia maendeleo ya mwanafunzi pindi anapokuwepo nyumbani.

Swali:Je ni wazazi wangapi hufuatilia mwenendo wa mtoto kitaaluma?

Changamoto ya usafiri kwa wanafunzi wengi haswa wa shule za serikali,unakuta mwanafunzi kaamka saa 11:30 alfajiri anajiandaa kusudi awahi shule,lakini anapofika kituoni kupanda gari kwenda shule,wanafunzi hawa wamekuwa wakibaguliwa matokeo yake mtoto anapoteza muda hapo kituoni na kufika shuleni saa 1:30 asubuhi na saa 2:00 asubuhi vipindi vinatakiwa kuaanza.

Bado muda wa kurudi nyumbani anapitia mateso hayohayo anafika nyumban saa 12 jioni wakati mwingine saa 1 usiku,afikapo nyumbani kama n msichana lazima asaidie kazi za hapo nyumbani matokeo yake mwanafunzi analala saa 3 usiku au saa 4 usiku na hajafanya kazi ya shule pia kujisomea na kesho pia anatakiwa aende shule.Alafu mwishowe wanafunzi wakifeli serikali inashangaa…!!!inashangaa nini wakati matatizo wanayaona na hawayafanyii kazi?

Swali:Je mwanafunzi huyo atakuwa na ufanisi na kuweza kuelewa yale anayofundishwa?

NINI KIFANYIKE KUBORESHA ELIMU YETU YA TANZANIA.

  • Kuipa kipaumbele sekta ya elimu kama moja ya sekta nyeti hapa nchini,kama ilivo kwa baadhi ya sekta nyingine kama sekta ya utalii,sekta ya madini na sekta ya nishati.Hii itasaidia kuongezeka kwa uhitaji wa elimu.Pia,itasaidia kuongeza chachu kwa wanafunzi wa elimu za juu kwa kutaka kuwa bora zaidi ili kuweza kuendana na soko la ajira.
  • Kuboresha mazingira ya elimu;pamoja na serikali kutoa elimu bure lakini bado haijawa kwenye ufanisi mkubwa,zipo baadhi ya shule zina mazingira magumu mf;ukosefu wa madarasa ya kujisomea,madawati,vitabu,nyumba za walimu na walimu wenyewe,pia mishahara ya walimu iongezwe au walimu wapunguziwe kodi kama ilivyo kwa baadhi ya viongozi wetu kama wabunge ili kuwapunguzia gharama za maisha na stress za uchumi hii itawasaidia kuwaongezea ufanisi wa kazi zao.
  • Kupitia sekta ya usafirishaji waandae magari au kuzungumza na uongozi wa makondakta na madereva wa daladala kuwapa kipaumbele wanafunzi haswa muda wa asubuhi na muda wa jioni.Mfano mzuri kwa mkoa wa Dar Es Salaam Serikali kushirikiana na UDA Rapid Transit(UDART) wanaweza kuandaa magari maalumu kwa ajili ya kuwabeba wanafunzi,hii itasaidia kuwapunguzia uchovu kwa wanafunzi wataweza kuwahi kufika shuleni na majumbani kwao kwa wakati sahihi.
  • Kuweka vigezo vyenye kumpa kipaumbele mwanafunzi wa shule za serikali kwenye kupata mkopo wa serikali,kwani vigezo vilivyopo sasa hivi ni kama havina faida kwa aliyesoma shule za kata kwani yeye na aliyesoma shule za private ni sawa mbele ya mkopo wa serikali.
USHAURI WANGU KWA SERIKALI YANGU KUPITIA WIZARA YA ELIMU.
Ni muda sasa kwa serikali yetu kupitia wizara ya elimu kufanya mabadiliko katika mfumo wa elimu wa hapa nchini ili kupunguza wimbi la wasio na ajira mtaani na pia kuongeza idadi ya wanafunzi watakaojiajiri.

  • Kuboresha au kuzibadili sheria zilizopo kwani kutokana na sheria za sasa hivi hazimruhusu mwanafunzi aliehitimu chuo kikuu kupata mkopo kutoka kwenye taasisi za kifedha kama benki na taasisi nyinginezo.Hali hii husababisha wanafunzi hao kukosa sifa za kupata mkopo hivyo kukosa mitaji ambayo ingewasaidia kujiajiri badala ya kutegemea ajira zitokanazo na serikali na taasisi za kiraia hivyo kuongeza idadi ya wasio na ajira huko mitaani.
  • Mwanafunzi ananza elimu ya msingi akiwa na miaka 7,maudhui ya darasa la 1 na la 2 yafundishwe ndani ya mwaka 1,maudhui ya darasa la 3 na la 4 afundishwe mwaka unaofuata,halafu kwa madarasa yaliyobaki kwa maana ya darasa la 5,la 6 na la 7 utumike mwaka mmoja kwa kila darasa kusoma maudhui ya darasa husika.Kwa maana hio mwanafunzi anamaliza elimu ya msingi akiwa na miaka 11.
  • Kwa upande wa elimu ya sekondari,kawaida masomo yanayofundishwa ni 11kuanzia kidato cha 1 hadi cha 2 alafu mwanafunzi huchagua kusoma masomo katika mchepuo wa sayansi,biashara na Sanaa.Je nini kitaharibika kama mwanafunzi huyo ataanzia kusoma katika mchepuo wa ndoto yake yaani kama ni sayansi aanze kuwa na msingi wa sayansi pekee kuanzia kidato cha kwanza mpaka kidato cha 4.Hii itamsaidia kuokoa muda kama angelisoma masomo yote na baadae kwenda kusoma sayansi.
  • Baada ya kumaliza kidato cha 4 kuna muda ambao ni bure kwa wanafunzi yaani asilimia kubwa hupumzika nyumbani wakisubiri matokeo ya kidato cha 4.Je kwa nini serikali isitoe elimu ya ufundi ndani ya muda huo walau kuanzia mwezi wa kwanza hadi mwezi wa nne ili kuwapa ujuzi wanafunzi hao mbali na elimu ya darasani na tena iwe lazima kwa wanafunzi wote waliohitimu kidato cha 4.
  • Kwa upande wa elimu ya kidato cha 5 na cha 6 hakuna shida,suala la kwenda mafunzo ya JKT kwanza yawe ya lazima na kwa asiyekwenda mafunzo hayo asipate sifa za kujiunga na elimu ya chuo kikuu,kupitia mafunzo hayo wafundishwe kilimo na ufugaji pamoja na mafunzo ya awali ya jeshi kama ilivo kawaida,pia muda wa kwenda mafunzo uongezwe toka miezi 3 hadi miezi 4 yaani miezi 2 ya kwanza iwe kwa ajili ya mafunzo ya kilimo na ufugaji miezi miwili iliyobaki iwe kwa ajili ya mafunzo ya awali ya jeshi.
  • Tukimalizia na elimu ya chuo kikuu mwaka wa 1 na wa 2 wanafunzi wa vyuo vikuu wafanye mitihani ya mwisho kama ilivyo kawaida lakini kwa mwaka wa 3 au wa 4 wanafunzi waingie mtaani kufanya utafiti wa changamoto zilizopo mtaani na kueleza kwa namna gani elimu aliyoipata akiwa chuo kikuu kwa miaka 3 itamuwezesha kupambana na changamoto zilizopo kwenye jamii kwa maelezo yaliyoandikwa vizuri.
 
Back
Top Bottom