Hizi sheria vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hizi sheria vipi?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Kaitaba, Nov 16, 2009.

 1. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ebu fikilia, jamaa yangu kaibiwa tv yake, mwizi kakamatwa, baada ya kesi kumalizika huyo jamaa kahukumiwa miaka 6 jela, akitoka anunue tv ya huyu jamaa yangu,

  swali ni hili,
  -Kufungwa kwa huyu mwizi, jamaa yangu imemsaidia nini?
  -akitoka jela pesa ya kununua hiyo tv atakuwa nayo?
  -Huyu jamaa yangu akae miaka yote hiyo 6 akisubili kununuliwa tv? ni kwa nini mali za huyu mwizi zisinadiwe na pesa ikipatikana zinunue tv?

  Mimi naona hii sheria haiko sawa,
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Live mapungufu hapo...Ni jambo ambalo katika hali ya kawaida haliko applicable kabisa...Mwambie nduguyo ajinunulie TV sasa hivi, na huyo jamaa akitoka atalipa fedha ya thamani ya tv hiyo kwa wakati huo, hapo ni tukiwa tunasubiri sheria ifanyiwe marekebisho!
   
 3. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ebu angalia na huyu jamaa wa Singida, kaingiliwa ndani kwake na kuibiwa simu ya nokia na pesa sh, 70,000/= kisha mwizi kambaka mkewe mbele yake,

  Huyu mwizi jana kahukumiwa miaka 65 jela, sasa huyu jamaa na mkewe wamesaidiwa nini na sheria hizi mbovu?
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  NIONANAVYO, hapo pana vitu tofauti..kuna sheria za makosa ya jinai na sheria za madai, sheria za jina ni ugomvi kati ya mtuhumiwa na dola na aliyefanyiwa kitendo cha jinai i.e kuibiwa,anakuawa ni mlalamikaji tu i.e, shahidi kwa upande wa dola au jamhuri...katika kesi za madai..ni ugomvi,kwa lugha ya kawaida, kati ya mtu na mtu,yaani mdai na mdaiwa. Kesi za hapo juu ni kesi za jinai...ambazo dola kupitia,mkurugenzi wa mashitaka ndio wanaoziendesha na mahakama hutoa adhabu kwa mujibu wa sheria husika na kosa lenyewe.
  Vipi mlalamikaji anapata haki yake katika jinai.
  Inawezekana mfano katika hukumu kama hiyo hakimu au jaji,baada ya kutoa hukumu ya kifungo,kulingana na kosa linalohitaji hukumu ya kifungo,akamtoza faini mtiwa hatiani au fidia..mfano kesi ya ubakaji...kama ya babu seya...kifungo na fidia...ni uamuzi wa mahakama itakavyoona inafaa kwa mujibu wa kesi na mazingira yake...mara nyingi hutokezea katika kesi za uharibifu na upotevu wa mali kwa hujuma kama wizi.
  Upande wa pili, mlalamikaji anaweza kufungua kesi ya madai...kudai fidia au kurejeshewa mali yake iliyopotezwa na mtuhumiwa katika jinai na kama hukumu imetoka anachofanya ni kuchukuwa kopi ya hukumu na mwenendo wa kesi katika jinai,ambayo haijakatiwa rufani au kuombwa kupitiwa na mahakama ya juu,na kuwa ushahidi wa kutosha kusukuma madai yake ya fidia i.e.,conclusive evidence
  Kadhalika,bado mahakama inatoa nafasi baada ya hukumu kama za hapo juu ya pande husika kukata rufani kama hawajaridhika na kutiwa hatiani kwa mshitakiwa au kuadhibiwa kwake.
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,612
  Trophy Points: 280
  Huyu mwizi jana kahukumiwa miaka 65 jela kwa kuiba simu ya nokia na pesa sh, 70,000/= je kama huyo mwizi aliyeiba Simu ya Nokia kisha akamuuwa mwenye simu angelihukumiwa miaka mingapi? miaka 1000? au 100? kweli bongo kuna haki za kibinadamu.
   
 6. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ndiyo maana waarabu ukimgonga mtu na kumuua kwa mfano, wanatilia mkazo kufanya some sort of condolence payment kwa familia ya wafiwa kuliko kumhukumu dereva, hususan kama ni "accident".

  Tatizo ni kwamba hatuna ile original African justice system, tushaitupa na sasa tunatumia system ya waingereza na West, system ambayo inatilia mkazo zaidi "Law and Order" pamoja na kuhukumu vikali kwa minajili ya ku create a disincentive kwa wengine.Uzoefu umeonyesha hii haifanyi kazi.

  System yetu original Waafrika ilitilia mkazo faini sana, halafu hizi faini alikuwa analipwa aliyekosewa.

  There has got to be a hybrid of the eastern and western justice systems that will prove more practical than each on its own.

  Hii ni PhD thesis kama watu hawajaiandika bado.
   
 7. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Sasa ni ni kifanyike maana zinatugandamiza sana, na hii diyo inayopelekea watu wengi kumalizana nje ya mahakama. wewe fikilia mwanao kabakwa na kuambukizwa ukimwi, mahakama inachofanya ni kumfunga maisha mtuhumiwa, lakini haiangalii huyu aliyeathilika atasaidiwa vipi.

  Nyingine hii inatia hata kichefu chefu, jamaa anamjaza mimba mtoto wa shule, mahakama inachojua ni kumfunga miaka 30, hapo imemaliza haiangalii matunzo ya huyu binti na mtoto atakayezaliwa,

  Mbaya zaidi ni hii, Mzazi anashindwa kumpeleka mtoto shule, mahakama inachofanya ni kumfunga mzazi mwaka mmoja, sasa hapo atakayemuhudumia huyu mtoto na wadogo zake kwa mahitaji ya nyumbani ni nani????!!!!
   
Loading...