Hivi Wanawake wote mpo kama huyu?

Hivi Wanawake wote mpo kama huyu?

Japo hutakiwi kumuendekeza huyo mkeo ila kwa upande mwingine mwanao akikaa hapo atateseka na hata uwezo wake darasani unaeza kuyumba. Mpeleke mwanao boarding kwa usalama wake dhidi ya manyanyaso ya mama wa kambo.
 
"Moyo wake umeshindwa kabisa kumkubali mtoto","umemsababishia shambulio la moyo"

Pole sana mkuu,tena sana aisee maana unaishi na shetani ndugu yangu.Nasikitika kukwambia kuwa huyo mwanamke ni hatari sana aisee,dah! Mungu akutangulie maana hizo kauli zake ni nzito mnoo.

Ningekuwa mimi huyo mbona angehama nyumba aniache na wanangu.
 
pole sana mkuu ila nakushauri mpeleke boarding atapata malezi better zaidi ya mkeo
 
Kuyafanya haya yote bado hayabadilishi uhalisia ya kwamba huyo ni mwanao...

Wewe ni mwanaume na ni kichwa cha familia, kaa chini umuonye huyo mkeo ya kwamba aamue moja;

Kuishi kwa amani na 'mtoto wenu' au yeye aondoke

Kweli kabisa! Mimi ni mwanamke ila nimekasirishwa na tabia mbovu na roho ya kutu ya huyo dada!..
Roho mbaya utadhani mtengeneza sumu???
Mtoto mtoto mama yake hayupo wewe ndiyo mama unashindwa kweli kupenda mtoto uliyemkuta kabla ya ndoa???
Mi ningekuwa mwanaume ningefukuza kwanza nijipange upya!
 
pole sana mkuu ila nakushauri mpeleke boarding atapata malezi better zaidi ya mkeo

Unajua sista roho inaniuma kwasababu mtoto atakosa malezi ya baba na mama kisa roho mbaya ya mwanamke! Kuna faida kubwa sana sana kupata malezi ya wazazi na siyo ya matrons shuleni!
 
Hata mimi yamenikuta ndg nimeamua mwanangu aishi kwa mama yake mzazi kwanza, mpaka atakapokuwa mkubwa
 
Hapana kaka angu co wanawake wote tupo ivo, ni weakness za mtu binafsi, sasa ndio yawezekana ulichukua jukumu la kumleta mtoto bila kumshirikisha wazo hilo ndo maana kawa ivo ingawa cdhani kuwa ni kosa la kukoseana amani ivo ndani ya nyumba, kaa angea naye asipokuelewa tafadhari uyo mtoto mpeleke kwa bibi la sivo utaachiwa maumivu,
 
Kwa huo mtazamo wa mkeo, bora umrudishe kwa mama ake aisee.
 
hapana kaka angu co wanawake wote tupo ivo, ni weakness za mtu binafsi, sasa ndio yawezekana ulichukua jukumu la kumleta mtoto bila kumshirikisha wazo hilo ndo maana kawa ivo ingawa cdhani kuwa ni kosa la kukoseana amani ivo ndani ya nyumba, kaa angea naye asipokuelewa tafadhari uyo mtoto mpeleke kwa bibi la sivo utaachiwa maumivu,
ok thanks ntaongea naye ingawa nshaongea naye sana
 
Mpeleke boarding jpo mdogo, lkn ni bora huko kuliko io harsh environment iliyopo
 
Kuyafanya haya yote bado hayabadilishi uhalisia ya kwamba huyo ni mwanao...

Wewe ni mwanaume na ni kichwa cha familia, kaa chini umuonye huyo mkeo ya kwamba aamue moja;

Kuishi kwa amani na 'mtoto wenu' au yeye aondoke

Ni kweli lkn ngumu kumeza.
 
Na waswas na wew unaroho kama yu uyo dada....always mtoto hanaga makosa kukaa na babaake ni hak yake unavokaa vizur na mtoto wa mwenzio unajipatia baraka kutoka kwa mung

Sina hiyo roho mbaya mtoto ni lazima apate penzi la babake na mamake mzazi. Ndoa ni ngumu sana hata wanaume ni wachache sana wanaoweza kulea mtoto wa mwanaume ndio maana unaona mleta mada anaogopa kumpeleka mtoto kwa mamake kwa kuwa mamake kaolewa! Hakuna haja ya kutumia ubabe ni wao wakae chini waelewane, mtoto ni mdogo sana kuanza kuwa mistreated.
Mleta mada usijaribu kumletea mkeo ubabe ndio utazidi kuongeza moto.

Kukaa vizuri na mtoto au mtu yoyote ni baraka lakini si wote wanaoelewa kama mke wa mleta mada so aende na mkewe taratibu.

Kumpeleka boarding sikushauri kabisa. Penda mkeo na omba sana Mungu atabadilika ns kumpenda mwanao
 
Pole sana mkuu. Ngoja waje wenye expiliensi haya mambo..
 
Mpeleke boarding jpo mdogo, lkn ni bora huko kuliko io harsh environment iliyopo

Boarding skul kwa watoto sio nzuri. Kila mtoto ana haki ya kupata na kuenjoy malezi ya wazazi wake na hapo ndo anapojifunza kwani Familia ndio shule ya kwanza katika nyanja mbalimbali.
 
nakushauri muache mkeo kwani hana huruma na malaika ndo atakuwa na huruma na wewe?
 
huyo mkeo ana matatzo... we mwambie kama vipi achape lapa akapumzike kwao mpaka atapoona moyo wake umemkubali huyo mtoto. kuna wanawake hawafai kudekezwa. kama alishajua mapema kuwa una mtoto na hawez kuishi nae asingekubali kuolewa.
option nyingne ni kumpeleka boardng umkabidhi kwa mwalimu ambae atakuwa anakupa updates za maendeleo yake mara kwa mara.

ila hebu mtishie mkeo hiyo option ya kwanza uone kama moyo wake hautolazmika kumlea dogo.

yote yakifeli mlete kwa aunt ninyo nitakulelea. lol
 
Back
Top Bottom