Simba mbele ya Al alhy ni kama unyoya, labda wabadilike.

Mr Alpha

Senior Member
Jul 31, 2018
195
522
Siku za karibuni Al Ahly wamekuwa na ujasiri mkubwa wakikutana na simba. Sababu kuu ni kwamba wanajua lazima wafanikishe malengo yao mbele ya simba kwakua simba imekosa kabisa mbinu ya kuwadhibiti.

Udhaifu mkubwa walionao simba ni kwenye kufanya marking, Al Ahly wamekuwa wakijipigia simba kirahisi sana magoli mengi ya simba yamekuwa hayadumu sababu ya uzembe, poor marking

Al Ahly ni kama wanapigia hesabu nusu fainali saiv, simba kwao ni kama njia nyeupe hilo wanalijua kabisa na hawana presha rekodi zinawabeba na hata ukiangalia uchezaji wa simba hata saiv bado udhaifu huo wanao

Mbinu pekee ya kuviokoa vilabu vyetu dhidi ya miamba hii ni kucheza kitimu, kushambulia na kuacha ubinafsi. Tabia ya kuharibu nafasi za magoli zitawagharimu mno

Tabia ya uoga na mipango ya kijinga ya kuogopa mpinzani ugenini au nyumbani itawarudisha muendelee na majungu yenu kwenye ligi

Hatua hii inahitaji soka serious nyumbani na ugenini hakuna kukubali kumpa adui nafas ya kufanikiwa popote iwe mvua au jua, ukiruhusu adui apige pasi na kupress unastukizwa unapigwa magoli ya reja reja na wachezaji kuishia kulaumiana, lazima kuwe na mipango mikali kumzuia adui kutengeneza mashambulizi, kaben kwa kasi mkiwa hamna mpira na shambulien kwa umoja mkipata mpira mtakuja kunishukuru.
 
images (1)-1.jpeg
 
Back
Top Bottom