Hivi Wanawake wote mpo kama huyu?

Hivi Wanawake wote mpo kama huyu?

Jamani wanajamvi msaada tutani , mke wangu ananishangaza sana.

Kabla sijamuoa nilimpa taarifa kuwa nina mtoto na akakubali kuwa atamlea kama mwanaye na akashauri nimchukue kutoka kwa mama yake ili tuishi naye sasa siku zikawa zinakatika mtoto umri umesogea na mda wa kwenda shule umefika ikabidi niende kumchukua , ila tukakubaliana kuwa nimwache kwa mama yangu kwanza , to cut story short nilikuta kwa mama mazingira si mazuri kwan mama ni mtu yupo bize sana na kazi zake ni mwajiriwa pia kilimo na mengineyo nikaona mda wa kumwangalia mtoto utakuwa mchache nikabadaili mawazo nikaja naye ninakoishi.

Nilipofika naye nikampa taarifa kwanini sikumwacha mtoto na kuamua kuja naye ikawa ni ugomvi kwenda mbele kila mtoto anachokifanya kwake ni kibaya, kila ntachomfanyia mtoto anasema namdekeza kwa kweli mimi kama baba naumia sana kwani sina hata nafasi ya kumsaidia mtoto wangu kumjenga kifikra na kimawazo , kwan nikitoka naye tu inakuwa nongwa nikaa naye kwenye kochi nongwa nikila naye nongwa , nina watoto wawili mmoja nimezaa naye na bado mdogo sana hajaanza kuonge na bahati nzuri wote wa kiume sasa nafikiria mambo mawili matatu ambayo ndiyo nahitaji ushauri kwenu,

1. Je nimpeleke mtoto boarding school mpaka mdogo wake akuwe ili niwe natoka / au nakaa nao pamoja kwan nataman kuwajenga wanangu kimaadili mapema.

2.Nimpeleke tu akaishi kwa bibi yake rejea hapo juu kuhusu mama yangu na ufinyu wa nafasi ya kulea mtoto mdogo kwan sisi wote watoto wake tushaanza kujitegemea.

3.Nivumilie tu labda ipo siku atajirudi kwan ashaniambia kuwa moyo wake umeshindwa kabisa kumkubali mtoto wangu huyu na anadai nimemsababishia shambulio la moyo kwa mawazo.

4. Naipenda familia yangu , nampenda mke na watoto wote sipendi kumpoteza hata mmoja, je nifanyeje wadau nipo njia panda.


Kwa hayo machache naitaji busara zenu zaid , hii sio hadith nio maisha halisi ya mtu hivyo utani tupa kule changia mawazo ya busara kama huna cha kuchangia naomba upite wima sio lazima kuandika.


ASANTEN KWA KUNISIKILIZA, NAWASILISHA.

Mke c damu yangu, watoto ndio damu yako, fanya maamuz mwenyewe kuhusu huyo mkeo, km ni mimi ningefukuzia mbali mwanamke. Wewe ni baba chukua jukumu lako km baba.
 
Huna akili boya wewe,hivi kama mwanaume unashindwa kujua kama Wewe ndio kichwa cha nyumbaa? Hilo jini lako litasababisha mtotowako awe hata shoga jinga sana Wewe ,ushauri unaomba wa nini sasa?
Wewe ni mr. or mrs , subir yakikukuta walau nusu ya haya utajua kuwa unahitaji ushaur au la.
 
Du pole mtoto bado mdogo,sana mimi wala sishangai yashanikuta hayo nami nimelelewa na mama wa kufikia yani hayo unayoongea ni kama umecopy na kupaste maisha yangu yani mzee alikua akininunulia vitabu vya shule ni shida, nikipewa kishilingi mia cha kwenda nacho shule ni shida mtu ananuna , nikiumwa mzee akinijulia hali ni matatizo yani hakuna jema yani wamama sijui huwa wapoje japo sasa nimekua binti mkubwa miaka 27 sasa lakini chamoto nilikiona katika makuzi yangu, mbaya zaidi ukute huyo mama awe na ndugu zake humo ndani yani unatengwa ka yai viza aisee watakuteta kiruga , watakusengenya yani matatizo juu ya matatizo. Du mhurumia huyo mtoto tena kama mama yake yupo mpeleke tu mimi mwenzenu sikua na pakukimbilia wala pa kupata unafuu
mama angu alfariki nikiwa nna umri wa miaka 2 tu. Ndio baba huwa wanajitahidi kukinga vifua lakini inafikia pindi nae anakua upande wa mkewe sasa sijui uwa ni limbwata cijui ni nini kwa kweli. Namhurumia sana mtotot hapa machozi yanilengalenga thread yako imenikumbusha mengi niliyopitia dah dunia hii! Tena sa nyingine utakuta anampelekea maneno ya uongo baba ako ilimradi tu mtoto uonekane mbaya yani mzazi kama hana akili ya kujiongeza utatembezewa fimbo kila siku. Yani kwa kweli baadhi ya mama zetu hawa wa kufikia watoto wao ndo huwa wanapenda wapewe kipaumbele mwenzangu na mimi unaonekana kama zombi hivi unawekea watu kiwingu. Nimesikitika sana pole sana mana nimekumbuka mbali.
Pole sana kama usemavyo humo ndani kuna ndugu zake kibao pia kuna mtoto mdogo kabisa wa miaka mitatu wa mama yake mdogo na anafanya mambo ya ajabu kuliko mtoto wangu akilia kidogo hata kama kaanguka utasikia we kwanini unampiga mwenzako unamwoneka au kwa sababu mdogo yaan ni shidaaaaaaaaaa
 
Nimejikuta nawaza kwa sauti japo sikutaka kuchangia ila wacha niulize tu kisha nishauri!

Kwani mama wa mwanao ameolewa? Kama jibu ni hapana, na unadhani ana mazingira bora ya kumlea mwanaye mrudishe kwa mama yake uwe unatafuta muda hata mara 2 hadi 4 kwa mwaka unaenda na kukaa na mwanao umjenge utakavyo hadi mdogo wake akifika darasa a pili ndo umchukue.

Angalia tu uamuzi huu usisababishe kuongeza mtoto wa tatu huko....
kaolewa nilizaa naye nikiwa mwanafunzi nilipomaliza chuo nilimkuta kashaolewa
 
Nina rafiki ana miaka 30 sasa,ila alikua na mama wa kambo anasema mambo aliyofanyiwa na mama yake huyo wakati baba yake yupo kazini yalimwathiri mpaka leo,amechukia kuoa,
amechukia kuishi na watu hasa wanawake,
inshort ameathirika kisaikolojia mpaka leo,
kama kweli unampenda mwanao tafuta namna ya kumweka mbali na mama huyo aliyepata shinikizo la moyo kutokana na uwepo wa mwanao hapo nyumbani,

Wewe umekuwaje rafiki yake kama ana chuki na wanawake?
 
Huo si uamuzi rafiki akiondoka mwanamke itamlazim huyo baba akatfute mama wa tatu na mtoto pia wa mama tofauti, wayazungumze tu sometimes ukitumia ubaba wako kwa ubabe utamuharibu pia mtoto.Mama ana nafasi nzuri ya kumjenga au kumuharibu mtoto. Akimuwekea mgomo baridi atamlea mtoto ka yai sidhani kama unayajua madhara yake huyo mama akiamua kufanya hivyo ili tu abaki kwenye ndoa yake

Sio lazima aoe, ni bora nimpeleke mwanangu boarding nikijua kuwa sina mke wa kumlea kuliko kujua kuwa nina mke mwenye uwezo wa kulea mwanangu lakini mke huyo amejawa na roho mbaya...

Huyo mwanamke hana sifa ya kuitwa mama, wala hana sifa ya kuwa ndani ya ndoa abadani asilani...

Sisi Waafrika tuna hulka ya kuleleana watoto tena kwa upendo kabisa hata kama hakuna undugu...

Kwa wale waliokulia vijijini wanatambua fika ambavyo tukiwa wadogo unaweza kuachwa kwa mama jirani na ukatunzwa vizuri pasipo ubaguzi wowote...

Nijuavyo mimi sifa ya mwanamke ni kuwa na utu na ubinadamu kwa kuwa anajua ni nini maana ya thamani ya uhai...

Hebu walau wanawake wajifunze walau hata kupitia picha hii ambapo mwanamke yu radhi kumnyonyesha mwana mbuzi ili walau naye apate malezi...

Sasa kama mwanamke anaweza kuonesha uungwana kwa mnyama kiasi hiki sembuse mwanadamu mwenzake???

300491_10150319698416805_300530356804_8252892_477793362_n.jpg
 
Mh hapa pagumu.cz mama yake mzazi kama nae kishaolewa na mwanaume mwngne huwez jua hali itakuwaje uko,na ukisema umuache hyu mke Roho mbaya naye ushazaa nae huyu mtoto mdogo malez yake itakuaje?kitendawili kinarud kulekule!jaman wanasema ndoa karata but ukishaona tiari una mtoto kabla inabidi umakini Wa hali ya juu..hyo mke ungemtest kwanza kama anaeza kuishi na mtoto Wa kambo bfor.vngnevyo Maji yashamwagka,ongea na mama yako muone mnasolve vipi hii ishu ka vpi umrudshe uko under extra care ya ndugu Wa kumuangalia pindi mama akiwa busy
 
Nilichoona hapo kaka unampenda sana mkeo na huwezi kuchukua maamuzi juu yake ila nakusihi jambo ogopa sana mwanamke akishaonyesha kitu flani hakubaliani nacho atafanya lolote ili aepukane na icho kitu naomba utumie akili ya kumrudisha huyo mtt kwa mama atafanyiwa vizuri ukiwepo ila ukiwa haupo atafanyiwa vya ajabu na vitamuumiza baadae kiakili mtoe huyo mtt haraka huyo dada ni jini sio mtu tena mbele ya huyo mtt mijanamke mingine fyuuuuiuu.
 
Huyo mkeo ndiye atakaye kuwa anashinda mtoto nyumbani muda mwingi zaidi yako kama mwanamke anaonekana ni mzito katika kumkubali ni vyema ukampeleka kwa bibi yake kumuepushia shida mtoto. maana anaweza akawa ananyanyaswa bila wewe kujua
.Wanawake wengine sijui wanashida gani kwani huyo mtoto anapunguza nini hapo nyumbani au anakula kiasi gani kwanza yeye kamkuta na aliaambiwa je ingekuwa mtoto kazaliwa wakati ushamuoa ingekuwa kuwaje?
 
Mkuu Kaa chini na mkeo na jaribu kusikiliza concerns zake. Na umweleweshekwa mara ya mwisho umuhimu wa watoto tena ndugu kukua pamoja. Muweke wazikabisa kuwa mtoto haendi kwa bibi wala wapi bali atalelewa kwenye famila yenuhivyo ajiadjust kuelewa hivyo. Naona mkeo ana insecurities tu ila pia ana dalili za hatari sanakwenye ndoa yenu maana haitaishia kwa mtoto tu. Je mama yako akiugua ukitakaaje kwako kwa matibabu? Au bahati mbaya dada yako kafariki ukitaka mumleemwanae? Muonye kuhusu athari za wivu na uchoyo na kama haelewi jaribukushirikisha wasimamizi wenu wa ndoa au wazee wamweleweshe . Ni dhambi kubwasana kumuadhibu mtoto asiyehusika. Pia mambo ya Mungu ni siri kubwa , huyomtoto anayemchukia anaweza kuwa msaada mkubwa sana katika maisha yenu.Muhakikishie kuwa unawapenda wote kama familia na hauko tayari kuitenga familia. La watoto wote wawili waende kwa bibi wewe utamjengea bibi na kuweka msaidiziawalee wote. In this case u need to strictly stand as a man.
 
Ila jamani ndo nasisi tujifunze hapo.........hivi unaachaje mwanao alelewe na mwanamke mwingine wakati we mwenyewe uko hai? Mi hatakama ninamaisha ya tabu kiasi gani siwezi kukubali mwanangu alelewe na mama wa kambo.......ni bora mtoto wangu ale mchicha na maharage akiwa amekaa tena anaamani zote kuliko ale nyama za kuku uvunguni mwa kitanda au store huku analia.
 
Mama yake mzazi ameshaolewa na boarding schools huwa zina mwisho wake...

Sijui kama watu mnatalitambua hili kuwa kwa namna yoyote ile, kumtenga huyo mtoto kwa kuyafanya hayo mnayoyashauri kutaleta athari kwa mtoto kujiona kuwa anatengwa na wazazi wote wawili...

Siku zote mchawi mkabidhi mwana akulele, wa kudeal naye hapo ni huyo mwanamama mkorofi...

Yani i mean mama yake mzazi wa huyo baba mtoto mi nimeshuhudia watoto wengi wakitesa sana hata akimkabithi mchawi kwa kesi hi.aisee nimeona mateso yanayowaathiri watoto bora boarding au kwa bibi yake mbona wengine tuliweza survive boarding hivo hivo na udogo wetu ndo mana inatakiwa kuzaa watoto kwenye ndoa kuepusha haya matatizo huyu mwanaume angekuwa na msimamo ingekuwa sawa mana wanawake wanamuinfluence mwanaume anakuwa ana msikiliza yeye na mtoto anaumia
 
Asante sana watu8, hili ndo jibu sahihi kabisa, harafu sijui kwa nn nina hasira

Kuyafanya haya yote bado hayabadilishi uhalisia ya kwamba huyo ni mwanao...

Wewe ni mwanaume na ni kichwa cha familia, kaa chini umuonye huyo mkeo ya kwamba aamue moja;

Kuishi kwa amani na 'mtoto wenu' au yeye aondoke
 
Binafsi nimelelewa na mama mdogo lakini she is the best and am proud of her! kwani kuna ugumu gani kukaa na mtoto wa mwanamke mwenzio ambaye alikuwa na mumeo kabla yako mimi binafsi sielewi shida ni nini? na nimejifunza kitu kikubwa sana kutoka kwa mama yangu huyu jamani.
Hiki kilikuwa ni kipindi chake kizuri cha kujiongezea credit kwa mumewe kwa kumpenda huyo malaika sema hajielewi .
 
Hili nitatizo gumu kwani anassema umemkwaza roho yake, komaa naye mtoto asiondoke hapo, hakikisha kuwa mtoto ana vitabia vibaya, boardingi sio nzuri walitaka kuniaribia mtoto wangu,
Niambie ana miaka mingapi nikupe njia sahii
 
Nadhani huna uhakika na kile unachokiongea......hivi unajua wanawake wanavyolundikiwa watoto tena wengine wamezaliwa ndoa ikiwa imefungwa tayari?

Sasa ndio umeandika nini?
 
kwa watoto waliopatikana kwenye michepuko wakati watu wana ndoa yao tayari naweza kukubaliana na wewe,lakini kwa watoto waliopatikana kabla ya ndoa na wawili hao wakaambiana ukweli juu ya hao watoto kabla ya kufunga ndoa mara nyingi watoto hao hawateswi na mama wa kambo,na nina ushahidi wa kutosha kwenye familia yetu

Una uhakika gani?
 
Wanawake wote wapo hivyo ndugu tatizo ulifanya haraka kumleta huyo mtoto.
 
Wanawake wote wapo hivyo ndugu tatizo ulifanya haraka kumleta huyo mtoto.


Have u reseached or u have a generalization syndrome? Haraka 5 yrs? no wonder time management is a critical issue
 
Back
Top Bottom