Hivi wataalam wa kilimo toka SUA wana impact gani! Mbona hawasikiki?

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,660
15,744
Yani mchango wao hauonekani kabisa katika kuinua sekta ya kilimo na mifugo.

Sekta ya kilimo imeendelea kuwa duni tangu nchi ipate uhuru na hawa jamaa wameshindwa kabisa ku transform kilimo.

Kifupi hawana impact kama Makapuku forum.

Siku mkirogwa mkanipa urais hiki chuo ntakifuta katika siku zangu mia za kwanza...
 
Watafute upate ushauri usilalamike.

Angalia wenzako hapo-http://ushaurikilimo.org/maswalimajibu.php
 
Ulishakwenda kwenda kupmba ishauri wakakunyima? Usikimbilie kulaumu watalamu kama huna ufahamu. Kwa kifupi kilimo endelevu ni muunganikano wa watalamu, wakulima na serikali. Sasa chambua hapo iyajua wapi pana tatizo
 
Yani mchango wao hauonekani kabisa katika kuinua sekta ya kilimo na mifugo.
Sekta ya kilimo imeendelea kuwa duni tangu nchi ipate uhuru na hawa jamaa wameshindwa kabisa ku transform kilimo.
Kifupi hawana impact kama Makapuku forum.
Siku mkirogwa mkanipa urais hiki chuo ntakifuta katika siku zangu mia za kwanza...
Huwezi kuona kwa macho mkuu,hawa watu shughuli zao ni kwenye field zaidi na sio kama unavyoona fani nyingine kama wanasiasa,wanasheria,wahasibu n.k n.k...
 
Toka kianzishwe hao graduates huwa wanapotelea wapi? Maana mashamba na kilimo bado kimedumaa tu.
Naona kama wamezubaa, Nchi haiwezi kuwa na CHUO KIKUU cha kilimo miaka mingi lakni bado wananchi wanalia kwa kukosa ushauri wa kitaalamu.
 
Tupe heshima yetu mkuu ilaum serikali yako CIO cc cc tunatumika sana mashamban na tunajituma sn kwa wakulima njoo sua uclalamike tuu bure!!!
 
Mimi nahisi Kilimo hakiwezi kukua Kwa kuangalia wataalam Tu. Kwa mfano kama kuna ukame SUA hawafundishi kuleta mvua, kama Ni kujenga miundo mbinu ya umwagiliaji inategemea bajeti ya serikali sio maafisa Kilimo, Lakini unataka uone wanatekeleza kaone mwamko wa wakulima hata katika matumizi ya mbegu zilizoboreshwa Siku hizi vijiji wanatumia sana kuliko hapo nyuma.
 
Yani mchango wao hauonekani kabisa katika kuinua sekta ya kilimo na mifugo.
Sekta ya kilimo imeendelea kuwa duni tangu nchi ipate uhuru na hawa jamaa wameshindwa kabisa ku transform kilimo.
Kifupi hawana impact kama Makapuku forum.
Siku mkirogwa mkanipa urais hiki chuo ntakifuta katika siku zangu mia za kwanza...
Wewe uko Dar es Salaam technologies za Kilimo utazijuaje?There are so many technologies in various crops, soil science and water management, horticulture, livestock ,food nutrition etc. which you take for granted ambazo zimetoka SUA na other research institutions.Bahati mbaya local technologies zinapigwa vita sana
na international companies ambazo ziko eager to make money through their technologies.Kwa mfano local varieties developed by our local institutions for Maize kama TMV 1,Kito,Katumani,Ilonga Composite zinakuwa strangled by introduced varieties tena makusudi and nothing is being done to protect them. Infact international companies are at war with our germplasm.

Kwa makusudi kabisa we need to develop our local seed industry and maintain our germplasm.Tatizo ni kwamba Monsanto wakale wapi? They are doing all they can,using all means at their disposal to make sure that we use their technologies by using their massive acquired wealth.
 
What i can say ni kwamba wakulima wa kitanzania hawataki kibadilika ndio maana kilimo hakisongi ,ukifanya utafiti wakulima wamefundishwa sana na taasisi za binafsi na za kiserikali but ukipima impact ya mafunzo ni zero sababu mtu amachofundishwa sicho anachokifanya ,na hapo ndipo anaepima kilimo kama mtoa mada kwa impact huoni kama kuna kilichofanyika . First ni watanzania tujifunze kubadilika na kupokea elimu ndipo kilimo kitasonga.
Huwezi amini mpaka leo hii wenzetu wanatoka kwenye hybrid wanaenda kwenye G.M.O (siungi mkono lakini gmo) ila sisi bado tunatumia mbegu za kichanjani,bado tunakamua mbegu kwenye mazao ya shambani na kuzipanda tena . Kila mtu angekua kwenye hybrid ungeona impact ,kila mtu angejua anatoa nn shambani ungeona impact. Ila mtanzania anatumia milioni 2 kuzalisha zao akivuna anauza milioni 1 na anajisifia amepata faida ,inasikitisha sana kwa sisi ambao tuko field na tunaona hali ilivyo na hakika binafsi ndio inanipa morali ya kuongeza bidii kubadili mindset za farmers
 
SUA bora ifutwe haina impact yoyote kwa Taifa

Suluhu sio kufuta mkuu, kama approach yetu itakua ni KUFUTA chochote kile kinachoonekana kuwa haki_perform badala ya kuangalia ni namna gani tunakiwezesha kuleta tija, basi mimi nashauri TUIFUTE NCHI kwanza.
 
Yani mchango wao hauonekani kabisa katika kuinua sekta ya kilimo na mifugo.
Sekta ya kilimo imeendelea kuwa duni tangu nchi ipate uhuru na hawa jamaa wameshindwa kabisa ku transform kilimo.
Kifupi hawana impact kama Makapuku forum.
Siku mkirogwa mkanipa urais hiki chuo ntakifuta katika siku zangu mia za kwanza...

Kosa lako la SASA ni kufikiri kwamba tunaweza tukarogwa na tukakupa urais, kosa lako la BAADAE (ikitokea tumerogwa) ni kuifuta hiyo taasisi muhimu hata kama impact yake inaonekana ni ndogo.

Tukiachilia mbali makosa hayo, ni ukweli usiopingika kwamba umeleta mada nzuri sana na yenye tija kwa mustakabali wa nchi yetu inayotegemea kilimo. Kwa maoni yangu SUA bado wana deni kwa nchi na pia inawezekana nchi nayo ina deni kwa SUA.

Acha mjadala uendelee...
 
Back
Top Bottom