Hivi Wanawake wote mpo kama huyu?

Hivi Wanawake wote mpo kama huyu?

mke wako anajua utahamisha mapenz kwa mtoto mkubwa na kumwacha wa kwake hyo inatokea sana kwa familia ya aina yako

kussolve peleka mtoto boarding wkt ukimjenga mkeo kifikra awaone watoto wote ni wa kwake

ikishindikanaa wyf wako ni shida na atakua amekukalia kichwan hapo maamuz magumu yatahitajika.
 
Huna akili boya wewe,hivi kama mwanaume unashindwa kujua kama Wewe ndio kichwa cha nyumbaa? Hilo jini lako litasababisha mtotowako awe hata shoga jinga sana Wewe ,ushauri unaomba wa nini sasa?
 
Jamani wanajamvi msaada tutani , mke wangu ananishangaza sana.

Kabla sijamuoa nilimpa taarifa kuwa nina mtoto na akakubali kuwa atamlea kama mwanaye na akashauri nimchukue kutoka kwa mama yake ili tuishi naye sasa siku zikawa zinakatika mtoto umri umesogea na mda wa kwenda shule umefika ikabidi niende kumchukua , ila tukakubaliana kuwa nimwache kwa mama yangu kwanza , to cut story short nilikuta kwa mama mazingira si mazuri kwan mama ni mtu yupo bize sana na kazi zake ni mwajiriwa pia kilimo na mengineyo nikaona mda wa kumwangalia mtoto utakuwa mchache nikabadaili mawazo nikaja naye ninakoishi.

Nilipofika naye nikampa taarifa kwanini sikumwacha mtoto na kuamua kuja naye ikawa ni ugomvi kwenda mbele kila mtoto anachokifanya kwake ni kibaya, kila ntachomfanyia mtoto anasema namdekeza kwa kweli mimi kama baba naumia sana kwani sina hata nafasi ya kumsaidia mtoto wangu kumjenga kifikra na kimawazo , kwan nikitoka naye tu inakuwa nongwa nikaa naye kwenye kochi nongwa nikila naye nongwa , nina watoto wawili mmoja nimezaa naye na bado mdogo sana hajaanza kuonge na bahati nzuri wote wa kiume sasa nafikiria mambo mawili matatu ambayo ndiyo nahitaji ushauri kwenu,

1. Je nimpeleke mtoto boarding school mpaka mdogo wake akuwe ili niwe natoka / au nakaa nao pamoja kwan nataman kuwajenga wanangu kimaadili mapema.

2.Nimpeleke tu akaishi kwa bibi yake rejea hapo juu kuhusu mama yangu na ufinyu wa nafasi ya kulea mtoto mdogo kwan sisi wote watoto wake tushaanza kujitegemea.

3.Nivumilie tu labda ipo siku atajirudi kwan ashaniambia kuwa moyo wake umeshindwa kabisa kumkubali mtoto wangu huyu na anadai nimemsababishia shambulio la moyo kwa mawazo.

4. Naipenda familia yangu , nampenda mke na watoto wote sipendi kumpoteza hata mmoja, je nifanyeje wadau nipo njia panda.

Kwa hayo machache naitaji busara zenu zaid , hii sio hadith nio maisha halisi ya mtu hivyo utani tupa kule changia mawazo ya busara kama huna cha kuchangia naomba upite wima sio lazima kuandika.

ASANTEN KWA KUNISIKILIZA, NAWASILISHA.

Mpeleke mtoto kwa mama yake....ila uwe unamhudumia. Wanawake wana roho mbaya sana wakichukia...anaweza mfanya kitu usimulie hadi vitukuu vyako.
Mpeleke kwa mama yake ila uwe unampa matunzo yoteee. Na mwambie huyo mkeo kwamba utampa matunzo yote yeye na mama yake. Akikua....akifika sekondary mpeleke boarding.
 
Kagundua we ni dhaifu unampenda kushinda mtoto wako anataka kukupima.Achague kunyoa au kusuka.NYUMBA INAPENDEZA NA WTOTO
 
miaka mitano ndo kafunga mwezi wa sita.

Du pole mtoto bado mdogo,sana mimi wala sishangai yashanikuta hayo nami nimelelewa na mama wa kufikia yani hayo unayoongea ni kama umecopy na kupaste maisha yangu yani mzee alikua akininunulia vitabu vya shule ni shida, nikipewa kishilingi mia cha kwenda nacho shule ni shida mtu ananuna , nikiumwa mzee akinijulia hali ni matatizo yani hakuna jema yani wamama sijui huwa wapoje japo sasa nimekua binti mkubwa miaka 27 sasa lakini chamoto nilikiona katika makuzi yangu, mbaya zaidi ukute huyo mama awe na ndugu zake humo ndani yani unatengwa ka yai viza aisee watakuteta kiruga , watakusengenya yani matatizo juu ya matatizo. Du mhurumia huyo mtoto tena kama mama yake yupo mpeleke tu mimi mwenzenu sikua na pakukimbilia wala pa kupata unafuu
mama angu alfariki nikiwa nna umri wa miaka 2 tu. Ndio baba huwa wanajitahidi kukinga vifua lakini inafikia pindi nae anakua upande wa mkewe sasa sijui uwa ni limbwata cijui ni nini kwa kweli. Namhurumia sana mtotot hapa machozi yanilengalenga thread yako imenikumbusha mengi niliyopitia dah dunia hii! Tena sa nyingine utakuta anampelekea maneno ya uongo baba ako ilimradi tu mtoto uonekane mbaya yani mzazi kama hana akili ya kujiongeza utatembezewa fimbo kila siku. Yani kwa kweli baadhi ya mama zetu hawa wa kufikia watoto wao ndo huwa wanapenda wapewe kipaumbele mwenzangu na mimi unaonekana kama zombi hivi unawekea watu kiwingu. Nimesikitika sana pole sana mana nimekumbuka mbali.
 
bora umpeleke kwa bibi yake na umuwekee mfanyakazi kwa ajili ya kumsaidia mtoto,hapo kwako mtoto ataharibiwa kisaikolijia na huyo mkeo na anaweza hata kumfanyia kitu kibaya kupitia watu wengine,mara 100 kwa bibi pamoja yuko bize atakuwa na uchungu nae
 
wanawake waliowengi...hawawezi kulea watoto wa wenzao...

kuwa na msimamo hilo la kwanza, pili mfanye ajue wote ni watoto wenu na wote wako sawa...huo ujinga ujinga wake we chapa vibao tu...mtu ulishamwambia sahiz analeta mbwembwe za nn
 
Huyo mwanamke kama angekuwa na mtoto wa nje hata kama ungekuwa humtaki ungefyata kimya, maana unaonekana unaongozwa na mkeo.
Mwanamke ameona wewe ndio una shida nae sana, hivyo anakuendesha, subirh mama yako na ndugu zako wapigwe marufuku kuja hapo kwako ndio utajua. lakini kumbuka kuwa duniani huna ndugu zaidi ya wazazi,watoto, kaka&dada zako, mke si ndugu yako. Kwangu mke asije kujaribu kutingisha kiberiti kwa hao watu, nampa taraka siku hiyohiyo. kama hamtaki mtoto wako aondoke.
 
Kuyafanya haya yote bado hayabadilishi uhalisia ya kwamba huyo ni mwanao...

Wewe ni mwanaume na ni kichwa cha familia, kaa chini umuonye huyo mkeo ya kwamba aamue moja;

Kuishi kwa amani na 'mtoto wenu' au yeye aondoke

Kwa wanawake wa namna yake, atakubali kuwa mpole kinafiki ila huyo mtoto atakiona cha moto wakati baba yake kaenda job or hayupo nyumbani. Mtoto atateseka kimya kimya!
 
Nimejikuta nawaza kwa sauti japo sikutaka kuchangia ila wacha niulize tu kisha nishauri!

Kwani mama wa mwanao ameolewa? Kama jibu ni hapana, na unadhani ana mazingira bora ya kumlea mwanaye mrudishe kwa mama yake uwe unatafuta muda hata mara 2 hadi 4 kwa mwaka unaenda na kukaa na mwanao umjenge utakavyo hadi mdogo wake akifika darasa a pili ndo umchukue.

Angalia tu uamuzi huu usisababishe kuongeza mtoto wa tatu huko....
 
Kwa wanawake wa namna yake, atakubali kuwa mpole kinafiki ila huyo mtoto atakiona cha moto wakati baba yake kaenda job or hayupo nyumbani. Mtoto atateseka kimya kimya!

Pia mkuu lazima tukubali kuwa kumuhamisha mtoto huku akijua kuwa anachukiwa na mama yake wa kufikia hakutakuwa na msingi mzuri kisaikolojia...

Ni rahisi kudeal na huyo mtu mzima ambaye ameamua tu kujivika ukatili
 
Muda wote nakuona humu jamvini sikuwa najua jinsia yako...umeandika kwa hisia sana

Kweli kabisa! Mimi ni mwanamke ila nimekasirishwa na tabia mbovu na roho ya kutu ya huyo dada!..
Roho mbaya utadhani mtengeneza sumu???
Mtoto mtoto mama yake hayupo wewe ndiyo mama unashindwa kweli kupenda mtoto uliyemkuta kabla ya ndoa???
Mi ningekuwa mwanaume ningefukuza kwanza nijipange upya!
 
Kuyafanya haya yote bado hayabadilishi uhalisia ya kwamba huyo ni mwanao...

Wewe ni mwanaume na ni kichwa cha familia, kaa chini umuonye huyo mkeo ya kwamba aamue moja;

Kuishi kwa amani na 'mtoto wenu' au yeye aondoke

Huo si uamuzi rafiki akiondoka mwanamke itamlazim huyo baba akatfute mama wa tatu na mtoto pia wa mama tofauti, wayazungumze tu sometimes ukitumia ubaba wako kwa ubabe utamuharibu pia mtoto.Mama ana nafasi nzuri ya kumjenga au kumuharibu mtoto. Akimuwekea mgomo baridi atamlea mtoto ka yai sidhani kama unayajua madhara yake huyo mama akiamua kufanya hivyo ili tu abaki kwenye ndoa yake
 
Nina rafiki ana miaka 30 sasa,ila alikua na mama wa kambo anasema mambo aliyofanyiwa na mama yake huyo wakati baba yake yupo kazini yalimwathiri mpaka leo,amechukia kuoa,
amechukia kuishi na watu hasa wanawake,
inshort ameathirika kisaikolojia mpaka leo,
kama kweli unampenda mwanao tafuta namna ya kumweka mbali na mama huyo aliyepata shinikizo la moyo kutokana na uwepo wa mwanao hapo nyumbani,
 
  • Thanks
Reactions: Kbd
Du pole mtoto bado mdogo,sana mimi wala sishangai yashanikuta hayo nami nimelelewa na mama wa kufikia yani hayo unayoongea ni kama umecopy na kupaste maisha yangu yani mzee alikua akininunulia vitabu vya shule ni shida, nikipewa kishilingi mia cha kwenda nacho shule ni shida mtu ananuna , nikiumwa mzee akinijulia hali ni matatizo yani hakuna jema yani wamama sijui huwa wapoje japo sasa nimekua binti mkubwa miaka 27 sasa lakini chamoto nilikiona katika makuzi yangu, mbaya zaidi ukute huyo mama awe na ndugu zake humo ndani yani unatengwa ka yai viza aisee watakuteta kiruga , watakusengenya yani matatizo juu ya matatizo. Du mhurumia huyo mtoto tena kama mama yake yupo mpeleke tu mimi mwenzenu sikua na pakukimbilia wala pa kupata unafuu
mama angu alfariki nikiwa nna umri wa miaka 2 tu. Ndio baba huwa wanajitahidi kukinga vifua lakini inafikia pindi nae anakua upande wa mkewe sasa sijui uwa ni limbwata cijui ni nini kwa kweli. Namhurumia sana mtotot hapa machozi yanilengalenga thread yako imenikumbusha mengi niliyopitia dah dunia hii! Tena sa nyingine utakuta anampelekea maneno ya uongo baba ako ilimradi tu mtoto uonekane mbaya yani mzazi kama hana akili ya kujiongeza utatembezewa fimbo kila siku. Yani kwa kweli baadhi ya mama zetu hawa wa kufikia watoto wao ndo huwa wanapenda wapewe kipaumbele mwenzangu na mimi unaonekana kama zombi hivi unawekea watu kiwingu. Nimesikitika sana pole sana mana nimekumbuka mbali.

Pole sana mkuu haya ndo maisha usipolelewa na mama yako ni shida jamani mi hadi naona huruma watoto wanapata shida hadi wanaathirika kisaikologia na kiakili.hi imetokea kwa wengi hadi rafiki yangu kupigwa bila sababu kuzushiwa uongo Mungu awasaidie wote wanaolelewa na mama wasio wao
 
Unachosema kaka hujakosea ila kumbuka mimi ni mkristo as you know ndoa zetu hazinaga taraka

Mkuu hebu acha kujitetea bwana, hebu nieleze ni ukristo gani unaruhusu manyanyaso kwa watoto?

Au huo ukristo wenu unafanya kazi kwenye suala la talaka tu na kwenye masuala mengine unawekwa kando?

na mbaya zaid nimesha zaa naye mtoto mmoja sasa huoni bado kuna tatizo la kuwatawanya watoto hapo pia mi bado kijana early 30's je nikioa mke mwingine nina uhakika gani kama hata kuwa kama huyu kwani hata mama wa mtoto wangu wa kwanza ashaolewa na mtu mwingine , yeye sikuwah kuishi naye before.

Nisome vizuri pale mwanzo, sikukueleza kuwa umpe talaka huyo mkeo bali nimekueleza kuwa kama huyo mwanamke hataki kumkubali mwanao kuwa sehemu ya familia basi yeye (huyo mwanamke0 atafute ustaarabu mwingine.

Kitendo hicho hakina maana yoyote wala hakikaribiani na talaka
 
Hata akimuonya haitasaidia wanawake wanakuwaga na roho mbaya ingawa wamezaa hata akimuonya atakuwa ana pretend tu ukiondoka mateso kama kawa huyo mtoto ampelekee kwa mamaake mzazi basi au boarding

Mama yake mzazi ameshaolewa na boarding schools huwa zina mwisho wake...

Sijui kama watu mnatalitambua hili kuwa kwa namna yoyote ile, kumtenga huyo mtoto kwa kuyafanya hayo mnayoyashauri kutaleta athari kwa mtoto kujiona kuwa anatengwa na wazazi wote wawili...

Siku zote mchawi mkabidhi mwana akulele, wa kudeal naye hapo ni huyo mwanamama mkorofi...
 
Back
Top Bottom