Hizi ni siku za mwisho mwisho za IGP Sirro kuendelea kushika wadhifa wake?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,162
Huna sababu ya kuwa mtabiri au kwa jina lingine anaitwa mnajimu, kujua hatma ya yatakayomkuta IGP Sirro Katika siku za karibuni.

Hilo jambo ni dhahiri, aidha atajiuzulu kwa aibu au atafutwa Kazi na mteule wake!

Hatua ya Mheshimiwa Rais kuunda Tume yake huru kwa ajili ya kuchunguza Mauaji ya mfanyibiashara Mussa Hamisi, yanayotokana na kifo kilichotokea cha mtuhumiwa huyo, akiwa ndani ya rumande ya Polisi, ikiwa tayari IGP Sirro alishajiundia Tume yake ya kuchunguza Mauaji hayo hayo ni hatua moja kubwa kwa IGP kung'amua kuwa hatakiwi kuendelea kuhudumu kwenye nafasi hiyo kwa siku zijazo.

Hata hivyo hatua hiyo ya Rais, inatafsiriwa na wachambuzi wa kisiasa, kama kutoiamini Tume iliyoundwa na IGP Sirro ya kuchunguza tukio hilo la Polisi na baadaye kuja kutuletea ripoti yao ya "kimangumashi" ya Mauaji ya mfanyibiashara huyo.

Hatua hiyo peke yake ingemfanya IGP
Sirro ajiuzulu mapema, badala ya kusubiri aibu ya kutenguliwa kwake, baada ya hizo siku 14 walizopewa hiyo Tume huru kuwasilisha mapendekezo yake.

Ninadiriki kumshauri kwa nia njema kabisa, IGP Sirro ajiuzulu sasa hivi, badala ya kusubiri matokeo ya tume hiyo, ambayo yatamtia "kitanzini"

Suala lingine ambalo naliona limefanywa na Rais Samia, ambalo naliona nalo ni la busara Sana, ambako halikufanywa na IGP Sirro ni la kuwasimamisha RPC na RCO wake wa Mkoa wa Mtwara.

Hivi tutaweza vipi kuiamini Tume ya IGP Sirro, ambao tayari wameshaanza kutupiga "fix" eti mmoja wa mapolisi aliyekuwa mahabusu amejinyonga kwa kutumia "dekio" la mahabusu?

Hivi huyu IGP Sirro anataka kutufanya watanzania wote ni malofa na wajinga wa kutupwa?

Hivi kwa mazingira za mahabusu zetu za Polisi tunavyozijua, hivi ni lini mahabusu yoyote nchini imewahi kuwa na "dekio" la kudekia?

Inabidi IGP asome alama za nyakati na atambue wazi kuwa muda wake wa kulitumikia Jeshi hilo umefika kikomo na atambue wazi kuwa ingawa Jeshi lake la Polisi, linaamiinika kuwa ni nguzo muhimu Sana kwa Sisiem kuendelea kukaa madarakani, kwa kutumia "mitutu" yao ya bunduki kufanya wizi wa kura kwa manufaa ya Chama tawala, hivi sasa ajue hata hao wanaSisiem, wameshamchoka na wameona potelea mbali, ngoja aje IGP mwingine "watakayemfundisha" mbinu za wizi wa kura, lakini ni lazima IGP Sirro aondoke, kwa vile anaendelea kuliaibisha Taifa hili kwa vitendo vya kinyama vinavyofanywa na Jeshi lake la Polisi.
 
wafuasi wa Gaidi mboe mnahaha sana.
Halafu hawa wafuasi huwa wananipa shida Sana kuwaelewa.Na hawa ndio wanaofanya iwe ngumu kuitoa CCM.Kwa kuwa ni wanafiki Sana. Kwa Sasa wanapinga ngoma ili SIRO aondoke.Lakin SIRO amekuwa anawalinda CCM.

SIRO ni rafiki wa CCM. Kushangilia ili SIRO aondolewe ,sio kushinda uchaguzi.Ni kushinda 0.00000000000001. Pia kushangilia Ndugai kuondoka sio ushindi wa uchaguzi.Atakuja mwingine wa CCM.Mambo yatakuwa vilevile.Hii ngoma ya kushangilia Ndugai au SIRO kuondoka inawasaidia nn?
 
Halafu hawa wafuasi huwa wananipa shida Sana kuwaelewa.Na hawa ndio wanaofanya iwe ngumu kuitoa CCM.Kwa kuwa ni wanafiki Sana.Kwa Sasa wanapinga ngoma ili SIRO aondoke...
Wafuasi wa CHADEMA tunakuchekesha?

Kwani hujui haya yanayomkuta IGP Sirro ni kutokana na karma?

Hivi utawezaje kumbambikia Kesi ya ugaidi Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini?
 
Hili suala si la wafuasi wa Mbowe, hata hao wafuasi wa kindakindaki wa CCM weshaliona hilo kuwa IGP Sirro "His days are numbered" Full Stop
haahaaa,
mtaishia kupiga ramli.
mnadhani Gaidi lenu litachomoka?
safari hii ataozea hukohuko.
 
Tanpol kama ni kujitia aibu wanajitia wenyewe na hawajaanza leo.

Hebu imagine hapo Mambosasa aliwaamimisha watu hizo ndio footage za CCTV kwenye tukio la kutekwa Mohammed Dewji.

Kwa kiwango cha elimu na tabia za watanzania polisi wataendelea kucheza shere tu.

images (97).jpeg
 
Tanpol kama ni kujitia aibu wanajitia wenyewe na hawajaanza leo.

Hebu imagine hapo Mambosasa aliwaamimisha watu hizo ndio footage za CCTV kwenye tukio la kutekwa Mohammed Dewji.

Kwa kiwango cha elimu na tabia za watanzania polisi wataendelea kucheza shere tu.
View attachment 2109056
Yaani huyo Sirro na Jeshi lake wanatufanya watanzania wote, kuwa hatuna akili na ni wajinga wa kutupwa, kwa kuweza kutudanganya wanavyotaka!
 
Back
Top Bottom