Hizi ajali Tanzania nani anawajibika?

Hizi ajali Tanzania nani anawajibika?

hizo ni fadhila watu wanarudisha kwa miungu yao kafara sio kawaida mwezi 8 na wa 9 ni sheedah kwa ajali
 
Dah hz ajali imekuwa n kitu cha kawaida kbs,ila kama kuna k2 chini ya kapeti bs walala hoi tutamalizika kwa kweli.
 
Hivi punde tumeshuhudia Ndugu zetu tunaowapenda sana wakipoteza maisha wakiwa safarini kwenye harakati za kuangaikia maisha kutokana na uzembe wa madereva wetu na vyombo vyao kuwa vibovu kwa haraka haraka ndani ya miezi miwili yani August na September 2014 kuna ajali kubwa tatu zimetokea ambazo zimehusisha na kugalim maisha si chini ya watu 80 ambao hatuwezi jua uwepo wao ungeifanya nchi hii iwe kwenye level gani kimaendeleo aiza kutokana na maderva kuendesha magari kwa kasi au kutofuata sheria za barabarani na hata wengine kuendesha vyombo vya abiria pasipo kuwa na leseni vinachangia na kugalim maisha yetu, swali JE NINI KIFANYIKE KUPUNGUZA AU KUKOMESHA AJALI ZA BARABARANI????????

Maana sote ni abiria watarajiwa na wengine hivi sasa wanapanga safari wengine wapo safarini wengine ndiyo wanaingia kwenye vyombo vya usafiri ikiwa yote hii ni kutafuta liziki ya maisha huku una uwakika wa kutofika unakokwenda na pengine kuacha wanaokutegemea wapweke na kutojua kesho yao.

MFANO HARISI ANGALIA HII PICHA

MAISHA YETU YAKO MIKONONI MWA HAWA MADEREVA.jpg
 
Superfeo nayo imenyonga wanne leo hii hatari aiseee
 
Hiyo picha inaonesha kutokujali kwa hali ya juu kwa madereva wetu.
 
Simple sana kila mtu kutimiza wajibu wake kuanzia police dereva mmiliki hadi abiria! Mungu ibariki tz Mungu bariki wananchi wake
 
1.Kiundwe chombo huru mfano kama ilivyo TAKUKURU, cha kuchunguza ajari, bila kuingiliwa na police japo wanaweza kuhusishwa katika chombo hicho. mfano. gar kama imetoka mwanza saa 6:00am ikafika Dodoma saa 5 au sita asubuhi tofauti na ratiba ya Sumatra inayo onyesha kwamba bus lazima lifike saa 9 au kumi (mfano) hivyo likifika mapema police walikamate na uenda lisiendelee mbele au lipigwe faini kali ikiwemo na dereva kupelekwa mahakaman hata kama haijatokea ajari, kufika mapema kuna onyesha alikuja kwa mwendo wa hatari sana.

2.Chombo hicho kiwe na mamlaka ya kuchunguza ufuatiliaji wa police traffic kwenye mabasi, ikigundulika gari limepita sehemu mapema na hapo kuna askari na hakuchukua hatua kama hiyo juu, basi chombo kiwe na mamlaka kumfungulia askari mashtaka hata kama ajari haijatokea.

3.Ratiba za Sumatra zibandikwe kwenye gari kila abiria azisome na kujua gari alilo panda litafika moro , au Dodoma au manyoni (mfano) muda gani? na hivyo ikitokea gari imefika mapema, abiria awe na uwezo na ushahidi wa kupiga sim kwa police kiongozi.

4.Ratiba ya Sumatra ikiwekwa kwenye gari, iwekwe na namba za viongozi wa chombo hicho cha kuchunguza ajari na namba na wakurugenzi wa Sumatra. Ikitokea gari imepita sehemu mapema bila police kuchukua hatua, abiria atachukua hatua ya kuwafahamisha viongozi wale.

5. Chombo kiwe na mamlaka ya kukagua ubora wa magari kwa kushirikiana na Jesh la police.

6Itungwe sharia kali, dereva wa basi atakaye sababisha ajari kwa uzembe na kuua watu, basi kesi yake iwe ya mauaji kwa makusudi na kifungo chake kiwe sawa na mtu aliye mkata panga mwenzie kwa makusudi.miaka 30

6.Sheria hiyo, baada ya ajari na mahakama kujiridhika kuwa dereva alifanya uzembe, napendekeza na police traffic waliokuwa zamu barabarani siku husika watiwe hatiani ikiwezekana pia na wao wapewe kifungo.

7.Sheria hiyo imbane hata mmiliki wa gari, baada ya uchunguzi na mahakama kuridhika kwamba dereva hakuwa na leseni inayostahili au pia na gari lililo sababisha ajari lilikuwa na ubovu, mfano matail yamechoka. basi mmiliki wa basi nae ahesabiwe kosa la mauaji kwa kuajiri dereva asiye kuwa na sifa au kwa kutofanya service ya gari yake. Na hivyo adhabu atakayo pewa dereva apewe na bosi wake. wakale wote dona segerea.

YANGU NI HAYO. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Back
Top Bottom