Hizi ajali Tanzania nani anawajibika?

Hizi ajali Tanzania nani anawajibika?

rosemarie

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
6,887
Reaction score
3,445
Watanzania wenzangu naomba kuuliza, hizi ajali je kuna mtu yeyote au kiongozi yeyote anayetakiwa kuwajibika?

Kama yupo ni nani? kama hayupo tufanyeje? nimepanda basi la New Force kwenda Mbeya niliomba kushuka Iringa kwa sababu nilishindwa kuvumilia.

Mwendo wa kasi overtake kwenye kona na mlimani dereva hajali, wakati wa kurudi ilibidi tu tutafute ndege maanake tuliona ajali hii hapa.

Kwenda Arusha nako ni hivyo hivyo unapanda Machame Express na Ngorika shida ni hizo hizo, mkifika mahali pa kupumzika mnaambiwa ni dk5 kula na kujisaidia, hizi shida zote za nini?

Hivi hatuna serikali?

Naomba kujua hizi ajali tufanyeje?

Sisi Watanzania mbona tumezubaa sana hatuchukui hatua?

Tutadharauliwa mpaka lini?
 
Kweli ni tatizo maana sasa imefikia hatua mtu ukitaka kusafiri unapata mawazo kwsbb uhakika wa kufika salama siku hz ni mdogo.
Btw,rip wote waliopatwa na ajali huko morogoro.
 
Bibie we acha tu mimi siku hizi nikienda Dar natumia usafiri binafsi ukipanda bus ni mateso mtindo mmoja unapewa dk 10 kula na kujisaidia sasa kama umekaa siti za mwisho utakoma mpaka ushuke tayari dk 6 zimekatika unabakiwa na dk 4 niambie kama si mateso ni nini.

Watanzania wenzangu naomba kuuliza,hizi ajali je kuna mtu yeyote au kiongozi yeyoote anayetakiwa kuwajibika?kama yupo ni nani?kama hayupo tufanyeje???nimepanda basi la New Force kwenda Mbeya niliomba kushuka Iringa kwa sababu nilishindwa kuvumilia,mwendo wa kasi overtake kwenye kona na mlimani dereva hajali,wakati wa kurudi ilibidi tu tutafute ndge manake tuliona ajali hii hapa,kwenda Arusha nako ni hivyo hivyo unapanda Machame Express na Ngorika shida ni hizo hizo,mkifika mahali pa kupumzika mnaambiwa ni dk5 kula na kujisaidia,hizi shida zote za nini???hivi hatuna serikali???naomba kujua hizi ajali tufanyeje???na sisi Watanzania mbona tumezubaa sana hatuchukui hatua???tutadharauliwa mpaka lini????
 
Watanzania wenzangu naomba kuuliza,hizi ajali je kuna mtu yeyote au kiongozi yeyoote anayetakiwa kuwajibika?kama yupo ni nani?kama hayupo tufanyeje???nimepanda basi la New Force kwenda Mbeya niliomba kushuka Iringa kwa sababu nilishindwa kuvumilia,mwendo wa kasi overtake kwenye kona na mlimani dereva hajali,wakati wa kurudi ilibidi tu tutafute ndge manake tuliona ajali hii hapa,kwenda Arusha nako ni hivyo hivyo unapanda Machame Express na Ngorika shida ni hizo hizo,mkifika mahali pa kupumzika mnaambiwa ni dk5 kula na kujisaidia,hizi shida zote za nini???hivi hatuna serikali???naomba kujua hizi ajali tufanyeje???na sisi Watanzania mbona tumezubaa sana hatuchukui hatua???tutadharauliwa mpaka lini????


Kama ingekuwepo sheria isemayo pindi ajali ikitokea na ikaua watu kadhaa viongozi wanaosimamia uchukuzi na usalama barabarani wawajibike, basi ajali hizi zingepungua kwa kiasi kikubwa, lakini sheria zote zinatungwa kuwabana waendeshaji tu huku zikiwaacha viongozi wanaopokea rushwa kwa wamiliki wa mabasi na madereva.

Watanzania hawajazubaa ila ni kwamba tunaburuzwa na mamlaka pamoja na serikali, kwasababu ukifuatilia kwa karibu utagundua kuwa hayo mabasi kwa asilimia kubwa yana mikono ya viongozi wa serikali ambao ni ngumu kuwabana na kuwawajibisha kutokana na either uzembe wao au personal interests zao, kumbuka ilipotokea ajali ya meli kwenye bahari ya Hindi mwaka jana kama sijakosea, wabumge walimtaka Mwakyembe aachie ngazi lakini alijitetea kuwa yeye siye mhusika, kwahiyo nadhani ifike wakati sheria zibadilishwe zisiishie kwa madereva tu zi apply mpaka kwa viongozi pamoja na mamlaka zote ndipo kuheshimiana na kuthaminiana kutakuwepo, ukizingatia kuwa hakuna anayejali kwasababu wao wanasafiri kwa ndege na mashangingi, hawataki kusikia usafiri wa reli kwasababu masilahi yao yataharibiwa.
 
Atakapokufa mtoto wa mmoja wao kwenye haya mabasi ndio watazikumbuka sheria na kuchukua hatua
 
Mh Rais JK, watanzania wamesikia salamu hizi zako kwa karibia MIAKA 10 sasa. Kwa Ajali hizi 2 ZA wiki hii naomba kutosikia salamu zako hizi kwanza, nadhani zinachochea Ajali sababu kila ukizitoa tu INATOKEA nyingine.

Safari HII utanikosha nikisikia, WAZIRI kasimamishwa, mkuu wa usalama barabarani kawajibika, RPC Mkoa wa Morogoro kapigwa chini ......

Vinginevyo Tamka AJALI TANZANIA HAZIEPUKIKI. NA TANZANIA BILA AJALI HAIWEZEKANI.
 
Haya majanga sasa yamezidi....Maamuzi magumu ndio wakati wake ..
 
Kweli kabisa naon Hawapo serious kutoa roho za watu tu
 
Kuna mtu kanitumia hii picha ya ajali nyingine kati ya dar express na simba mtoto muda huu, ila bado hajanipa taarifa kamili imetokea wapi
 

Attachments

  • 1410183497989.jpg
    1410183497989.jpg
    41 KB · Views: 146
Hivi hawa madereva wanawahi wapi jamani jamani Mungu tusaidie jamani
 
Kuna mtu kanitumia hii picha ya ajali nyingine kati ya dar express na simba mtoto muda huu, ila bado hajanipa taarifa kamili imetokea wapi

Fuatilia ulete taarifa acha habari nusunusu
 
Ukichunguza utagundua makampuni ya mabasi either yanamilikwa fully au majority share holders ni viongozi. Na kama tujuavyo viongozi wa TZ ni niguse uone. Hata ajali iue kijiji kizima no one is held accountable.

Atakapokufa mtoto wa mmoja wao kwenye haya mabasi ndio watazikumbuka sheria na kuchukua hatua
 
ivi mmesahau mkapa aliingiaje, ?? Mv bk. Treni dom.

Mkulu ndo anavyomaliza.

,, nchi imeingia mikataba ya kishetani.
 
Watu walishafanya research za kutosha juu ya visababishi vya ajali maeneo tofauti nchini,Zipo tu hakuna wakuzifanyia kazi,ikiwemo kibaha kama case study.Nilipata bahati ya kusoma kwa uchache research moja ilifanywa na mtu wa masters.

kwa maoano yangu hivi ni vitu sugu visababishavyo ajali za mabusi.

a)Mwendo kasi kama Bus linakimbia vita.

b)Abiria kupuuzia madereva wasio na umakini na utu safarini

c)Mabus mabovu kuachiwa barabarani,gear box mbovu gari lipo barabarani kama kawaida.inafikia kila kituo Bus linasimama kufanyiwa service.Na hili limezaa tatizo lingine la Rushwa.

e)Rushwa imekua kama makusanyo ya kawaida kujikimu kwa Trafic.huku kuna kibus kidogo mpaka kisukumwe ndo kinawaka na safari inaanza na kituo cha polisi kipo pembeni tu.

f)Wamiliki wa mabasi kuwawekea Conditions madera wao kua ni lazima wawahi kufika,mabus yake yasije yakakosa wateja kwa kupitwa na kuachwa nyuma na mabusi mengine.Uhasama wa makampuni ya mabusi unawafanya madereva wasiwe na hiari zaidi ya kukimbiza MWENGE,

g)Kuna madereva akili zao ni BENDI MOJA ,zimedata,hawa hawana sifa ya kuwa madereva,wanaviburi na Roho zao washaziweka mfukoni.Sehemu yeyote.I mean YEYOTE wanapita wapendavyo,Kuovertake Kwao ndio kuendesha Basi,hapa linazaliwa tatizo lingine SERIKALI

h)SERIKALI ina sheria nzuri tu Na Vyombo vya kutosha vinavyo deal na Usalama barabari.Inshu ni utendaji kazi wake na Usimamizi wa sheria hizo barabarani.Vyombo hivyo ni dhaifu sana kusimamia utendaji na sheria hizo,Kuna MAGUMASHI ya kufa mtu.

Kwa hayo machache kuna madereva ni wazuri na Wanaelewa kazi zao.

SUNATRA na Polisi kitengo cha trafic wawajibike kwa haya yote
 
Back
Top Bottom