Tujipange kununua simu, WhatsApp haitafanya kazi kwenye baadhi ya simu kuanzia Novemba

Mrkingcamel

Member
Jul 27, 2021
16
12
Maelfu ya watu duniani wanatumia mtandao maarufu wa WhatsApp kuwasiliana na ndugu, jamaa na watu wao wa karibu kwa meseji na video lakini watu wengi watashindwa kuitumia huduma hiyo kutokana na mifumo ya simu zao kuanzia mwezi Novemba mwaka huu.

Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa na chapisho la 'The Sun' la nchini Uingereza limeeleza kuwa program ya WhatsApp haitafanya kazi wa baadhi ya simu janja kuanzia Novemba 2021.

Kwa mujibu wa chapisho hilo imeelezwa kuwa program hiyo haitafanya kazi kwa baadhi ya simu za iPhone na Android na watumiaji wa simu hizo wameshauriwa kununua simu mpya au kusasisha simu zao (software updating.)

Imeelezwa kuwa aina 40 za simu janja hazitapata huduma hiyo huku huduma ya kusasisha ( software updating,) kwa watumiaji wa simu hizo utafikia ukomo Novemba mosi mwaka huu.

Ili watumiaji kuweza kutumia huduma hiyo watumiaji wa simu za Android wanatakiwa kutumia Android 4.1 na zaidi na watumiaji wa iPhone kutumia iOs 10 na zaidi.

Simu ambazo zitakosa huduma ya WhatsApp kuanzia Novemba ni pamoja na :

iPhone

iPhone 5

iPhone 6S Plus

iPhone SE

Samsung

Galaxy Trend Lite

Galaxy Trend II

Galaxy SIII

Galaxy S3 Mini

Galaxy Xcover 2

Galaxy Core

Galaxy Ace 2

LG

Lucid 2

Optimus F7

Optimus F5

Optimus L2 II Dual

Optimus L5

Best L5 II

Optimus L5 Dual

Best L3 II

Optimus L7

Optimus L7 II Dual

Best L7 II

Optimus F6, Enact

Optimus L4 II Dual

Optimus F3

Best L4 II

Best L2 II

Optimus Nitro HD

Optimus 4X HD

Optimus F3Q

ZTE

ZTE V956

Grand X Quad V987

Grand Memo

Sony

Xperia Miro

Xperia Neo L

Xperia Arc S

Huawei

Ascend G740

Ascend Mate

Ascend D Quad XL

Ascend D1 Quad XL

Ascend P1 S

Ascend D2

Other smartphones

Alcatel

Archos 53 Platinum

HTC Desire 500

Caterpillar Cat B15

Wiko Cink Five

Wiko Darknight

Lenovo A820

UMi X2

Run Fl1

THL W8
 
Sasa mkuu android 4.1 wakati saiv tunaelekea android 12 kweli kuna hasara hapo? Hivi kuna mtu ana simu ya 2012 humu?
 
Yaaani nijipe moyo kwa huo ujinga uliandika hapo? yani usikute umeandika hapo kwa wivu wa simu ambayo haumiliki, tunaposema uchawi sio kupaa angani
Hahahahaha mimi nimewaletea mjue na si wivu sawa sm ninayo tumia mm adrd t yenyew 5 nilibahatish kenya
 
Back
Top Bottom