Hiyo Mvua ni ishara ya Machukizo mbele za mungu dhidi ya hawa MAGAMBA

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Sep 2, 2011
4,873
1,216
mvua ni ishara Kuwa Mungu amechukia kuona Serikali ya kibabe ya Magamba,
Mungu amechoshwa nayo kbs na huo ni kama ujumbe kwao,yeye ndo kila kitu,..
Muendelee kuikumbatia Magamba.mungu ataleta mvua ya Moto kbs
 
Msitake kumsingizia mungu mambo ambayo yamefanywa na binadamu.

Kikwete kachaguliwa na binadamu, wanaomuachia aendelee kukalia urais binadamu.

You have control of your own destiny, habari za kumsingizia mungu ni kujiliwaza tu.
 
Hizi mvua hazizuiliki, lakini maafa haya yanazuilika.

Na maafa kama haya yanatokana na kuamini mungu sana. Barabara zinajengwa bila uimara, kwa sababu watu wanaamini mungu atatulinda. Watu wanakaa mabondeni, kwa sababu wanaamini mungu atawalinda. Serikali hainunui vifaa vya kuokoa watu wala kuwaandaa watu kwa majanga, kwa sababu wanaamini mungu atawalinda.

Ukiamini hamna mungu, inabidi uchukue hatua za kujiandaa wewe mwenyewe, hata kama huwezi kuzuia mvua, mvua ikija utakuwa umejiandaa.

Kwa maneno mengine, imani ya kwamba mungu atatulinda ni kichaka tu cha kufichia uvivu wa kufikiri na kujiandaa.
 
Ni wake up call kwa wana Darisalaam ambao wanafanya kosa la msingi la kulala wakati huu wa ukombozi wa nchi toka kwa magamba
 
mvua ni ishara Kuwa Mungu amechukia kuona Serikali ya kibabe ya Magamba,
Mungu amechoshwa nayo kbs na huo ni kama ujumbe kwao,yeye ndo kila kitu,..
Muendelee kuikumbatia Magamba.mungu ataleta mvua ya Moto kbs

Si kweli maana mvua haidwadhuru magamba bali wanyonge magamba yana adhabu yao.
 
Si kweli maana mvua haidwadhuru magamba bali wanyonge magamba yana adhabu yao.
Watu wameshndwa kuwaondoa kwa kupokea hongo za Vyakula,vtenge,kanga,Kofia na pombe,wote wamekosa.
Ishara ya wazi Magamba hamna kitu.
 
usiwe na fikra za kipumpavu ww.watu wanakufa,wanapoteza mali zao na kudhalilika eti unasema Mwenyezi anatuadhibu sbabu ya magamba.uwe na utu na roho za kibinaadamu usiweke siasa ktk kila kitu hata ww yanaweza kukupata zaidi ya haya tuache unafki tuombe maghfira sote tunaweza potea
 
Kuna hoja nyingine tunazitoa as if ni wapiga lamli tukijaribu kumuagulia Mungu. Hivi Mungu humuadhibu mtawala kwa kuwaumiza wananchi wasio na hatia. Recall mfalme wa Babeli, Mungu alimuadhibu yeye individually kwa kumfanya aishi kwa kula majani kama ng'ombe na kunyeshewa mvua. Lakini hakuwaletea mafuriko wananchi kwa adhabu ya mfalme. Kama kweli mvua hizi zatokana na ghadhabu ya Mungu basi ni juu ya wote wakaao katika nchi na si juu ya kiongozi wa nchi.
 
Back
Top Bottom