Nasikitishwa na kukerwa na hawa watangazaji wa baadhi ya radios hasa pale wanapoonyesha hisia zao za kiasiasa waziwazi na hata kuwa bias wanapotoa taarifa. Hasa nikizungumzia kituo cha radio cha clouds fm katika kipindi cha asubuhi ambacho kianendesha na huyu kijana aitwaye Gerald Hando.
Huyu mtu amekuwa wa hovyo sana hasa kwa kubagua magezeti ya kusoma, lakini kwa magazeti machache anayosoma anadiriki kusoma mambo machache tu ambayo yanaki-favour chama tawala. Mwanzake Paul James amekuwa mjanja zaidi kwa kujiweka pembeni (huenda hataki kuonyesha hisia zake), lakini huyu Hando anaamua kujitoa mhanga kwa kufanya wendawazimu huo.
Tunaamini si radio ambayo inamilikiwa na mwanasiasa au kuwa katika mlengo flani wa chama, tunadhani ingekuwa vyema kusimama katikati pasipo kubagua nini usome na nini usisome. Mbona mwenzie Godwin Gondwe pamoja na kushiriki ktk kura za maoni kwa tiketi ya chama tawala kwa tiketi ya Ubunge lakini akiwa anasoma habari huwezi kutambua kama ni mtu ambaye yuko chama flani. Hii ina maana kuwa na-practice professionalism.
Vijana wa kihuni kama hawa Kusaga angetimua wote, ingawa najua Kusaga pia ni walewale!
Nawasilisha!