Hivi watanzania mnataka siasa za aina gani?

Kazanazo

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2023
Posts
5,557
Reaction score
8,195
Hili swali linapaswa kujibiwa na watanzania wote, hivi mnataka siasa za aina gani?

Mnataka siasa za kistaarabu zisizo na unafiki na ukali hasa kutoka viongozi wa juu

Au mnataka siasa za misifa na ukali ukali wa kutumbuana kwenye kadamnasi bila kufuata itifaki?

Hii inahusu zaidi chama kilichopo madarakani mnataka kiwe na siasa za namna gani mnazozipenda?
 
Hili swali linapaswa kujibiwa na watanzania wote he mnataka siasa za aina gani?

Mnataka siasa za kistaarabu zisizo na unafiki na ukali hasa kutoka viongozi wa juu

Au mnataka siasa za misifa na ukali ukali wa kutumbuana kwenye kadamnasi bila kufuata itifaki?

Hii inahusu zaidi chama kilichopo madarakani mnataka kiwe na siasa za namna gani mnazozipenda?
Tunataka siasa za kuongozwa na watu tunaowataka sisi wenyewe na kwa kuzingatia rule of law!
 
Huyo unaemtaka unataka awe na haiba gani ya uongozi?

Mstaarabu asie na sifa na mwenye hekima au mkali mkali mwenye misifa na kutumbua watu ovyo bila itifaki?
 
Hili swali linapaswa kujibiwa na watanzania wote, hivi mnataka siasa za aina gani?

Mnataka siasa za kistaarabu zisizo na unafiki na ukali hasa kutoka viongozi wa juu

Au mnataka siasa za misifa na ukali ukali wa kutumbuana kwenye kadamnasi bila kufuata itifaki?

Hii inahusu zaidi chama kilichopo madarakani mnataka kiwe na siasa za namna gani mnazozipenda?
Mwafrika hanaga la maana alitakalo. Kiufupi hatueleweki nini hasa tunachotaka. Siasa za China zingetufaa sana.
 
Siasa za uwajibikaji, za ushawishi, ambazo zinatambua mamlaka ya viongozi inatoka kwa watu na wajibu wa viongozi ni kutekeleza matakwa ya wananchi.
Raisi awe na haiba gani ya uongozi mtumbuaji mtumbuaji bila kufuata protocol au mstaarabu asie na ukali ukali na kupenda kusifiwa
 
Siasa za kupenda kusifiwa ni “performative” hazina tija yoyote kwa wananchi, zinamnufaisha anayesifiwa tu. Lakini, wanasiasa kwa hulka zao ni watu wa kutafuta kusifiwa, kuonesha ya kuwa wanakubalika. Katika jamii iliyojaa watu walio na elimu duni ni vigumu sana kuepuka wanasiasa wa namna hii. Pamoja na kudai siasa safi, sisi wananchi tujielimishe juu ya uongozi, utawala bora na maendeleo ya watu. Ujinga wa wananchi unazaa UCHAWA.
 
Mwafrika hanaga la maana alitakalo. Kiufupi hatueleweki nini hasa tunachotaka. Siasa za China zingetufaa sana.

Siasa zetu sasa hivi zina tofauti gani na za China? Rafiki kipenzi wa CCM ni chama cha kikomunist cha China. Ama kiini macho cha vyama vingi kimekuziba macho mkuu?
 
Raisi awe na haiba gani ya uongozi mtumbuaji mtumbuaji bila kufuata protocol au mstaarabu asie na ukali ukali na kupenda kusifiwa

Bora awe mtuambuaji, mkali anayependa sifa. Lakini kwanza asiwe muuaji, mtekaji, mtesaji,mfiraji wa Watanganyika.

Awe mzalendo, asiwe fisadi na kujaza familia yake serikalini,asiwe mbaguzi na kuwatenganisha Watanzania kidini, kikabila, kikanda.

Rais anayeweza kusimamia huduma jamii kama maji, umeme kwa 27,000, kusimamia rasilimali zetu, sio kugawa hovyo rasimali za Taifa,mchapakazi, kupunguza rushwa na uonevu.

Muhimu asiwe na dharau, chuki kubwa kwa Watanganyika na kuhamisha kodi zao, rasimali zao kwenye familia yake akiwachukulia Watanganyika kama watumwa wake.
 
Tunataka siasa za haki
Haki juu ya nini?

Kiongozi wa chama tawala awe na aina gani ya uongozi au awe na haiba gani kama kiongozi mkuu wa nchi mpole mstaarabu au mkali na mtumbuaji?
 
Hapa sio kuwa atakuwa Mungu mtu mpenda kusujudiwa maana utumbuaji wakati mwingine haufuati utaratibu na itifaki je huoni atakuwa dictator?
 
Mnataka siasa za kistaarabu zisizo na unafiki na ukali hasa kutoka viongozi wa juu
Hizo siasa za kistaarabu kutoka kwa hawa ccm?
Maana nitauliza ni kipi kinafanya wasiwe wastaarabu?

Wananchi wanachotaka ni nchi kupata maendeleo umaskini kupungua
 
Ni bora kujiridhisha kwanza makosa kabla ya kutumbua. Nina uhakika Rais huwa anapewa briefing ya kutosha kabla ya kufanya utumbuaji.

Mbona huyu wako ametumbua wengi tu kutumia mabavu kama Ndugai, DGIS waliokataa uhuni wake. Ameteka watu kibao kama Heche, Kibao, Soka, Dr Godfrey Malisa, Polepole, Chaula na wengine wengi.

Lakini ni bora kuliko muuaji, mtekaji, mfiraji, mtesaji, mbaguzi, mdini, fisadi kuu.
 
Hili swali linapaswa kujibiwa na watanzania wote, hivi mnataka siasa za aina gani?

Mnataka siasa za kistaarabu zisizo na unafiki na ukali hasa kutoka viongozi wa juu

Au mnataka siasa za misifa na ukali ukali wa kutumbuana kwenye kadamnasi bila kufuata itifaki?

Hii inahusu zaidi chama kilichopo madarakani mnataka kiwe na siasa za namna gani mnazozipenda?
Swali lako lakijinga/kifala na haliwezi kujibiwa na waTanzania wote.
Mpaka leo hujui maana ya siasa ni nini??!
Hizo siasa za kistaarabu kutoka kwa hawa ccm?
Maana nitauliza ni kipi kinafanya wasiwe wastaarabu?

Wananchi wanachotaka ni nchi kupata maendeleo umaskini kupungua
Mkuu tuwaulize kwanza; Maana ya siasa ni nini? Kumbe kuna siasa ya ustaarabu na isiyo ya kistaarabu??
 
Haki juu ya nini?

Kiongozi wa chama tawala awe na aina gani ya uongozi au awe na haiba gani kama kiongozi mkuu wa nchi mpole mstaarabu au mkali na mtumbuaji?
Huyo kiongozi mpole mstaarabu unampata wapi kwenye chama tawala?
 
Swali lako lakijinga/kifala na haliwezi kujibiwa na waTanzania wote.
Mpaka leo hujui maana ya siasa ni nini??!

Mkuu tuwaulize kwanza; Maana ya siasa ni nini? Kumbe kuna siasa ya ustaarabu na isiyo ya kistaarabu??
Hadi Leo nakua na huu umri sijawahi kuona huo ustaarabu, sijui yeye kauona wapi
 
Haki🇹🇿
Justice🇬🇧
Justicia🇪🇸
Justis🇯🇲
Giustizia🇮🇹
Gerechtigkeit🇩🇪
正義🇯🇵
正义🇨🇳
 
Haki juu ya nini?

Kiongozi wa chama tawala awe na aina gani ya uongozi au awe na haiba gani kama kiongozi mkuu wa nchi mpole mstaarabu au mkali na mtumbuaji?
Kiongozi haitaji haiba mkuu anahitaji kufata katiba,sheria na kanuni za nchi.
 
Back
Top Bottom