Baada ya kusikiliza hotuba ya J.K nimegundua kwamba hakukuwa na nia ya dhati ya kuandika katiba mpya bali CCM walikuwa wanapima uelewa wa wananchi kuhusu kero za muungano.
Sidhani kama kulikuwa na nia dhabiti ya kupata feedback ya kweli ya kile wanachokitaka watanzania going forward.
Hakukuwa na sababu ya kupoteza muda na pesa kwa misimamo ambayo Rais na CCM walishajua wanachokitaka
Nimesikitishwa sana na udhaifu mkuu wa kiuongozi.Na upotevu wa pesa za kodi kwa decisions ambazo mkuu wa nchi kashaweka upfront.
Kama maoni ya tume hayafai why wasting the time and resources?
After all idea ya katiba mpya haikuwa ajenda ya CCM.
Tanzania nakusikitikia!
Kikwete ni raisi wa hovyo na alipaswa kuzomea.
Kikwete anapewa heshima lakini hajieshimu.
Wapinzani na nyinyi mbadilike!Kwanini jana mlikaa na kumsikiliza mtu anaeongea kama mwenyekiti wa chama?!
Wapinzani mlipaswa ama kumzomea au kutoka nje ya bunge na si kuja kulalamika huku kwenye mitandao.
Wapinzani msiwe "soft" hii itakuwa katiba ya CCM.
Kikwete alistahili kuzomewa kwani hajieshimu na anatumia cheo chake kwa faifa ya CCM.
In short,Kikwete hakustahili kwenda kujadili rasimu ndani ya bunge.
Huyu ni raisi wa hovyo na mnafiki kupindukia asiostahili kuheshimiwa kama raisi.
Jiheshimu uheshimiwe na si vinginevyo.
kinachoshangaza ni hapo anaposema wanaotaka serikali tatu idadi ni ndogo kuliko wanaotaka 2, kajuaje? au kamtumia prof maji marefu maana shek yahaya hayupo.
Leo nimeshuhudia majibu mepesi kwa maswali magumu mno...
Ikiwa matatizo ya muungano bado yapo hata wakati tunasherehekea miaka 50, je si wakati muafaka wa kujaribu serikali 3?
nilijua mapema with CCM hakuna katiba mpya mbali ilikua changa la macho
katiba inatungwa,na utashuhudia ikijadiriwa kifungu kwa kifungu hadi mwisho,then itapigiwa kura,kisha watapelekewa wananchi waikubali ama waikatae,fullstop.
Kwa masikitiko makubwa nikiungana na Watanzania kote nchini na duniani Rais wetu JK umetutia aibu sana hasa kwa hotuba yako iliyojaa maelekezo kwa wabunge wa bunge la katiba wafanye nini na nini wasifanye,lakini ni wazi mbinu zako watu wameshazijua vizuri kuwa huitakii mema Nchii hii hasa uliposema wanaotaka Serikali tatu wangoje kwanza uondoke madarakani.
Hapa kwahili jambo tunatakiwa sana tumshirikishe Mungu ili wale wote wenye nia ovu kama JK washindwe mapema na mchana kweupe tena waziwazi hasa anapotaka Zanzibar iwe nchi ndani ya nchi,yaani kama ilivyo Lesotho ndani ya Afrika Kusini.
Mungu huwa hashindwi jambo maana kamuumba JK nasisi pia .
YEREMIA 32;27
Tazama ,mimi ni Bwana ,Mungu wa wote mwili;je! Kuna neno gumu lolote nisiloliweza?
Mpango huo uliandaliwa mapema,sheria ilitungwa wabunge wote na wawakilishi wawe kwenye bunge idadi yao anaijua na msimamo wa ccm uko wazi ni serikali 2.Pia uteuzi wake miongoni mwa wajumbe 200 makada wa ccm kibao.