Malimi Jr
JF-Expert Member
- May 28, 2017
- 1,291
- 2,759
Mkuu historia uliyoitoa hapa haitakiwi kufundishwa hapa nchini hata duniani kote.Wazungu walishafuta hayo mnayoyaita Makabila, ni lazima uelewe Kabila ni neno la dharau na maana yake ni mtu ambaye hajatastaarabika bado, yaani hajaweza kujenga Taifa, na ndiyo maana neno Kabila hutumika Afrika Kusini kwa Sahara, native Americans, aborigines hao ndiyo Wazungu hutumia neno Kabila lkn wengine wote walishafuta!
Isitoshe Tanzania haina Makabila 120 kama mnavyoanini na hayo yote unayoyaita Makabila Tanzania yalianzishwa na Wazungu/ Waarabu kabla ya Wageni kuja kwa mfano kulikuwa hakuna Wanyamwezi, Wahaya, Wagogo, Wachaga n.k. kama tuwajuavyo leo hii!
Hivyo neno Kabila ni neno la dharau kwa Mwafrika kama vile nigger tu!
Tuanze na neno USTAARABU(KUSTAARABIKA). Enzi za ukoloni mataifa ambayo yalitawaliwa na Wafaransa yalilazishwa kutumia lugha ya kifaransa kama lugha ya taifa na wale waliofuzu kuongea kifaransa walipewa kazi na waliitwa wastaarabu(kuongea kifaransa tu tauari wewe ni mstaarabu) Je, ustaarabu ni nini?
Ukisema wazungu/waarabu ndio walioleta ukabila/makabila huku afrika. Je, wazungu/waarabu ndo walikuwa wanafundisha kiyoruba, kikuyu, kizaramo, kizulu, n.k??
Unaposema Tanzania hakuna makabila yaani hakuna wamatumbi, wakurya, wahadzabe, wahaya, wanyamwezi, n.k. Je, ustaarabu ni kukataa kila kitu hata kile kile kinachoonekana shahili dhahiri??
Pia, nimeshangaa kuona unatukuza wazungu/waarabu kama wa watu waliostaarabika halafu hapo ukasema ndio walioleta ukabila mwishoni tena unadai ukitaja kabila kwa wazungu /waarabu ni dharau sana. Je, hao wazungu walitumia njia gani kuenenza ukabila ikiwa wao ni wastaarabu??