Hizi shule binafsi dawa yao ni moja tu kulipa madeni yao halafu kuhamisha mtoto kwenda shule ya umma hata kwa mwaka mmoja tu

Kuna watu humu, walikurupushwa Sana ilipotangazwa 29/06/2020
JamiiForums835603031.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa unakataaga nini na unakubali nini?

Kwa nini umsomeshe tuition Wakati yuko shule? Hiyo si itakuharibia ratiba? Huku unalipa tuition kumbe una hela? Pia hizo tuition hazijawahi saidia ni ujanja ujanja tu, na huwa zinaleta madhara watoto kuingia kwenye usherati na madawa Ya kulevya na pia huwa zinamchanganya Mtoto, huku anafundishwa hiki Shuleni nje anafundishwa kingne, ndio maaana baadhi ya shule binafsi Kama St. Francis mbeya Mwanafunzi haruhusiwi kusoma tuition hata Kwa kujificha au St. Marie's Mazinde Juu, acha vikra hizo wewe baba wajibika Kwa watoto acha uzembe wa kukimbilia vya bure, vya bure havina faida
Tuition zina madhara???!!!!!Samahani,una level gani ya elimu au umesoma shule ya aina gani,wewe kama una elimu ya kuunga unga basi utakua mwalimu wa private
 
Kuna njia nyepesi ya kufuta huu mnaoita uhuni, Serikali iboreshe shule zake tu basi hizo Private zitakufa bila kupenda au zitashusha ada.
Upande wa Zanzibar kuna ujenzi unaendelea wa mashule ya kisasa, SMZ ikitumia akili na sio zile siasa za vyama basi ipeleke Walimu bora, vifaa vya kufundishia vya kutosha na motisha kwa hao watumishi mbona vishule private watafugia kuku mbona majengo yao ni bora kuliko shule za Private.
Huku bara Prof Ndalichako ni too manual, yaani tunaweza muita Fiat, nguvu nyingi mwendo mdogo au ubunifu zero, mama bado hajatembea na ndoto za Rais na sijui Kama kuna kitu chochote kile atakuja kukumbukwa zaid ya mkwara kwa wanafunzi waliodai hela zao nakuwaambia wachina ''I will put you inside''
 
Wenye Shule za accademia binafsi wengine ni wajeuri sana na wenye dharau kubwa sana kama yule mama wa ile Shule ya pale maeneo ya mbezi beach!

Kuna clip imetembea akiongea kwa dharau sasa serikali ilivyotoa muongozo sijui atajisikiaje?!
 
Back
Top Bottom